Fukwe (Beach) za Tanzania na hatma yake

Wacheni wacheni wacheni ,hivi hapo kama angekodishwa mzungu mngepiga makelele,mimi nimefurahi sana kuona aliekodi ni mzalendo ingawa sijafahamu nia na madhumuni haswa ya maradi aliokusudia ,inawezekana mtu akajenga na kuinvest nyumba na kukodisha au akaweka sehemu ya Park na kuweza kujipatia fedha ,hivi ndivyo wananchi wanavyotakiwa wawekeze , mtu anaweza sehemu hiyo akaizingira na kuweka mambo ya kufurahisha jamii at the week end ndugu na jamaa wanajimwaga huko,just akaweka kiingilio labda shilingi mia tano au mia tatu kiasi hata mlala hoi anaweza kwenda kujiburudisha ,hayo ndio mambu yalioko ulaya.
na zaidi kuwa jamaa hakununua isipokuwa amekodi sasa tatizo lipo wapi Karume na Salmini wamekodisha visiwa kwa muda wa miaka 99 kuna nchi unakodi nyumba kwa miaka mia na sio unakodi unanunu nyumba kwa muda wa miaka mia ,yaani mjenzi mmiliki na hata aliekodi watakuwa hawapo tena na hiyo ndio biashala.
hapo kuna watu wamekosa mlo tu hakuna cha Chiligati wala wala Chiligate wanataka wamegewe tu ,na jamaa akimuwahi huyo wa waziri kwa donge nono basi mtaona ila hamtasikia kitu.

Watu wenye mawazo kama yako ndiyo watakaotufikisha pabaya. Wewe tatizo lako ni asikodishwe mzungu lakini hao wawahili wenzetu wanao tufanya vibaya kuliko hata huyo mgeni huoni tatizo? Ufukwe wa Oistabei ni aibu tupu. Pale palikuwa ni sehemu ambayo kila mtu anaweza kwenda kuogelea au kupunga upepo. Wakati wa enzi yake palijaa mikoko na maji na bech ilikuwa safi. Leo pamekuwa Disco (asante Coco beach), sehemu ya kutambiana magari na pikipiki, kuchomoma mishkaki ili mradi kila kitu isipokuwa kuogelea kwa usalama! Mikoko haipo tena na minazi yote vipara. Hata katika hali hii duni palikuwa ni sehemu ambapo wasioweza kwenda bongoyo waliweza kwenda kupumzika bila tatizo. Leo wahuni wanataka ku'privatise' na kuiharibu kabisa nawe unashangilia? Huu upuuzi wa kuwa ati amekodishwa na wala hakuuziwa kwani nani Tanzania anauziwa ardhi? Ardhi yote si leasehold na ina muda wake wa kumiliki? Yaani tumefika mahali kuwa hata Mungu hatumuogopi kwa ulafi wetu? Mungu atunusuru na waovu wote, wageni na waswahili wenzetu. Hawana tofauti hawa.
 
Hawa madiwani waliotia saini kukodisha waulizwe vitu viwili:-

(1) Je, ilifanyika "Social Impact Assessment" kabla ya ukodishaji huo?
(2) Je, mwekezaji amefanya "Environmental Impact Assessment?

Jibu litakuwa...

...

...

Hawajui vitu hivyo ni nini.
 
Kapten Chiligati asema kuikodisha `Coco Beach` kwa miaka 37 ni kosa

2008-05-24 15:34:10
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Wakati Manispaa ya Kinondoni ikiwa inadaiwa kukodisha ufukwe wa Coco almaarufu kama `Coco Beach` kwa mfanyabiashara mmoja Jijini atakayeutumia kwa miaka 37, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kapteni (Mstaafu) John Chiligati, amesema kisheria, ni kosa na laana kubwa kumkodishoa mtu eneo kwa muda unaozidi miaka mitano.

Akihojiwa na Radio One jana asubuhi, Kapteni Chiligati amesema sheria inaruhusu kukodishwa kwa ufukwe kwa muda usiozidi miaka mitano.

Hata hivyo, akasema sheria hiyo inapiga marufuku uuzwaji wa ufukwe kwenda mtu yeyote.

``Haya ni maeneo ambayo yapo chini ya Serikali za mitaa... lakini sheria inaruhusu kukodishwa kwa miaka isiyozidi mitano kwa ajili ya kuendeleza na kutunza maeneo hayo,`` akasema Kapten Chiligati.

