Gairo: DC amtuhumu mwenyekiti wa CCM kuhongwa gari na mbunge Shabiby, mwenyewe akana asema amenunuliwa na Dkt. Mwigulu. Kesi iko Takukuru

Shabiby kaa mbali na huyo mwanamke. Ni mchepuko wa boss mkubwa. Achia ubunge na kila kitu. Endelea tu na biashara zako.

Huu ni ushauri wa bure, utafilisiwa, utasingiziwa kesi na ubunge utakosa.

USIJE UKASEMA SIKUKUAMBIA!.
 
Pamoja na yoote hayo naomba kwa leo tuyaache hadi baada ya siku 7 ili tuendelee kutafakali hotuba ya rais mtarajiwa mh Lissu
Mkuu wa wilaya ya Gairo amemtuhumu mwenyekiti wa CCM wa wilaya kwamba amehongwa gari na mbunge Ahmed Shabiby ili wambebe kwenye uchaguzi. Mkuu wa wilaya amewataka Takukuru wamshughulikie mwenyekiti huyo.

Naye mwenyekiti wa CCM amesema gari hilo hajahongwa na Shabiby kama inavyodaiwa bali amenunuliwa na waziri wa Katiba na sheria Dr Mwigullu Nchemba. Mwenyekiti amesema yeye pia ni msaidizi wa Dkt. Mwigulu jimboni Iramba akisimamia mahusiano ya mbunge na Waislamu hivyo amenunuliwa gari hiyo kama kitendea kazi.

Kuhusu kuchunguzwa mwenyekiti amesema ni kweli aliitwa Takukuru wilayani na wakamwambia tuhuma hizo ni za kisiasa hivyo jalada limepelekwa Dodoma ambako alihojiwa Ijumaa iliyopita na sasa anasubiri majibu.

Mwisho mwenyekiti amebainisha kuwa mkuu wa wilaya ni mtu mkorofi na kwamba anataka kugombea ubunge wa jimbo hilo na kila wakati amekuwa anawatisha kwamba yeye ana ulinzi wa kigogo aliye juu.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!
Screenshot_20200608-210107.jpeg
 
Huyo ashapewa mrungula na kuchikuchi hota hai
... kwa tuhuma hizo yeye DC, Shabiby, Mwigulu, na huyo Mwenyeki wa CCM (W) wanatakiwa "kuchinjiwa" mbali kabisa huko wafutwe kabisa uanachama. Akisimamia "mahusiano na waislamu"! Kuna cheo cha aina hiyo siku hizi hadi kununuliwa gari la kutekeleza jukumu hilo?
 
Shabiby kaa mbali na huyo mwanamke. Ni mchepuko wa boss mkubwa. Achia ubunge na kila kitu. Endelea tu na biashara zako.

Huu ni ushauri wa bure, utafilisiwa, utasingiziwa kesi na ubunge utakosa.

USIJE UKASEMA SIKUKUAMBIA!.

Kakosa sifa kitambo sana ubunge sio ajira ya kudumu , akae pembeni aendelee na bziness
 
Back
Top Bottom