Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Na msemaji wa jeshi anasema HAWAJUI YATAISHA SAA NGAPI... Yaani ni kungoja kudra za M/MUngu....! Sitaki hata ku-imagine wakina mama na watoto wana hali gani jamani...

mmnh!Tanzania bwana kila kitu ni kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu,bah!
 
ahhh waaache kula kuku wawaze kukusaidia wewe wa mabomu?
Wao wamesema mtoke hapo ..MUENDE WAP NI KWAMBA MTAJIBEBA..MTAJIKUSANYA...haman ndg anayeish kgambon?au kunduchii?utajibeba...yaan nataman kulia..mtu na familia yake usiku u ataenda wap jaman?nyumba zmebomoka msaada apo wataupata afta semester....si leo ata kdg...na mvua hii jamani, na usiku u? Eeh Mola tusaidie
Jamani, mnakumbuka mwinyi alisema atajiuzulu? Khe khe.... Hafanyi hihyo.... Ni kinyume na maumbile
 
Tuendelee kuomba maana kuna mtu nimeongea nae kutoka airport anasema hajawahi kuona kama hiyo watu ni wengi sana wanaotembea
 
Serikali na Jeshi la Tanzania nao ni punda kabisa. Mtatunziaje silaha kubwa kama mabomu hayo mijini? Kwa wenzetu hata duka la baruti za sherehe (fireworks) haliwekwi mjini, sasa iweje mabomu ya kivita eti yatunziwe mjini?

Mwaka jana kuna yaliyolipuka huko Mbagala, na na bado eti viongozi wetu hawakuona umuhimu wa wa kubadilisha sehemu ya kutunzia mabomu. Tunajifunza nini? Sana sana nadhani mabomu hayo ni yale yaliyoachwa na Nyerere takribani miaka 30 iliyopita sasa yameanza ku-expire, ndiyo maana yalipuka yenyewe.

Ni majuha tu hakuna akili kule!
 
Sasa hivi tangazo limetoka wananchi wanaokaa Gongo la Mboto wahame, Wahamie wapi, kwa njia ipi, hakuna anayetoa maelezo. Hatujifunzi wala hatuna mbinu za kukabiliana na majanga.

Milipuko ya Mbagala Serikali walisema RAIA WALIJENGA KARIBU NA MAENEO YA JESHI KWA NGUVU NA WAKASHAURIWA WAHAME.
  1. Je,kwako Mhe. Dr. Mwinyi Waziri wa Ulinzi HAWA RAIA WA GONGO LA MBOTO NAO WAMEHAMA KUYAFUATA MABOMU AU MABOMU YAMEWAFUATA RAIA?????
  2. Kama milipuko ya Mbagala mliona TATIZO NI RAIA KUWA KARIBU NA MAENEO YA JESHI KWANINI HAMKUWAHAMISHA RAIA WOTE WALIOKARIBU NA MAENEO YA JESHI HASA MAGHALA YA JESHI(ARMOURY)?
Tunataka KESHO ASUBUHI UTANGAZE KUJIUZULU KAZI YA JESHI IMEKUSHINDAAAAAAAAAAAAAAAAAA!
Tunakuomba kwa heshima na taaadhima ujiuzulu kufuata nyayo za Babako mzee Mwinyi aliyejiuzulu miaka ile ya 70s kuwajibika alipokuwa Waziri wa Mambo ya NDANI. Itakujengea heshima kama babako na pengine ukaukwaa Urahisi wa Zanzibar na baadaye Bara kama babako.

Kazi kwako.



 
hivi hapa tbc1 wanaposema wananchi waondoke mbona hawasemi wameandaa kambi ya dharura wapi? .hivi mtu aondoke sasa hivi jamnai aende kulala wapi wakati hata hela ya gesti au kuchukua atm card hawezi kutokana na kukimbia. Hivi tunawapeleka wapi watanzania? Jamani.

Usishangae ndio kwanza jk anavuta shuka huku akimtuma mwinyi akaangalie ili aje kuzungumza kwenye hotuba ya kufunga mwaka 2011
usiku huu sijui wanataka watu waende wapi-utakuwa mgeni wa nani usiku huu-maana unaweza fika ukamkosa-nae alishakimbia
 
Huyu mtoto wa mwinyi sasa imefika wakati wake wa kutuachia wizara yatu
 
Anasemaje??

Kwa bahati mbaya ameeleza tu jinsi watu walivyopaniki, wamama wanalia wanakimbia na watoto wao, mmoja amehojiwa anasema ameacha kila kitu amekimbia na watoto wake kutoka gongo la Mboto hadi uwanja wa ndege. Bado anajitaidi kujisogeza karibu na eneo la tukio kama ataweza!!!
 
Yaani ule upuuzi wa Mbagala umejirudia????
Vipi kuhusu INTELIJENSIA YA IGP MWEMA haijaweza kubaini hiyo milipuko???
Vipi kuhusu ULINZI shirikishi???
Yaleyale ya RICHMOND/DOWANS,umeme wa DHARURA. Kila kitu ni dharura kwa Tanzania.

Hapo ndipo tunapozidi kujua UDHAIFU WA SERIKALI YA CCM. Kuwa hawa jamaa hawana akili kabisa na wala huwa hawapendi kufikiri. Kwanini baada ya matukio ya Mbagala hawakuchukua TAHADHARI ya kufanya ukaguzi wa ARMOURY ZOTE KAMA KUNA HATARI MILIPUKO MINGINE KAMA HII??