Akasema maeneo hayo ni mali ya umma ambayo yametengwa kwa ajili ya starehe na burudani na kwamba ni mita 60 kutoka majini kwenda nchi kavu.

Kuhusu sakata hilo, Kapteni Chiligati akasema bado taarifa kuhusiana na jambo hilo bado hazijamfikia.

Eneo linalodaiwa kukodishwa lina jumla ya hekta 21.6 na linaanzia maeneo ya Toure Drive na kuishia Bwalo la Maofisa wa Polisi.

Hali hiyo imefanya baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Kinondoni kudai kuwa wamerubuniwa na kutia saini baadhi ya mikataba ambayo imeandaliwa na kupitishwa na watendaji waandamizi na matokeo yake ni kuitia hasara manispaa yao na pia kubariki ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi .

Kutokana na suala hilo, watendaji wa manispaa hiyo wamegawanyika huku baadhi wakiwa matatani kutokana na kutetea uuzwaji wake na huku wengine wakiupinga.

Hata hivyo, uongozi wa manispaa hiyo umekaririwa ukidai kuwa ufukwe wa Coco umekodishwa na si kuuzwa

Yeye kama waziri anaweza kabisa kuvunja mikataba kama hii kwa kutumia sheria ambazo amepewa kama waziri husika . Je, kwa nini hafanyi hivyo badala ya kulia nyau?
 
Yeye kama waziri anaweza kabisa kuvunja mikataba kama hii kwa kutumia sheria ambazo amepewa kama waziri husika . Je, kwa nini hafanyi hivyo badala ya kulia nyau?

Mchanga wa macho huu...waziri ameenda kwenye media kusema mkataba ni laana ili iweje. Ana ajenda yake ya kujitafia umaarufu...lakini kwanza anawatayarisha wadanganyika...halafu mkataba ukivunjwa muhusika ataenda mahakamani, serikali itatumia milioni kibao kujitetea mahakamani...serikali itashindwa itaamuriwa kumlipa muhusika fidia, watakata rufaa na ulaji utaendelea...bongo mambo tambarare.
 
...hivi Aliyekodishiwa Ni Yule Bwana Mdogo Alphonce Mutta...maana Ndio Amekuwa Akipaendesha Muda Mrefu...

..lakini Simply Kwa Sea Front Kama Ile Kuwa Mordernised Hakuna Ubaya...si Mnatembea Nchi Za Wenzetu Mnaona ..mradi Asijenge Permanent Structures...

..tatizo La Hiyo Manispaa Ya Kinondoni Ni Ufisadi Wa Salum Londa ....na Yule Mvuta Bangi Bujugo...ambaye Pia Anamiliki Zile Shule Anazoziita International Schools Amabazo Hazina Hata Bustani Au Kiwanja Cha Mazoezi Ya Aina Yoyote Kwa Vijana.....sijui Inakuwaje Zinasajiliwa Chini Ya Kiwango Namna Ile,...
 
Bado Ikulu tu! Nchi yote tayari... hamjui kwani? Hayo majengo ya BoT mpaka walipe huo mkopo wa kuyajenga unadhani kitabakia kitu? Hahaha! Ka-nchi haka kazuri kweli! Kila kitu kiko sokoni, pesa yako tu bwana na bibi!
 
Ni nani aliyekodishiwa eneo? Serikali ilikuwa ikipata mapato gani? ni mipango gani inafanywa kwa huu mkataba na ardhi na eneo litatumika kwa kazi gani na manufaa ya nani?
 
Hawa madiwani waliotia saini kukodisha waulizwe vitu viwili:-

(1) Je, ilifanyika "Social Impact Assessment" kabla ya ukodishaji huo?
(2) Je, mwekezaji amefanya "Environmental Impact Assessment?

Jibu litakuwa...

...

...

Hawajui vitu hivyo ni nini.

Kwa mujibu wa sheria zetu diwani hana mahali pa kusaini (Waraka wa Madili ya viongozi na madiwani wa mwaka 2005) kuna kipengere kinasema "NI MARUFUKU KWA DIWANI KUFANYA KAZI ZA KITALAAM". Madiwani wanachokifanya ni kuamua katika vikao vyao halali (Vikao vya Kamati kisa Full Council). Mkurugenzi na watendaji wengine yaani Mwanasheria, Afisa Mipango Miji nk wanalazimika kutekeleza maamuzi ya Madiwani.

Ila ninahisi kwamba kunauzembe wa Kitengo cha Sheria na Idara ya Mipango Miji, kwani walipaswa kuwaeleza Madiwani kwamba sheria hairuhusu kukodisha fukwe kwa zaidi ya miaka 5. Endapo madiwani hawakukubaliana nao walipaswa kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya au Wizarani moja kwa moja ili DC au Wizara ya Ardhi watoe taarifa TAMISEMI. Kwa mujibu wa Sheria ni Waziri wa TAMISEMI tu ndiyo mwenye mamlaka ya kufuta maamuzi ya Halmashauri. Waziri wa TAMISEMI anaweza hata kunyang'anya baadhi ya majukumu ya Halmashauri akampatia mtu au organ fulani ya Serikali.
 
Sasa yeye huyo Chiligati akiwa kama Waziri wa ardhi badala ya kuendelea kulalama atumie wadhifa wake kutengua ukodishaji huo haraka sana.

Waziri wa ardhi hana mamlaka dhidi ya maamuzi ya Halmashauri, Mamlaka hayo anayo Waziri wa TAMISEMI tu. Hii ni kwa mujibu wa Sheria na 7 na 8 za mwaka 1982, Local Government Authority Act.
 
Sheria hairuhusu kufanya lolote within 60 meters from the water inwards, anything behind that is fair game...maintenance of that area was long overdue, labda ataweka park nzuri or something sustainable...Its a lease, tatizo liko wapi kwa Mfanyabiashara ku-lease ardhi? kosa Waziri anasema ni time ya miaka 37 na inatakiwa iwe miaka mitano...SIYO UFISADI KUKODI ARDHI FOR DEVELOPMENT!!!!coco beach is fair game.
 
Kwa maoni yangu binafsi, ni kwamba Cocobeach kwa maana ya ufukwe wote si wa kumkodisha mtu, halafu huyo mtu atoze watu pesa za kiingilio kwenda kupunga upepo au kuogelea, unaweza kumkodisha mtu kaeneo kadogo kwa ajili ya kujenga hoteli, au restaurant, au huduma zozote zile ziwazo. lakini ufukweni ni mahala ambapo wananchi wanakwenda kufurahia zawadi hii ya bahari aliyotupa Mwenyezi Mungu.haipaswi kuwatoza watu pesa kwenda ufukweni
 
Jamani hii sasa ni hatari, yaani hadi sehemu za kupumzika walala hoi pia mntaka kuzipiga bay? Hii kweli ni balaa sasa, yaani nchi inauza kila kitu migodi imekodishwa miaka kwa miaka, bandari wamepewa sijui nani kwa miaka kibao, bonde la mto rufiji wamepewa sijui watu wa bioenergy, uwanja wa ndege tumegawa, ngorongoro sijui kapewa nani. Mungu atubariki jamani, hii inatisha.

Ni ngumu sana kutokutabiri kwamba kuna siku tutaanza kuchapana vyuma vya moto.
 
Sheria hairuhusu kufanya lolote within 60 meters from the water inwards, anything behind that is fair game...maintenance of that area was long overdue, labda ataweka park nzuri or something sustainable...Its a lease, tatizo liko wapi kwa Mfanyabiashara ku-lease ardhi? kosa Waziri anasema ni time ya miaka 37 na inatakiwa iwe miaka mitano...SIYO UFISADI KUKODI ARDHI FOR DEVELOPMENT!!!!coco beach is fair game.

So far hakuna mtu anaefahamu huyo muwekezaji anataka kufanya nini. Jee kama anataka kufungua park kisha akakodisha wananchi kukaa, jee kama anataka kutengeneza hotel, au mgahawa.

Hatujui nini kitafanyika baada ya yeye kuchukua deal, kuepuka hayo ni bora kuzima deal nzima.
 
Kwa maoni yangu binafsi, ni kwamba Cocobeach kwa maana ya ufukwe wote si wa kumkodisha mtu, halafu huyo mtu atoze watu pesa za kiingilio kwenda kupunga upepo au kuogelea, unaweza kumkodisha mtu kaeneo kadogo kwa ajili ya kujenga hoteli, au restaurant, au huduma zozote zile ziwazo. lakini ufukweni ni mahala ambapo wananchi wanakwenda kufurahia zawadi hii ya bahari aliyotupa Mwenyezi Mungu.haipaswi kuwatoza watu pesa kwenda ufukweni

Ruksa kwa mtu yeyote kutembea 60 meters of land starting from the water...so huwezi kuzuiwa kuenda ufukweni, rukwa kuogelea na kutembelea...hiyo ni sheria...tatizo tu itabidi utafute parking sehemu nyingine...but the Law is Clear, 60 Meters of coastline is Public land!. Sidhani kama amepewa the illegal 60 meters. ndo maana nasema sehemu ya coco beach nyuma ya meter 60 kutoka kwenye maji ni fair game...ndo maana hata hoteli kubwa on the coast dar, unaweza kutembea kuanzia whitesands mpaka bahari beach bila matatizo ya kisheria.
 
Sheria hairuhusu kufanya lolote within 60 meters from the water inwards, anything behind that is fair game...maintenance of that area was long overdue, labda ataweka park nzuri or something sustainable...Its a lease, tatizo liko wapi kwa Mfanyabiashara ku-lease ardhi? kosa Waziri anasema ni time ya miaka 37 na inatakiwa iwe miaka mitano...SIYO UFISADI KUKODI ARDHI FOR DEVELOPMENT!!!!coco beach is fair game.

vitu kama kuweka park nzuri ndivyo vitu ninavyozungumzia kama huduma.kumkodisha mtu huduma katika ufukwe haina tatizo, tatizo ni kumkodisha huyo mtu Ufukwe, halafu awatoze watu kiingilio. kama suala ni huduma kama hiyo park basi watu wenye magari watalzimika kulipia huduma hiyo. lakini vipi kuhusu watu wasio na magari lakini wanataka kupunga upepo, au kuogelea?, watozwe pesa?
Kuwatoza pesa wananchi ili kufaidi Ufukwe kama ule wa cocobeach, ni jambo lisilo kubalika hata kidogo.

Katika mtindo wa kuwatoza wananchi kiingilio ufukweni ni dhahiri mtoza pesa atakuwa anachukua pesa za bure,
 
Sheria hairuhusu kufanya lolote within 60 meters from the water inwards, anything behind that is fair game...maintenance of that area was long overdue, labda ataweka park nzuri or something sustainable...Its a lease, tatizo liko wapi kwa Mfanyabiashara ku-lease ardhi? kosa Waziri anasema ni time ya miaka 37 na inatakiwa iwe miaka mitano...SIYO UFISADI KUKODI ARDHI FOR DEVELOPMENT!!!!coco beach is fair game.

Sheria awali ilikuwa ni meta 200 na sio 60. Kwa uroho wetu ili kuruhusu white sands ijengwe ikapuguzwa hadi 60. Matokeo tumeyaona ya beach erosion kunzia Ocean road hadi Tegeta! Pili, kisheria, beach ni eneo la public kwa hiyo hauwezi ku'privatise' ingawa kuna wajanja wanafanya hivyo. Tatu, kwa nini huyu so-called mwekezaji asiende kwenye hizo virgin beaches zilizozagaa badala ya kukazania beach ambayo imeshachoka na inahitaji kupumzika?
 
Ni uroho huo huo uliosababisha wakodishe huo ufukwe.
Hii ni laana,hata maharusi nao pale Aghakan siku hizi marufuku kupiga picha,baada ya siku chache tutasikia hapo napo tutasikia pamepata mwekezaji
 
Wacheni wacheni wacheni ,hivi hapo kama angekodishwa mzungu mngepiga makelele,mimi nimefurahi sana kuona aliekodi ni mzalendo ingawa sijafahamu nia na madhumuni haswa ya maradi aliokusudia ,inawezekana mtu akajenga na kuinvest nyumba na kukodisha au akaweka sehemu ya Park na kuweza kujipatia fedha ,hivi ndivyo wananchi wanavyotakiwa wawekeze , mtu anaweza sehemu hiyo akaizingira na kuweka mambo ya kufurahisha jamii at the week end ndugu na jamaa wanajimwaga huko,just akaweka kiingilio labda shilingi mia tano au mia tatu kiasi hata mlala hoi anaweza kwenda kujiburudisha ,hayo ndio mambu yalioko ulaya.
na zaidi kuwa jamaa hakununua isipokuwa amekodi sasa tatizo lipo wapi Karume na Salmini wamekodisha visiwa kwa muda wa miaka 99 kuna nchi unakodi nyumba kwa miaka mia na sio unakodi unanunu nyumba kwa muda wa miaka mia ,yaani mjenzi mmiliki na hata aliekodi watakuwa hawapo tena na hiyo ndio biashala.
hapo kuna watu wamekosa mlo tu hakuna cha Chiligati wala wala Chiligate wanataka wamegewe tu ,na jamaa akimuwahi huyo wa waziri kwa donge nono basi mtaona ila hamtasikia kitu.
__

