Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

tunataka mabadiliko bila sisi kuhusika , yani ni chadema, act, bunge la ulaya, tec, mpina, gwaji , na sasahivi tumemuweka mbele slowslow huku tukisubiri miujiza ipige kazi --- hatari sana hii mkuu
Kuna siku nilikuwa naongea na mtanzania mwenzangu huku Ujerumani. Nikamwambia ili tuendelee inabidi tufundishwe historia ya ulaya. Unajua wazungu wanaofanya kazi balozi zilizopo Tanzania wanatucheka sana. Yaani mambo ya kuipa dinj kipaumbele kuliko uanadamu ilikuwa miaka 600 iliyopita ulaya. Mambo ya kuwa machawa wa mkuu wa nchi ilikuwa miaka 500 iliyopita. Yaani nchi za kiafrika zinaishi miaka hiyo ya zamani. Ili zitoke huko lazima damu imwajike na nyingi sio ya kitoto. Hitler ndiyo aliyefanya leo hii Ujerumani ukisema uongo ni kesi kubwa sana.
 
Kuna siku nilikuwa naongea na mtanzania mwenzangu huku Ujerumani. Nikamwambia ili tuendelee inabidi tufundishwe historia ya ulaya. Unajua wazungu wanaofanya kazi balozi zilizopo Tanzania wanatucheka sana. Yaani mambo ya kuipa dinj kipaumbele kuliko uanadamu ilikuwa miaka 600 iliyopita ulaya. Mambo ya kuwa machawa wa mkuu wa nchi ilikuwa miaka 500 iliyopita. Yaani nchi za kiafrika zinaishi miaka hiyo ya zamani. Ili zitoke huko lazima damu imwajike na nyingi sio ya kitoto. Hitler ndiyo aliyefanya leo hii Ujerumani ukisema uongo ni kesi kubwa sana.
naam mkuu, huku bado mambo bado sana mkuu, to be fair hapa hata mimi nimeanza kubalance maneno mkuu 🤣

ila unachosema ndo uhalisia - bila sacrifice mambo yataendelea kubaki hivhivi tu na kuzidi,

maana ukiona watu wanachukua kadi za chama ili kulinda maslahi ujue tupo pabaya
 
Nimemsikiliza Mbowe vizuri kwenye mahojiano na muandishi wa habari juu ya kwenda kwake kwenye dira ya maendeleo. Binafsi sijaona neno lolote baya hata kwa yale aliyo yazungumza ,isipokuwa kuna watu ambao hawana uwezo wa ku raise issues isipokuwa wao wanasubiria matukio yatokee ndio na wao wapate chakuzungumza .
 
Yuko wapi Mzee wetu Cheyo aweke kaneno sisi tunataka pesa tu bana ahhhh am tired
 
Si mlimtukana matusi ya kila namna mkasema kanunulika, ngoja awaonyeshe sasa.Mliambiwa humu mpunguze ukali wa maneno, hamkuskia, matokeo yake ndo haya sasa

..Chadema walimtukana Mbowe.

..Ccm walimtukana, walimharibia mali zake, walimfunga, walimlipisha faini, walimfungulia kesi ya ugaidi.

..Kati ya Chadema na Ccm ni chama kipi kimemtendea ubaya zaidi Freeman Mbowe?
 
Hapana. Hawa ni watu Mbowe aliowapigania. Mbowe alikaa rumande na akafungwa jela pamoja na Heche katika kupigania maslahi ya chama. Heche aliposhindwa uchaguzi wa Uenyekiti wa Kanda Mbowe akamteua kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama. Mbowe alimpigania Lissu apelekwe nje ya nchi badala ya hospitali za ndani ya nchi. Lema alichukuliwa kama sehemu ya family ya Mbowe. Lakini wote hawa wakamchimba, wakaangalia bila kukemea wakati anazushiwa uongo na wafuasi wao. Hawa hawa walibeza mchango na umuhimu wa Mbowe hadharani. Hawa hawa ndio walichochea tuhuma za kuwa Mbowe amelamba asali na yuko mfukoni mwa Abdul. Hapana, usaliti waliomfanyia Mbowe hautasamehewa kirahisi. Hata kama Mbowe anaongea na Samia kumtetea Lissu hatawaambia maana wameisha dhihirisha unafik wao. Machozi ya mamba ya Lema hayatasaidia kitu. Badala ya kutafuta sympathy ya umma, wamfuate wakaongee nae na kumuomba msamaha kwa yote waliyomtendea. Kama hawaoni kama walimkosea, wamuache aendelee na maisha yake. Au wamfukuze tu kwenye chama.

