Furaha ya maskini ni kusikia tajiri kapata matatizo na si kuona umaskini unaondoka katika maisha yake.

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
Maskini ni kama mchawi tu maana hupenda sana habari mbaya.
Tena ukitaka afurahi zaidi asikie kuwa tajiri kafilisika, Boss kashushwa cheo. Hata wenyewe maskini hawapendani hasa pale maskini mmoja akionekana kupata chochote kitu.
Magufuli aliijua hii kanuni, akaanza kuwasumbua matajiri. Mioyo ya maskini ilifurahi sana bila kujali kuwa tajiri hawezi kafilisika kwa kiwango cha 0°.
Maskini walifurahi Magufuli alipowatumbua mabosi ambao walikuwa hawamtukuzi yeye na utawala wake, maskini walifurahi sana bila kujali kuwa zile nafasi hawatazirithi wao.
Magufuli mpaka kesho analiliwa na maskini , ukiwauliza kwanini mnampenda sana utawasikia eeh alikuwa mtetezi wa wanyonge, aliwanyoosha mafisadi . Kama alikuwa mtetezi wa wanyonge , je, miaka 6 ya utawala wake aliuondoa unyonge(umaskini) kwa Watanzania wangapi?
Aliongeza ufukara na umaskini miongoni mwa Watanzania maana wengi walikosa kazi kwakuwa mwajiri mkubwa (private sector) alimuua kwa mgongo wa kumnyoosha
Maskini wanaamini matajiri ni wezi wa pesa zao.
Maskini akisikia mtoto wa jirani kafeli form four moyo wake unakuwa mweupe hata soda anaweza kukununulia.
Roho ya "tukose wote" ni roho ya kichawi.
Maskini anafurahia tajiri kufungwa na kufilisiwa bila kujali kuwa bilionea mmoja analisha familia zaidi ya 1000 direct or indirect.
Ushauri : Tumia njia yoyote ila kuukimbia umaskini . Sijasema uue.
 
Kabisa mkuu, hii ni sadaka muhimu umetoa leo.

Hata humu jf, hebu angalia hawa maskini wanavyohangaika kurusha threads kila sekunde wakionyesha matamanio yao ya kuona Mama Samia anashindwa katika suala la bandari. Si kingine kinachowasumbua bali ni umaskini tu unaoambatana na pepo chafu ulilosema mtoa mada.
 
Unajadili jambo ambalo halipo kwenye mjadala.

Wewe chawa, Prof. Shivji ni maskini Kama wewe?

Shenzi sana.
 
Maskini ni kama mchawi tu maana hupenda sana habari mbaya.
Tena ukitaka afurahi zaidi asikie kuwa tajiri kafilisika, Boss kashushwa cheo. Hata wenyewe maskini hawapendani hasa pale maskini mmoja akionekana kupata chochote kitu.
Magufuli aliijua hii kanuni, akaanza kuwasumbua matajiri. Mioyo ya maskini ilifurahi sana bila kujali kuwa tajiri hawezi kafilisika kwa kiwango cha 0°.
Maskini walifurahi Magufuli alipowatumbua mabosi ambao walikuwa hawamtukuzi yeye na utawala wake, maskini walifurahi sana bila kujali kuwa zile nafasi hawatazirithi wao.
Magufuli mpaka kesho analiliwa na maskini , ukiwauliza kwanini mnampenda sana utawasikia eeh alikuwa mtetezi wa wanyonge, aliwanyoosha mafisadi . Kama alikuwa mtetezi wa wanyonge , je, miaka 6 ya utawala wake aliuondoa unyonge(umaskini) kwa Watanzania wangapi?
Aliongeza ufukara na umaskini miongoni mwa Watanzania maana wengi walikosa kazi kwakuwa mwajiri mkubwa (private sector) alimuua kwa mgongo wa kumnyoosha
Maskini wanaamini matajiri ni wezi wa pesa zao.
Maskini akisikia mtoto wa jirani kafeli form four moyo wake unekuwa mweupe hata soda anaweza kukununulia.
Roho ya "tukose wote" ni roho ya kichawi.
Maskini anafurahia tajiri kufungwa na kufilisiwa bila kujali kuwa bilionea mmoja analisha familia zaidi ya 1000 direct or indirect.
Ushauri : Tumia njia yoyote ila kuukimbia umaskini . Sihasema uue.
Ujengewe sanamu, hata asilimia kubwa wanaompenda dikteta mmagufuli ni mafukara
 
Unajadili jambo ambalo halipo kwenye mjadala.

Wewe chawa, Prof. Shivji ni maskini Kama wewe?

Shenzi sana.
Huna akili wala busara, katika nyie 20 mnaopinga ukimtoa prof shiv si mnabaki 19 maskini hohe hahe. Sasa hapo si ni sawa na wote tu maskini watupu. Unabisha nini sasa?

Unaniambia najadili ambalo halipo kwenye mjadala, hv mjadala uliopo ni upi kama sio athari za umaskini zinazowakabili?!!!! Mimi nimejadili nini kama sio umaskini wenu unavyowapatia roho mbaya. Tena wewe ndo inaonekana umaskini umekukula kwelikweli.
 
Pole sana
Mungu kauponya moyo wako , utazidi kubarikiwa.
Maskini ndio Ibilisi, Ibilisi ndio maskini

Sandali Ali leo umenena. Nilipovunjiwa nyumba zangu pale Kimara Temboni 14/09/2017 na serikali ya awamu ya tano, maskini walifurahi Sana, tingatinga lilipokua linavunja vitu vyangu ndani, matenki ya maji nje. Walikua wanachekelea. Cha ajabu Leo Nina nyumba nyingine nzuri zaidi wao wako pale pale.
 
Back
Top Bottom