Heshima mbele Wakuu.... Leo nimeona hii kwenye Alasiri nikapata mshituko kwa kweli.... Sikutegemea kuwa rushwa imetutafuna mpaka hatuna hata pa kujisitiri, hebu angalia hawa jamaa wa Manispaa ya Kinondoni wamekodisha ule ufukwe mzimaa kwa mtu/kampuni moja kwa jumla ya miaka 37??!?! Hawa wakuu kweli sasa wamekuwa zaidi ya vilafi manake ukumbuke hawahawa (wilaya hii hii) ndio walitoa kibali cha kujenga yale maghorofa marefu kule Masaki (Toure Drive) kisha yakabomolewa na leo tunaambiwa kesi ipo mahakamani kilichobaki pale ni magofu!! Hivi Tanzania inaenda wapi wajamani!?!!?!
Kapten Chiligati asema kuikodisha `Coco Beach` kwa miaka 37 ni kosa
2008-05-24 15:34:10
Na Sharon Sauwa, Mikocheni
Wakati Manispaa ya Kinondoni ikiwa
inadaiwa kukodisha ufukwe wa Coco almaarufu kama `Coco Beach` kwa mfanyabiashara mmoja Jijini atakayeutumia kwa miaka 37, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kapteni (Mstaafu) John Chiligati, amesema kisheria, ni kosa kumkodishoa mtu eneo kwa muda unaozidi miaka mitano.
Akihojiwa na Radio One jana asubuhi, Kapteni Chiligati amesema sheria inaruhusu kukodishwa kwa ufukwe kwa muda usiozidi
miaka mitano.
Hata hivyo, akasema sheria hiyo inapiga marufuku uuzwaji wa ufukwe kwenda mtu yeyote.
``Haya ni maeneo ambayo yapo
chini ya Serikali za mitaa... lakini sheria inaruhusu kukodishwa kwa miaka isiyozidi mitano kwa ajili ya kuendeleza na kutunza maeneo hayo,`` akasema Kapten Chiligati.
Akasema maeneo hayo ni mali ya umma ambayo yametengwa kwa ajili ya starehe na burudani na kwamba ni mita 60 kutoka majini kwenda nchi kavu.
Kuhusu sakata hilo, Kapteni Chiligati akasema bado taarifa kuhusiana na jambo hilo bado hazijamfikia.
Eneo linalodaiwa kukodishwa lina jumla ya hekta 21.6 na linaanzia maeneo ya Toure Drive na kuishia Bwalo la Maofisa wa Polisi.
Hali hiyo imefanya baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Kinondoni kudai kuwa wamerubuniwa na kutia saini baadhi ya mikataba ambayo imeandaliwa na kupitishwa na watendaji waandamizi na matokeo yake ni kuitia hasara manispaa yao na pia kubariki ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi .
Kutokana na suala hilo, watendaji wa manispaa hiyo wamegawanyika huku baadhi wakiwa matatani kutokana na kutetea uuzwaji wake na huku wengine wakiupinga.
Hata hivyo, uongozi wa manispaa hiyo umekaririwa ukidai kuwa ufukwe wa Coco umekodishwa na si kuuzwa.
SOURCE: Alasiri
24/05/2008 (www.ippmedia.com)
My take:
1. Waziri anasema taarifa hazijamfikia, jamani sasa ameshaona ata act au atangoja taarifa zimfikie?
2. Huyo aliyefanya kosa amechukuliwa hatua gani?
3. Madiwani wanasema wamerubuniwa kutia saini mikataba bomu, ha ha haaaaaa!! Shame on them, ina maana wao wanakutana kutia saini mikataba bila kuisoma?? Hawana common sense ya kujua jema na baya? Au kurubuniwa ni "In Kind?"
4. Watendaji eti wamegawanyika, then what?? Wanaweza wakabaki na mgawanyiko wao lakini sisi tunataka kujua ukweli na uamuzi kuwa reversed!
5. Eti eneo limekodishwa halijauzwa, hawa wakuu wanajua hata ukinunua shamba Kimanzinchana Serikali ikikupa Title deep ni ya muda gani?? 33 years, wao wamempa Mkuu 37 years.... Hawa watendaji wanatakiwa wapigwe bakora kabisa.... kutetea such nonsense ni upuuzi mkubwa sana!!!