Amandla...
Kwa hoja hizi mkuu Bado Sana, mbowe alichokifanya sio sawa, narudia tena Bora angekaa kimya.
 
Mbowe kazingua.Hata ndani ya CCM wanamchora kwamba jamaa sio🤔
 
Kwa kweli inahuzunisha sana. Mbowe amesababisha damu za vijana wengi zipotee, wakiamini wanapigania haki, kumbe mwenzao anawauza ili kujitafutia utajiri kupitia damu zao.

Uchaguzi hauwezi kuwa sababu ya Mbowe kufanya anayoyafanya sasa. Huyu kwa vyovyote hakuwa mpinzani wa kupigania haki, bali alikuwa mpinzani wa kutengeneza mazingira yatakayompa hela kutoka kwa watawala.

Ni aheri ameondolewa kwenye uongozi, sasa sura yake halisi inaonekana kwa kila mtu, hakuna anayeweza kudanganyika naye.
 
..Chadema walimtukana Mbowe.

..Ccm walimtukana, walimharibia mali zake, walimfunga, walimlipisha faini, walimfungulia kesi ya ugaidi.

..Kati ya Chadema na Ccm ni chama kipi kimemtendea ubaya zaidi Freeman Mbowe?
Siku zote matusi ya ndugu yako yanauma kuliko ya adui yako. Mbowe alitegemea na hakushangaa dhulma, uonevu, ukatili aliofanyiwa na CCM. Yote hayo yalimpa credibility kuwa yeye ni mpinzani kweli.

Lakini anaposimama mtu aliyekuwa Makamu wake, aliyekuwa mgombea wa urais, aliyepigwa risasi akiwa mnadhimu Mkuu wa upinzani na kusema kuwa chama chako kimejaa rushwa, kuwa umebadilika baada ya kuonana na Rais, pesa za Abduli zimepenya ndani ya chama na kuwa wewe ni muongo, watu watamuamini. Mtu huyo akiungwa mkono na wasaidizi wako wengine wa karibu ndio kabisa heshima na credibility yako itakuwa imetupwa. Watu hawa ni wabaya mara mia kuliko yule ambae inajulikana wazi hakupendi na hakutakii mema. Ndio maana kidonda walichokiacha kilikuwa kitahitaji muda na juhudi za dhati kabla hakija pona.

Amandla...
 
Mbowe kafanya hivi si kwa wakati sahihi lakini maneno yake Yana mashiko🤔
Screenshot_20250718-002741.png
Screenshot_20250718-002741.png
Screenshot_20250718-002828.png
Screenshot_20250718-002842.png
 
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA MBOWE!Mhe. Godbless Lema amemuandikia waraka Mhe. Freeman Mbowe. Kwa kuwa waraka huo umebeba maudhui yenye maslahi mapana, sisi tunauweka hapa kusudi kupanua wigo wa fikra.Je, nini kimekushangaza?

Je, nini maoni yako?Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula Itunge, Dar es Salaam; 17 Julai 2025; saa 2:50 usiku.Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe!Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu.

Sisi tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa wewe ni kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya wakati ulipokuwa Mwenyekiti wetu.Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku Mwenyekiti wetu,

Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.

Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbalimbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki.

Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.“Mungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.”Wagalatia 6:7Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi?

Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani.

Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano . Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.“

Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.” Mwanzo 4:10Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwa nini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki, maana hata kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu.

Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ? Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa.

Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma?“Dhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.”

- Nelson MandelaKwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba, usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini. Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko. Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.Huu si mwaliko wa ugomvi.

Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.“Haki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.”

Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali. Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya hakika.Godbless Lema, 17 Julai 2025
Nawashangaa sana ambao bado mnaamini kuwa dalali Mbowe alikuwa mpinzani.
 
Siku zote matusi ya ndugu yako yanauma kuliko ya adui yako. Mbowe alitegemea na hakushangaa dhulma, uonevu, ukatili aliofanyiwa na CCM. Yote hayo yalimpa credibility kuwa yeye ni mpinzani kweli.

Lakini anaposimama mtu aliyekuwa Makamu wake, aliyekuwa mgombea wa urais, aliyepigwa risasi akiwa mnadhimu Mkuu wa upinzani na kusema kuwa chama chako kimejaa rushwa, kuwa umebadilika baada ya kuonana na Rais, pesa za Abduli zimepenya ndani ya chama na kuwa wewe ni muongo, watu watamuamini. Mtu huyo akiungwa mkono na wasaidizi wako wengine wa karibu ndio kabisa heshima na credibility yako itakuwa imetupwa. Watu hawa ni wabaya mara mia kuliko yule ambae inajulikana wazi hakupendi na hakutakii mema. Ndio maana kidonda walichokiacha kilikuwa kitahitaji muda na juhudi za dhati kabla hakija pona.

Amandla...

..nimekuelewa.

..kidonda cha Mbowe kilichotokana na Ccm kimepona.

..kidonda cha Mbowe kilichotokana na uongozi mpya wa Chadema hakijapona.
 
Mbowe anawapa wakina Lema darsa la bure la siasa. Unachagua vita yako hasa kama katika nafasi ya uonge.
Mbowe alipotoka rumande alikubali mualiko wa Samia akaenda moja kwa moja. Baada ya kikao chao wakapiga picha ya pamoja na kutoa tamko kuhusu umuhimu wa haki. Hakuonyesha kinyongo kwa uonevu aliofanyiwa.

Baada ya kikao yakaanza mazungumzo kuhusu maridhiano. Matokeo ya mazungumzo hayo wakina Lissu wakaweza kurudi nyumbani, wafuasi wa Chadema wakaachiwa na mikutano ya hadhara ikaruhusiwa. Yote haya yasingetokea kama Mbowe angekataa kuonana na Rais.

Lema hapa anamlaumu Mbowe kwa kuitikia mualiko wa Rais kwenda Dodoma. Alitaka awe mstari wa mbele kuikemea serikali na angekuwa mahakamani siku zote ambazo kesi ya Lissu inapo sikilizwa. Angependa angeshinda Maria Space akirushia madongo serikali kwa imani kuwa hiyo ndio namna pekee ya Lissu kutoka rumande.

Badala yake Mbowe ameenda Dodoma. Ameshikana mkono na Rais na Rais amempa heshima ambao wengine hawakupewa. Matokeo ya haya ni Lissu kuachiwa kwa sababu tu Samia anamheshimu Mbowe kwa sababu ingawa ni mpinzani ameendelea kumpa heshima yake.

Mbowe anajua hii ni term ya mwisho ya Samia na akicheza karata zake vizuri Samia ataridhia mabadiliko ya Katiba ili ajenge legacy yake.

Amandla...
 
Hilo jitu ni lisaliti toka kitambo.
Asubuhi yuko chadema, usiku yuko ccm.
 
..nimekuelewa.

..kidonda cha Mbowe kilichotokana na Ccm kimepona.

..kidonda cha Mbowe kilichotokana na uongozi mpya wa Chadema hakijapona.
Kidonda cha CCM hakijapona. Anameza panadol anasonga mbele.

Kidonda cha wakina Lissu hakitapona kirahisi. Hasa wanavyoendelea kunyamazia matusi na kebehi za wafuasi wao.

Unakumbuka John McCain alivyomkemea yule mama aliyedai kuwa Obama hana mapenzi na Amerika wakati wanagombea urais? Kitendo kile kilimjengea heshima kubwa na shukrani kutoka kwa wakina Obama.

Kama Lissu ange simama na kumtetea Mbowe dhidi ya matusi yote yanayoelekezwa kwake, angesaidia sana kuponya jeraha alilosababisha.

Amandla...
 
Back
Top Bottom