WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku uamuzi wa Manispaa ya Kinondoni kuuza kwa mfanyabiashara mmoja maarufu eneo la ufukwe la Coco Beach.
Pinda alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na madiwani wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya habari kuhusu uamuzi huo unaoonekana kupigwa danadana na kufanywa kwa siri kuvuja na kuandikwa katika vyombo vya habari.
Alisema Jiji la Dar es Salaam limekumbwa na tatizo la migogoro ya viwanja ambalo kimsingi limesababisha kuibuka kwa manunguniko ya watu kila mara.
Tatizo la migogoro ya viwanja Dar es Salaam ni kubwa, siku za karibuni tumesikia uuzwaji wa Coco Beach uliofanywa na Manispaa ya Kinondoni. Tumeanza kusikia minongono katika hiyo beach. Huyo anayejenga mwambieni ajenge, kwa kuwa kila atakapojenga watu watabomoa.
Eti wanasema wanaipendezesha. Nauliza wanaipendezesha kwa ajili ya nani? Mnataka kupambana na jamii
kwa kuwa imeamka na haiko tayari kukubali hilo, nyie watu wa Kinondoni hamna la kufanya? alihoji Waziri Pinda na kuongeza: Hiyo ni Beach, iacheni hivyo hivyo, tafuteni mabeach mengine kama vile Rufiji mkajenge. Alisema kutokana na umuhimu wa Dar es Salaam na dhamira ya serikali ya kutaka ionekane kuwa ni kioo cha nchi, katika mwaka ujao wa fedha serikali imetenga sh bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha miundombinu.
Kwa nafasi ya Jiji la Dar es Salaam, lazima tufike mahali tuishawishi serikali, ili kuwekwe mfumo wa kuiangalia kwa jicho la tofauti na miaka mingine.
Kila mwaka zitolewe sh bilioni 10 kwa ajili ya mkoa huu, sh bilioni tatu kwa ajili ya kukarabati mifereji na sh bilioni sita kwa ajili ya kufungua barabara kama ile ya Mabibo, Mburahati hadi Kigogo, ili kupunguza msongamano, alisema Pinda.
Aliongeza kuwa, Dar es Salaam ndiyo kioo cha taifa, kwa kuwa ndiyo makao makuu ambapo kuna bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa na pia ndiyo chanzo cha treni ya kwenda maeneo mbalimbali nchini.
Katika maelezo yake, Waziri Mkuu alitoa agizo la kuhakikisha wamachinga wote waliopo katika maeneo yasiyoruhusiwa wanaondolewa na kuwekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa kazi hiyo.
Chonde chonde Mkuu wa Mkoa, lazima tujitahidi tuwe na nidhamu. Hawa wamachinga wanatakiwa wawe katika maeneo waliyotengewa, kwani nimeona hali ya wamachinga imeaanza kurudi. Tusiwaruhusu wakarudi barabarani, alisema Pinda.
Pia alisisitiza suala la usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam, na kumtaka kila mwananchi katika mtaa wake kujitahidi kuboresha usafi, kwani uchafu unachangia kuzorotesha manispaa kuweza kutoa huduma bora.
Alizitaka manispaa kuvuta kamba ili kuhakikisha suala la kukusanya uchafu linafanywa kwa umakini.
Pia aliagiza manispaa kuzingatia utoaji wa leseni za muziki na vileo kwa watu ambao hawajapewa, na kuwaonya wenye leseni wazingatie taratibu na sheria za leseni walizopatiwa.
juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 10 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hapo Pindisha kula tano, ila tu isiwe ni mbio za sakafuni na jeuri/nguvu ya soda. Maana hamkawii kupindisha
na kukuz , singapore, - 29.05.08 @ 10:01 | #13918
Kwanza kabisa nakupa pongezi Mh. Pinda kwa kuzuia uuzwaji wa Coco Beach. jambo lingine ni kuhusu Jiji la DSM, tatizo kubwa Viongozi wenye dhamana ya kusimamia Jiji hili ni kutokuwa na Vision ya namna gani Jiji hili linapaswa kuwa, na ndio utaona wakati zinafanyika jitihada za kuliboresha bado kuna mambo ya hovyo yanazuka siku hata siku kwa mfano bado ujenzi holela unaendelea kufanyika sio tu pembezoni mwa Jiji hata katikati ya jiji pia.Na huku uswahilini Sheria hazizingatiwi kabisa kwa mfano wenye hizo zinazoitwa Bar (kwa hakika ni Groceries) wanapiga muziki kwa sauti kubwa kabisa kiasi kwamba kunakuwa hakuna kabisa utulivu na wenye dhamana hawachukui hatua yoyote.
na A.S. Mbweni, DSM, - 29.05.08 @ 10:27 | #14021
Hapo Mh.Pinda afadhali umesema ukweli hakuna kuuza na tena akijenga bomoa kama masaki na hakuna fidia. Ili waelewe serikali ina mkono mrefu.