Mwiba kama alivyosema mmoja hapa kwamba mawazo yako ni hatari kwamba mtu mweusi ni ruhusa kuhujumu nchi, haikubaliki ndio mawazo ya kina Mkapa sasa hivi kwamba wao ni WATANZANIA wana haki ya kuiba, maana mbona eti wahindi wanaiba!!! SHAME!! Lakini kwa taarifa yako aliyekodishwa hapo si Mswahili bali Mswahili, Alfonce anayeendesha pale beach miaka yote kwa mkataba na MAnispaa anaondolewa kwa RUSHWA YA AIBU kwa sababu ua Jamaa mmoja MHINDI tena tapeli wa kutupa
 
Pinda azuia ufukwe kuuzwa Dar

na Lucy Ngowi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku uamuzi wa Manispaa ya Kinondoni kuuza kwa mfanyabiashara mmoja maarufu eneo la ufukwe la Coco Beach.

Pinda alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na madiwani wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya habari kuhusu uamuzi huo unaoonekana kupigwa danadana na kufanywa kwa siri kuvuja na kuandikwa katika vyombo vya habari.

Alisema Jiji la Dar es Salaam limekumbwa na tatizo la migogoro ya viwanja ambalo kimsingi limesababisha kuibuka kwa manung’uniko ya watu kila mara.

“Tatizo la migogoro ya viwanja Dar es Salaam ni kubwa, siku za karibuni tumesikia uuzwaji wa Coco Beach uliofanywa na Manispaa ya Kinondoni. Tumeanza kusikia minong’ono katika hiyo beach. Huyo anayejenga mwambieni ajenge, kwa kuwa kila atakapojenga watu watabomoa.

“Eti wanasema wanaipendezesha. Nauliza wanaipendezesha kwa ajili ya nani? Mnataka kupambana na jamii… kwa kuwa imeamka na haiko tayari kukubali hilo, nyie watu wa Kinondoni hamna la kufanya?” alihoji Waziri Pinda na kuongeza: “Hiyo ni Beach, iacheni hivyo hivyo, tafuteni ‘mabeach’ mengine kama vile Rufiji mkajenge.” Alisema kutokana na umuhimu wa Dar es Salaam na dhamira ya serikali ya kutaka ionekane kuwa ni kioo cha nchi, katika mwaka ujao wa fedha serikali imetenga sh bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha miundombinu.

“Kwa nafasi ya Jiji la Dar es Salaam, lazima tufike mahali tuishawishi serikali, ili kuwekwe mfumo wa kuiangalia kwa jicho la tofauti na miaka mingine.

“Kila mwaka zitolewe sh bilioni 10 kwa ajili ya mkoa huu, sh bilioni tatu kwa ajili ya kukarabati mifereji na sh bilioni sita kwa ajili ya kufungua barabara kama ile ya Mabibo, Mburahati hadi Kigogo, ili kupunguza msongamano,” alisema Pinda.

Aliongeza kuwa, Dar es Salaam ndiyo kioo cha taifa, kwa kuwa ndiyo makao makuu ambapo kuna bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa na pia ndiyo chanzo cha treni ya kwenda maeneo mbalimbali nchini.

Katika maelezo yake, Waziri Mkuu alitoa agizo la kuhakikisha wamachinga wote waliopo katika maeneo yasiyoruhusiwa wanaondolewa na kuwekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa kazi hiyo.

“Chonde chonde Mkuu wa Mkoa, lazima tujitahidi tuwe na nidhamu. Hawa wamachinga wanatakiwa wawe katika maeneo waliyotengewa, kwani nimeona hali ya wamachinga imeaanza kurudi. Tusiwaruhusu wakarudi barabarani,” alisema Pinda.

Pia alisisitiza suala la usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam, na kumtaka kila mwananchi katika mtaa wake kujitahidi kuboresha usafi, kwani uchafu unachangia kuzorotesha manispaa kuweza kutoa huduma bora.

Alizitaka manispaa kuvuta kamba ili kuhakikisha suala la kukusanya uchafu linafanywa kwa umakini.

Pia aliagiza manispaa kuzingatia utoaji wa leseni za muziki na vileo kwa watu ambao hawajapewa, na kuwaonya wenye leseni wazingatie taratibu na sheria za leseni walizopatiwa.
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku uamuzi wa Manispaa ya Kinondoni kuuza kwa mfanyabiashara mmoja maarufu eneo la ufukwe la Coco Beach.

