Fumbo la Eden! Nani aliwaambia wako uchi?

Fumbo la Eden! Nani aliwaambia wako uchi?

Kuna mtu aliwahi kuniambia maneno ya kwenye biblia na msaafu ni maneno yaliyoandikwa na wanadamu kwa kuangalia mambo yote ya kistaarabu yafuatwe/yafanywe na yasiyo ya kistaarabu yaachwe kwa kuyawekea faida yaliyo mazur na hasara yaliyo mabaya ili tuwe safi mbele ya binadamu na mbele ya mungu pia,mfano ukiangalia amri kuu za mungu zile usiibe,usiseme uongo,usizini e.t.c ni maneno yakufanya tuwe wastaarabu.
Hivyo ndo nlivyoambiwa lakini za kuambiwa changanya na zako.....
 
Bible ni neno linaloishi sio utunzi wa kibinadamu ule
 
Mtazamo wangu;Kwanza hadithi hii ya uumbaji ni hadithi tu.Tunda ni tunda tu na ililenga kuonyesha uumbaji wa Mungu na ilikuwa ni hadithi kwa ajili ya watoto na sio kwa ajili ya watu wazima wenye ndevu wanaoelewa na kuhoji.Kwa watoto hadithi hii ni nzuri sana na ambayo inaonyesha kwa hakika kuwa utii ni jambo bora na kwamba Utii ni bora kuliko sadaka rejea hadithi ya mfalme sauli wa wayahudi.

Sasa kufikiri kuwa tunda la kati ni kugegeda ni kukosa utashi.Amri ya Mungu ilikuwa ni zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi baas.

Ukweli ni kwamba Adam na Hawa walikosa utii kwa Mungu,tunaita Uasi.Kwa mujibu wa hadith nyoka alikuwa mwerevu na kuwa mwerevu huwa ni chanzo cha uasi na aliamua kuasi na yeye ndio baba wa uasi na baba dhambi.Kwa hiyo basi dhambi ya uasi ndio dhambi ya asili ambayo ilianza kutendwa na shetani ibilisi

Tukirudi katika maisha yetu ya sasa tuangalia chanzo cha matatizo mengi ya kijamii na watu kukosa utii/Kutokuheshimu natural order/Kutokuheshimu hisia zetu na hisia za wengine/kutokuheshimu mamlaka/kotukuheshimu uhai/Kutokuheshimu wazazi/Kutokuheshimu wakubwa/Kukosa utii kumekuwa chanzo cha mahangaiko ya wanadamu na yumkini
Ulimwengu haukuumbwa katika namna ambayo ilisimuliwa na ushahidi wa kisayansi unaonyesha kuwa ulimwengu bado unaendelea kuumbwa na kwamba labda bado tuko siku ya kwanza tu ya uumbaji.
 