Hapa naendelea kuunga mkono kauli ya Mh. Mkono kwamba haya mambo ya kuuza viwanja mara mbili au maeneo ya wazi wanasambabishwa na elimu mbovu inayoeleta mtazamo finyu juu ya mipango miji. Wataalum wetu je huo sio wakati wakupanua Bunju ,Boko, Mbagala na kigamboni hapo city pabaki hivyo ukiweka usafiri mzuri tena wa usalama wa kufika Bunju na Boko kupitia kwenye bahari na huku kigamboni ukaweka Daraja unafikiri kuna mtu ataagalia hako kacity kwa mtazamo finyu. Hebu tafuteni miradi mkubwa ya kupanua jiji tuacha kuinga wote mjini kwa wakati mmoja na kutoka kwa wakati moja. Kazi kwenu watu wa mipango miji kama kweli mlisoma au kuchugulia mithani pale Ardhi Institute.
na linambasha, Hongkong, - 29.05.08 @ 10:38 | #14026
HIVI NA SWALA LA ROSE GARDEN LIMEISHIA WAPI WAKATI ILE BAR INAJULIKANA KABISA HATA NA MTOTO MDOGO KABISA IKO KATIKA ENEO LA BARABARA????MADIWANI MANFANYA NINI NA MKUU WA MKOA MPO AU MLEWESHWA NA BIA ZA ROSE GARDEN MNASHINDWA KUFATA SHERIA YA MIPANGO MJI??????????????****** ZENU
na munir, dar, - 29.05.08 @ 08:07 | #14036
Nimeshaona kuwa waziri mkuu,amewaona hawa watu wa halmashauri ,niwahuni na ma fi sa di wa haliya juu.Ameamua kiukwe.Na asikomee hapo awafuatilie kuona undai, nilazima watu wa halmashauri wamepewa hongo.Tumechoshwa kusoma taaria za mambo ya halmashauri ,mara kubomoa mara hamishahamisha.Watu wanaishi kama wako kwa makaburu.Maana hujui halmashauri kesho itaropoka nini.Heko Mh WAZIRI MKUU KWA KUWASAIDIA WNYONGE.
na mtzmwenyeuchungu, tz, - 29.05.08 @ 08:27 | #14044
Andikeni majina yenu halisi ili hoja zenu zifanyiwe kazi! tumielewana akina mtzmwenyeuchungu na wenzako!
na mhariri, tanzania, - 29.05.08 @ 09:08 | #14058
kinachotakiwa humu ni hoja na siyo kujua ni nani kaandika, utawajua watu wote wewe? au unataka kuwafanya nini?
na mwenzake na mtzmwenye uchungu, dar, - 29.05.08 @ 09:34 | #14065
Mhe MIZENGO KAYANZA PINDA kama nilivyosema ni chaguo letu wote mungu
amlinde na na mafisadi na atashinda tu
na mimi nipo nyuma yake
na Daniel mugassa, DAR/Tanzania, - 29.05.08 @ 09:42 | #14069
oooh sawa waandishi wa habari muwe wabunifu katika kutatua matatizo ya miji yetu. asilmia kubwa ya matatizo ya Dar es salaam yanatokana na mfumo mbovu wa utwala wa ardhi.
kinondoni wanaongoza kwa rushwa hasa kitengo cha ardhi. kwa nini waandishi hamjafanya uchambuzi wa haya na kuyaweka bayana. Hebu sasa mufanye hivyo na hapo mtakuwa mmesaidia maeneleo ya jiji
letu.
na emanan, germany, - 29.05.08 @ 09:47 | #14071
Dar es Salaam ni Tanzania hii hii. Maamuzi mazuri na ya haraka kama haya yafanyike sehemu zote kuliko na migogoro kama huu wa Dar.
Tunategemea leo au kesho waziri wetu utatoa tena maamuzi kama haya kuhusiana na uwanja wa Nyamagana kule Mwanza. Wananchi hawataki uuzwe na wana sababu nzuri tu wameshazisema,viongozi hawataki kusikia. Wanasubiri mpaka damu imwagike ndiyo waje kukubaliana nao!
Viongozi wanawajibika kwa wananchi. Hivi hawa viongozi wa Mwanza wanawajibika kwa nani? Wakome kutuburuza wananchi maana sie ndiyo tumewafikisha hapo walipo.Watusikilize basi na watambue nasi tuna uelewa wa kutosha pengine hata kuwazidi wao.
Viongozi tujifunze kuwasikiliza wananchi hata walio chini!
na Pius - 29.05.08 @ 10:18 | #14080
[