Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Jamani this is so scaring...yaani nimeogopa utafikiri nipo maeneo ya karibu... jamani pole ndugu zetu. Tunawaombea Mungu awalinde, mtoke salama!!!
 
mitambo ya dowans si iwashwe jamani!?

umeme amna.

apoapo mabom.

duh!
 
Sasa hivi tangazo limetoka wananchi wanaokaa Gongo la Mboto wahame, Wahamie wapi, kwa njia ipi, hakuna anayetoa maelezo. Hatujifunzi wala hatuna mbinu za kukabiliana na majanga.
 
poleni sana ndugu na jamaa wa maeneo hayo Mungu awalinde mnapokimbilia muwe salama.
 
Kama kuna wadau walio karibu huko naomba wachukue picha za kutosha then hata kesho mungu akipenda waturushie hapa

Jamani watu wanaogopa usalama wao...kama wanasema yanaruka kwenda mbali....nani ambaye atasogea karibu kupiga picha????
 
Hali ni mbaya watu wanakimbia hovyo, emergency team iko wapi? So sad kwa watoto na wamama.
 
Shimbo amethibitisha kutokea kwa milipuko ya mabomu huko Gom's kwenye kambi ya jeshi, ghala no 5 la silaha. Amewaomba wanaoishi jirani wahame kwani hali ni mbaya.

SOURCE TBC TAIFA.

Na msemaji wa jeshi anasema HAWAJUI YATAISHA SAA NGAPI... Yaani ni kungoja kudra za M/MUngu....! Sitaki hata ku-imagine wakina mama na watoto wana hali gani jamani...
 
Dah!Hatari tupu!Natumaini watu wamenusurika!Kweli serikali yetu sijui inafanya nini mpaka mabomu yanalipuka tu hovyo mitaani!
 
walinzi wa ulinzi mtoto wa mwinyi baada ya yaliyotokea mbagala alituambia mabomu kwenye magala yote ya jeshi yataangaliwa,,, sasa kafanya nini?

serikali ya michakato inayoendelea mpaka lini? Wale wa mbagala mpaka leo wengine wanaishi maishi ya ukimbizi sasa hawa wengine kama kutatokea maafa itakuaje?
 
Kibonde anasema hali ni mbaya sana na anawasihi wale wote wenye ndugu zao maeneo hayo wasiende kwa sasa hivi. Na ameambiwa (habari zisizothiditika) kuwa basi moja lililokuwa na abiria limelipuliwa na mojawapo ya mabomu.
 
Poleni sana wote mliokumbwa na hili janga ushauri mlio karibu kimbieni na muende mbali

Inabidi vitu kama hivi vikae mbali sana na makazi ya raia (nilidhani tumeshajifunza na majanga yaliyotukumba kabla)

Shenzi zao kabisa hawajifunzi! Na hakuna maghala ya mabomu huko wanakoishi hao wakubwa. Shenzi kabisa!
 
walinzi wa ulinzi mtoto wa mwinyi baada ya yaliyotokea mbagala alituambia mabomu kwenye magala yote ya jeshi yataangaliwa,,, sasa kafanya nini?

serikali ya michakato inayoendelea mpaka lini? Wale wa mbagala mpaka leo wengine wanaishi maishi ya ukimbizi sasa hawa wengine kama kutatokea maafa itakuaje?

Wauaji wakubwa shenzi zao!
 
weeeeeee redio 1 ndio wa kujitoa muhanga acha kabida hapa tutapewa habari baadae sana hamna wa kusogelea hapo kamwe

Deogratius Rweyunga wa Redio one anaongea kutoka huko msikilize sasa!!
 
walinzi wa ulinzi mtoto wa mwinyi baada ya yaliyotokea mbagala alituambia mabomu kwenye magala yote ya jeshi yataangaliwa,,, sasa kafanya nini?

serikali ya michakato inayoendelea mpaka lini? Wale wa mbagala mpaka leo wengine wanaishi maishi ya ukimbizi sasa hawa wengine kama kutatokea maafa itakuaje?
Waziri sio Walinzi...
 
Sasa hivi tangazo limetoka wananchi wanaokaa Gongo la Mboto wahame, Wahamie wapi, kwa njia ipi, hakuna anayetoa maelezo. Hatujifunzi wala hatuna mbinu za kukabiliana na majanga.
Eti msemaji wa jeshi kasema wakae maeneo ya mabondeni, mh! Source: Channel 5
 
Back
Top Bottom