Umenifurahisha! Na ulitaka kupatia kidogo.
Japo Bible imeandikwa kuwa walikula tunda la kati lakini haikumaanisha hivyo! Ukweli ni huu naombeni muelewe:-
1.Mungu aliwaumba Adam na Hawa wakiwa na Umri gani?
Bible haiko wazi na wengi hawjiulizi hilo, hivyo kuwafanya washindwe kuelewa juu ya hii concept. Mungu aliwaumba Hawa watu wakiwa ni watoto. Ufahamu wao pia haukuwa Mkubwa.
2. Nyoka ni hisia. mawazo na fikra za alizoanza kuzipata Hawa baada ya kukua na kufikia umri wa kati (balehe). Hisia hizo zilimfanya Hawa ajiulize maxwali mengi na kumshawishi Adamu kufanya michezo na majaribio ya viungo vyao (kula tunda la kati). Hili liliwafanya wajitambue zaidi na kuanza kujua maumbile na majukumu yao. Pale Bible inaposema kuwa Mungu alikuja na kuanza kuwalaani haimaanishi vile wengi wanavyo tafsiri. Inamaanisha kuwa kutokana na cognitive maturity walioipata baada ya kubalehe, walianza kutambua majukumu yao. Kwanza ni Adam kuwa mume wa Hawa na kumtawala na kutafuta chakula, Pili, Hawa anatakiwa kuzaa na uzazi wake ni wa uchungu, Tatum, walitambua kuwa mawazo, hisia na fikra(nyoka) vinahitaji kufanyiwa uchambuzi na kuwa controlled ili kuishi vyama. Baada ya hatua hiyo ndipo walipoanza maisha ya utu uzima rasmi(wakajuana).
Note: Mungu aliwaumba Adam na Hawa kwa ukamilifu kama tulivyo binadamu wa leo. Hata mtoto wa leo anapokuwa mtoto huwa na ufahamu mdogo sana wa mambo(kuishi uchi na wanyama). Kwake dunia ni nzuri na hupata mahitaji yake kwa urahisi(maisha ya Eden).
Mtoto huyu anapofikia umri wa kati na kubalehe, na kuanza kuuchunguza mwili na kufanya majaribio mbalimbali (kushawishiwa na nyoka kula tunda. (ie. To attain maturity)), hubadilika na kuanza kujitambua. Hujua umuhi wa viungo vyao vya Siri na kuvaa vizuri kujisitiri, huanza kutafakari juu ya maisha na majukumu yao. Huanza kuchuja kila wanachoambiwa, hisi ama kufikiria(to develop ego) Pia uwezo wa kutambua jema na baya hudevelop. Baadae huingia kwenye mahusiano ya kiutu uzima na kuwajua wenzi wao. Majukumu ya mume ni kuhemea na kutunza familiar. Majukumu ya mke ni kumtii mume, kutunza familia na kuzaa.
HAKUNA JIPYA HAKUNA TAFSIRI ZAIDI YA HIYO. LABDA KAMA UMEAMUA KUDANGANYA.
Mkuu

1.hivi mungu alimuumba binadamu mara mbili?

Kama hakuumba mara mbili,then uwepo wa reproductive system mungu aliumba wa nini?

Here i mean uterus, oviducts ,vaginal with its cervix for female ,and sperms with its semen,epididymis for male.

Maana reproductive system support deliberate plan of sexual intercourse either for new offspring or to satiate pleasure

2. Kama mungu hakuruhusu hetero-sexual copulation,

Then wakati wa kumuumba eva,angemuumba hata dume tu...ili kuondoa upweke wa Adamu. .

lakini biblia katika genesis 1:26- 28 anawabariki kabisa akisema be fruitful? Hapa akibariki uzalianaji na copulation
 
Exactly mkuu

Isaiah 40:8 the green grasses dry up,blossom wither but the word of god dwells up forever
I love this book I adore it... It is a book beyond limits..! Human being limits ... Beyond normal understanding... Inahitaji kipawa cha kimungu kuweza kuilewa Biblia sio hizi elimu za darasani zilizojaa walimu bandia
 
Points zipi hizo mkuu??

Nimekusogezea hapa kitabu cha Mwanzo 3
1. Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema namabaya.6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwaajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishimilele;23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Katika yote mimi huwa nashangaa kusikia kuwa Mungu muweza wa yote alishindwa kumuona Adamu pindi alipojificha.Pia inaonesha kuwa Mungu aliwadanganya kuwa wakila tunda la mti ule watakufa kisha nyoka akaja kusema ukweli kuwa hawatakufa na baada ya kula kweli hawajafa bali walikuwa kama walivyoambiwa na nyoka.Ina maana Mungu alikosa mbinu ya kuwafanya wasile lile tunda?Na hadi nyoka anawashawishi Mungu hakugundua?Pia adamu alijifichaje hadi Alfa na Omega ashindwe kumuona wakati yeye huona hadi vilivyo ndani yetu?Yaani hii hadithi kwa upande wangu naona inamshushia Mungu heshima kimamlaka kwa sababu kwa humo bustanini Mungu ameonekana kama ni kitu chenye mawazo na umbo la kibinadamu.Hasa pale hadithi inaposema”Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu akitembea bustanini”.Napata tabu kujua huyu Mungu aliyeumba ulimwengu ndiye aliyezungumziwa humo au ni Mungu yupi mwenye uwezo mdogo kiasi hicho?Pia ni nani aliwaambia wapo uchi?
 
Eti Mungu hakumuona adamu alipojificha!Mungu alidanganya kuwa watakufa kisha nyoka akavujisha siri(Mungu alisema uongo?)mh!Twendeni tu mwisho tutafika.
 
Adam aliumbwa mzima kisha akapewa pumzi lakin Hawa alifanywa/aliumbwa kutoka ubavu wa adam
 
Mshana Jr
[emoji23]... [emoji95] ....[emoji379]
Siku hizi umeanza uongo enhee
 
Mm binafsi sioni km ni jambo la kuumiza zn kichwa.. "walipokula, wakafumbuliwa macho, WAKAJIONA wako uchi" tena ule ulikuwa ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Moja kwa moja tunapata kujua kuwa kwa sabb ndani ya lile tunda ndipo huo ujuzi(ujuaji wa mema na mabaya) ulipo, basi ndio mana walipokula tuu, ndipo walipojua. Ina maana MUNGU alitia huo ujuzi ndani ya lile tunda, kabla, walikuwa wakiishi km watoto tuu.. Km ivi leo tunavyoona watoto wachanga, wanaweza kula ht mavi, wasijue kuwa ni kitu kibaya, lkn wakikua, hujua kumbe hiki hakifai.. Kumbk ule ulikuwa ni mwanzo, na kila kitu huwa kina mwanzo, sawasawa na uumbaji wa MUNGU.. Kwa hy walipokula tuu lile tunda lenye sumu, ndipo walipokufa....

Niishie hapo, km sijaeleweka niulizeni, nitajibu kwa uelewa wangu
 
Acheni kufikiria Mambo ambayo yaweza hata kumkwaza Mungu kitabu kitakatifu kimeweka wazi basi.

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesemza, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
8 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
9 BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.

Sio mwaanza kuchunguza jambo lisilo kuwepo hata.
 
Katika yote mimi huwa nashangaa kusikia kuwa Mungu muweza wa yote alishindwa kumuona Adamu pindi alipojificha.Pia inaonesha kuwa Mungu aliwadanganya kuwa wakila tunda la mti ule watakufa kisha nyoka akaja kusema ukweli kuwa hawatakufa na baada ya kula kweli hawajafa bali walikuwa kama walivyoambiwa na nyoka.Ina maana Mungu alikosa mbinu ya kuwafanya wasile lile tunda?Na hadi nyoka anawashawishi Mungu hakugundua?Pia adamu alijifichaje hadi Alfa na Omega ashindwe kumuona wakati yeye huona hadi vilivyo ndani yetu?Yaani hii hadithi kwa upande wangu naona inamshushia Mungu heshima kimamlaka kwa sababu kwa humo bustanini Mungu ameonekana kama ni kitu chenye mawazo na umbo la kibinadamu.Hasa pale hadithi inaposema”Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu akitembea bustanini”.Napata tabu kujua huyu Mungu aliyeumba ulimwengu ndiye aliyezungumziwa humo au ni Mungu yupi mwenye uwezo mdogo kiasi hicho?Pia ni nani aliwaambia wapo uchi?
Adam na Hawa walikuwa waishi milele Ila wakala tunda mwisho wa siku SI waliishi wakafa Mungu hadanganyi, na Tena SI kwamba alishindwa kuwaona bali Mungu aliishi nao kama vile kawaida kabisa kama maisha ya kibinadamu
 
Acheni kufikiria Mambo ambayo yaweza hata kumkwaza Mungu kitabu kitakatifu kimeweka wazi basi.

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesemza, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
8 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
9 BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.

Sio mwaanza kuchunguza jambo lisilo kuwepo hata.
Mstari wa 11... Ni nani aliwaambia kuwa mu uchi?? Hili swali mpaka leo halina majibu... Adamu alikosa jibu na Matokeo yake akamsakizia mwananke kwa kusema.. Si huyu mwanamke uliyenipa! Lakini kwa hakika maandiko yako wazi kuwa hakuna mahala popote Eva anamwambia Adam sasa tu uchi! Kama Adam alishindwa kujibu swali kwanini ni nani aliyemwambia kwamba wako uchi unadhani ni ngurumbili gani katika dunia ya leo anaweza kujibu hilo swali?
 
Back
Top Bottom