Nahitaji fundi mzuri wa Fanicha (Furniture)

be unique

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,375
2,274
Habari wakuu,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, nahitaji kupata fundi wa fanicha za ndani na awe na utundu wa ubunifu wa vitu mbalimbali vya ndani (fanicha).

Ofisi inauza vitu used pamoja na fanicha,kuna muda fanicha zinakuja zinahitaji marekebisho kwahiyo inahitajika kuwepo na fundi.

Na kuna muda oda zinaletwa na wateja au ofisi inataka kutengeneza vitu fulani kwa ajili ya biashara kwaiyo inahitajika kuwepo na fundi.

Kuhusu malipo ni kila kazi atakayofanya inakuwa na pesa yake tayari, sio mpaka kitu kiuzike ndio alipwe kama fundi ila kila kazi atakayofanya atakuwa anapata malipo na biashara zikiwa zinaenda vizuri atakuwa anapata pesa ya ziada kama motivation.

Ningependelea awe mtu ambaye anajitafuta zaidi maana ofisi ipo (frame) ila ningependa awe anaishi hapo hapo kulingana na usalama wa eneo uwe mkubwa zaidi.

Ofisi ipo kigamboni ferry. Sichugui sehemu ambayo anatokea muhimu tufanye kazi kwa malengo.

Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom