Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

I see, mpaka yakija kuisha itakuwa balaa...HIvyo ninavyoyasikia, niko maeneo ya Makongo Juu lakini nyumba yote inatikisika... Nilikuwa na ki-wine changu kichwani chote kimeyeyuka, du! Leo ni kulala na jeans, yasijeruka mpaka huku. Mungu wasaidie ndugu zetu wa huko madhara yasiwe makubwa sana.

Kwakweli wine lazima iishe kichwani. Wanatuharibia maulid ye2. Mungu atuepushie balaa hili
 
mkuu ... hizi ni nini ..au unaongea huku unakimbia mabomu

mkuu zaidi, umenichekesha sana, na nimependa umakini wako... Maana hata mi skumwelewa nikopita tu! Inaonekana alkua kwny mbio au kilaji imekaa mahali yake wakati huu.

Ila ni hatari kwa nchi, kwa mara ya pili, kutokuwa makini na usalama wa raia wake. Mbona intelijensia zinazogusa maslah yao moja kwa moja km AR wanaRESPOND haraka ivo?

Imenipa sababu ya kupinga nchi kuwa na mabomu na energy za Nyuklia ovyo ovyo. Imajin yangekua manyuklia tumeshindwa yatunza namna iyo?
 
Sasa nadhani na jeshi inabidi liangaliwe kwa macho mawili... uchakachuzi kila sehemu!!!!
 
Kama moja lingeruka kuelekea Ikulu ndio wataanza kuya shughulikia lakini kama yanaruka kuelekea nyumba za Raia duh hawana wasiwasi hawa-jaama hawafai hata kidogo.
 
msemaji wa jesh toka g'mboto anasema maboni yamo mengi galani na yanaweza kulipuka hadi mpaka kesho.....
 
Mie nipo hapa mazimbu mara ya kwanza ni kishindo kiligonga radi c radi lakini milio iliyofuata ni kawaida ndo hapo nika associate na hyo taarifa maana c kawaida may be tusuburi asubuhi watasema nini.
 
There are currently 648 users browsing this thread. (220 members and 428 guests)

Kweli nimeamini JF inaongoza kufikisha ujumbe kwa waTZ
 
hakuna aliyefanikiwa kufika eneo la tukio hadi sasa hivi, kuna jamaa wa redio one wanasema wako njiani kuelekea huko labda tuwasubiri. Lakini hali ni mbaya kwa kuisikia tu huku mbali hivi!!


weeeeeee redio 1 ndio wa kujitoa muhanga acha kabida hapa tutapewa habari baadae sana hamna wa kusogelea hapo kamwe
 
wakubwa napata habari hapa Radio Free Africa kwamba mabomu yamelipuka gongolamboto kambi ya jeshi walio hko watujuze, nasikia ni kama movie watu wanakimbia huku na huko, kama kuna mdau huko atujuze

BEAST,DUDE la Edward Lowassa na Basha wake Rostam Aziz linakusanya Silaha kali Tayari kwa atakaye leta Fyoko 2015.
Kaeni mkao waa Kukimbila Ughaibuni.
 
Sasa wahame tu au serikali inafanya nini kusaidia kuwaondoa hapo ???
Hii nchi full usanii na viongozi (sorry watawala) wetu hawana maana...
ahhh waaache kula kuku wawaze kukusaidia wewe wa mabomu?
Wao wamesema mtoke hapo ..MUENDE WAP NI KWAMBA MTAJIBEBA..MTAJIKUSANYA...haman ndg anayeish kgambon?au kunduchii?utajibeba...yaan nataman kulia..mtu na familia yake usiku u ataenda wap jaman?nyumba zmebomoka msaada apo wataupata afta semester....si leo ata kdg...na mvua hii jamani, na usiku u? Eeh Mola tusaidie
 
Shimbo amethibitisha kutokea kwa milipuko ya mabomu huko Gom's kwenye kambi ya jeshi, ghala no 5 la silaha. Amewaomba wanaoishi jirani wahame kwani hali ni mbaya.

SOURCE TBC TAIFA.

Kwanini wasiende kusaidia wananchni huko!!
 
Hii ndo bongo bwana, kila kiongozi msanii, sijuhi hii nchi inaelekea wapi?
 
Matangazo yanaendelea kutolewa TBC na ITV watu waondoke majumbani kwa kuwa haijulikani milipuko itaisha sa ngapi

QN: Waondoke waende wapi?

Hapo sasa......hivi mbona tunasikiaga mijikozi kibao ikiendeshwa ya Risk Management sijui na Emergency hivi kweli hakuna kikosi cha majanga ya dharura? Unapomwambia mtu usiku huu aondoke kwake na familia yake aende wapi?? .....................
 
Back
Top Bottom