Safari hii tunataka WATU TUANDAMANE NCHI NZIMA KUSHINIKIZA DR. MWNYI ajiuzulu. Last time Mbagala alikomaa kuwa HAWEZI KUACHIA NGAZI. This time tuseme basi!!!!! You poor Tanzanians wake up please! Acheni kuzubaa,watakaouwawa na hayo mabomu ni ndugu zenu,jamaa zenu na rafiki zenu!!!

ANGALIZO: Nahisi kama vile kuna njama ya kulipua makusudi haya MABOMU ili kuwafanya Watanzania wasahau sakata la DOWANS NA MGAWO. Kwamba wakti watu wanatafakari hayo Maboumu ya G/Mboto MAFISADI WAPATE NAFASI YA KUKAMILISHA MIPANGO YAO YA KULIPA ILE 94b/=kwa DOWANS na wakti huohuo WAKIENDELEA KUWASHA MITAMBO YAO(DOWANS)!!!!!!

Tuna serikali ya kuchekeana sana na wananchi pia ni waoga sana.Watu watakufa, mali zao zitaharibiwa na shida zote hizo mawaziri wahusika wataleta porojo na kuendelea kushika madaraka kama vile haiwahusu.This got to end.Waziri lazima ajiuzuru manake mabomu katika makazi ya watu ni kujitakia kifo tu.Kwani kambi zilizoko mbali na miji haziwezi kuhifadhi mabomu?
 
Nitashangaa kama baadhi ya watu hawataachia ngazi hata kwa jambo kama hili. Ni maboom yanaendelea kulipuka hadi sasa. Eti wanatushauri tukakae mabondeni wakati hata hawasemi yataisha saa ngapi. Jamani hii ni serious sana wananchi hawana cha kufanya wala hamna directions zozote za maana kutoka kwa wahusika.
 
oh dear! tena? ... shimbo atatumaliza. imefika wakati hizi kambi za jeshi zilizopo dar zigeuzwe open spaces/malls/mashule
 
Tulianza na serikali na sasa sina imani n jeshi letu wananchi yaan JeiWii au JWTZ. Siamini kabisa kama hawa watu wanaoshindwa kuntrolsiraha kama wana uwezo wa kutulinda sisi wananchi!


Hivi mkuu leo ndo umejua hatuna jeshi? Tuna majuha na mabaradhuli; watu wanaofikiri jeshi maana yake ni kutishia raia. Hukumbuki maneno ya mp.........vu shimbo wakati tunaelekea uchaguzi mkuu. Hilo ndo jeshi letu ujue sasa.
 
Mabomu yanalipuka Gongo la Mboto polisi....

Taarifa zaidi kufuatia.

UPDATES: (by Invisible)

1. Hali ni mbaya jijini Dar, nyumba zinabomoka, watu wanakimbia ovyo!

2. Barabara ya Nyerere haitembei (kama unafikiria kwenda uwanja wa ndege ahirisha mapema), magari yameingiliana watu wanakimbia ovyo mitaani na barabarani kulikimbia eneo la maafa.

3. Dalili zinaashiria mabomu ni mengi zaidi na milipuko itaongezeka, kuna uwezekano wa kupoteza raia na watumishi (wanajeshi) wengi kufuatia milipuko hii

4. Watu kadhaa wamekufa kwa kugongwa na magari

5. Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Abdulrahman Shimbo amesema:

"Hali ni mbaya Kikosi namba tano maghala yamelipuka ni hatari, watu wahame, maghala yako karibu karibu sana, tunaomba wananchi wahame sasa hivi, tunajitahidi kuzuia moto unaotokana na hilo unaweza kwenda mbali sana hadi Kilomota kumi, wananchi walioko karibu na maghala ya kikosi Gongo la Mboto wasogee mbali sasa hivi.

mimi naishi huko na namshukuru Mungu nimeiokoa familia, WANAJAMII SIJIELEWI NA HALI NI MBAYA SANA, TUWAOMBEENI WENZETU. NIMEENDESHA GARI BILA KUJIELEWA KUIOKOA MY FAMILY,, TUONEENI HURUMA. nchi hii siielwewi kabisa.
am strongly condemning to the current govt of Tanzania kwa adha iliyotufika.
 
Jamani, mnakumbuka mwinyi alisema atajiuzulu? Khe khe.... Hafanyi hihyo.... Ni kinyume na maumbile

duu kinyume na maumbile\?
navuta taswira nione iyo kinyume na maumbile yake ikoje...
 
Hivi tv zetu haziwezi kukatisha matangazo na kutangazia wananchi hali tete hii?


serikali sasa inabidi itambue kuwa hakuna aja makambi ya kijeshi kukaa maeneo mjini: Ya mbagala tuliiona madhara yake na leo ya gongolamboto tunaona. Serikali inasubiri nini?
 
Intelejesia iko wapi bana,mi nilifikiri yale ya Mbagala yasingetokea tena kumbe wapi watu kumbe bado walikuwa wanafikiria njia mbadala za kushinda uchaguzi kwa kishindo na kujidowans

Intelijensia inaihusu Chadema tu isichukuwe nchi kwa kuandamana.
 
Back
Top Bottom