Fundi simu anahitajika, nina ofisi nahitaji fundi

The bump

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,136
1,952
Fundi simu anahitajika kama kichwa ya habari inavyosema hapo juu,fundi ninae muhitaji ni fundi makini,anaejua kazi,anaejua majukumu ya kazi yake Maeneo yote mawili software na hardware.

Japo matatizo ya software sio mengi lakini fundi mwenye anajua basic tips za kuondoa FRP,FLASHING TOOLS,nk na alie iva HARDWARE atafaa sana.

OFISI ipo mbezi mwisho,inajihusisha na uuzaji wa vifaa vya umeme na huduma nyingi ndani yake na moja ya huduma ninayotaka kuitoa ofisini ni ya Ufundi SIMU.

Fundi unaekuja vitu nitakavyokufanyia kwa makubaliano maalumu.

Kukununualia vifaa vyote muhimu vya kazi yako (Vyote Vyote)
Kukuwekea ofisi katika hali nzuri classic na usasa zaidi

Fundi njoo na idea tu,mambo mengine yanayotaka pesa,ofisi iweje,nini kinunuliwe nini kisinunuliwe Nitakua pembeni yako kukutimizia.

MALIPO

Sikulipi ila utanilipa kulingana na ulivyofanya kazi,napokea malipo ya siku siku ila baada ya mwaka tutakua tunalipana kodi ya miezi 6 na kuendelea.

Mwanzo huu sitokulipisha kodi wala malipo yoyote kwani ndio tunatafuta wateja na jina kwanza hivyo utakachopata kitakua chako na familia yako kwa miezi mi 3 ya mwanzo.

Miezi mi 3 ya mwanzo kwakua kutakua hamna wateja na hatujajulikana ubora wetu Ofisi itakupa chakula milo mi 3 asubuhi mchana na usiku + Nauli ya kuja kazini na Kurudia. KWA MIEZI MI 3 YA MWANZO ufanye kazi usifanye kazi.

FUNDI natamani Fundi anaejitambua aneweza tatua na kutengeneza simu BRAND KUBWA KUBWA na kwa ubora hasa kwenye upande wa vioo,touch,nk.

WE Deal with only BIG BRANDS SMARTPHONES na nyinginezo ila zaidi zaidi wateja walengwa ni wale wanaomiliki Simu za Gharama na za pesa Nyingi ambao wamekosa Mafundi bora wa simu zao kwa viwango vya hali ya juu.

Natamani mafundi WAWILI tu kwa yeyote anaemjua fundi bora sana hata kama yupo mbali ila mna mkubali kwa kazi zake naomba niunganishwe nae,

incase wakikosekana mafundi bora nitatumia mafundi bora huko walipo kuwapelekea kazi aAttach filesu kuja fanya kazi hizo ofisini kwa makubaliano maalumu.

Karibuni na asanteni kwa nyote mtakaonisaidia fanikisha hili.
 
Ungeweka Dials mkuu +255 kuja PM usumbufu, weka hata namba ya ofisi
 
Back
Top Bottom