Pinda alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na madiwani wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya habari kuhusu uamuzi huo unaoonekana kupigwa danadana na kufanywa kwa siri kuvuja na kuandikwa katika vyombo vya habari.

Alisema Jiji la Dar es Salaam limekumbwa na tatizo la migogoro ya viwanja ambalo kimsingi limesababisha kuibuka kwa manung'uniko ya watu kila mara.

"Tatizo la migogoro ya viwanja Dar es Salaam ni kubwa, siku za karibuni tumesikia uuzwaji wa Coco Beach uliofanywa na Manispaa ya Kinondoni. Tumeanza kusikia minong'ono katika hiyo beach. Huyo anayejenga mwambieni ajenge, kwa kuwa kila atakapojenga watu watabomoa.

"Eti wanasema wanaipendezesha. Nauliza wanaipendezesha kwa ajili ya nani? Mnataka kupambana na jamii… kwa kuwa imeamka na haiko tayari kukubali hilo, nyie watu wa Kinondoni hamna la kufanya?" alihoji Waziri Pinda na kuongeza: "Hiyo ni Beach, iacheni hivyo hivyo, tafuteni ‘mabeach' mengine kama vile Rufiji mkajenge." Alisema kutokana na umuhimu wa Dar es Salaam na dhamira ya serikali ya kutaka ionekane kuwa ni kioo cha nchi, katika mwaka ujao wa fedha serikali imetenga sh bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha miundombinu.

"Kwa nafasi ya Jiji la Dar es Salaam, lazima tufike mahali tuishawishi serikali, ili kuwekwe mfumo wa kuiangalia kwa jicho la tofauti na miaka mingine.

"Kila mwaka zitolewe sh bilioni 10 kwa ajili ya mkoa huu, sh bilioni tatu kwa ajili ya kukarabati mifereji na sh bilioni sita kwa ajili ya kufungua barabara kama ile ya Mabibo, Mburahati hadi Kigogo, ili kupunguza msongamano," alisema Pinda.

Aliongeza kuwa, Dar es Salaam ndiyo kioo cha taifa, kwa kuwa ndiyo makao makuu ambapo kuna bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa na pia ndiyo chanzo cha treni ya kwenda maeneo mbalimbali nchini.

Katika maelezo yake, Waziri Mkuu alitoa agizo la kuhakikisha wamachinga wote waliopo katika maeneo yasiyoruhusiwa wanaondolewa na kuwekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa kazi hiyo.

"Chonde chonde Mkuu wa Mkoa, lazima tujitahidi tuwe na nidhamu. Hawa wamachinga wanatakiwa wawe katika maeneo waliyotengewa, kwani nimeona hali ya wamachinga imeaanza kurudi. Tusiwaruhusu wakarudi barabarani," alisema Pinda.

Pia alisisitiza suala la usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam, na kumtaka kila mwananchi katika mtaa wake kujitahidi kuboresha usafi, kwani uchafu unachangia kuzorotesha manispaa kuweza kutoa huduma bora.

Alizitaka manispaa kuvuta kamba ili kuhakikisha suala la kukusanya uchafu linafanywa kwa umakini.

Pia aliagiza manispaa kuzingatia utoaji wa leseni za muziki na vileo kwa watu ambao hawajapewa, na kuwaonya wenye leseni wazingatie taratibu na sheria za leseni walizopatiwa.

juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 10 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hapo Pindisha kula tano, ila tu isiwe ni mbio za sakafuni na jeuri/nguvu ya soda. Maana hamkawii kupindisha

na kukuz , singapore, - 29.05.08 @ 10:01 | #13918

Kwanza kabisa nakupa pongezi Mh. Pinda kwa kuzuia uuzwaji wa Coco Beach. jambo lingine ni kuhusu Jiji la DSM, tatizo kubwa Viongozi wenye dhamana ya kusimamia Jiji hili ni kutokuwa na Vision ya namna gani Jiji hili linapaswa kuwa, na ndio utaona wakati zinafanyika jitihada za kuliboresha bado kuna mambo ya hovyo yanazuka siku hata siku kwa mfano bado ujenzi holela unaendelea kufanyika sio tu pembezoni mwa Jiji hata katikati ya jiji pia.Na huku uswahilini Sheria hazizingatiwi kabisa kwa mfano wenye hizo zinazoitwa Bar (kwa hakika ni Groceries) wanapiga muziki kwa sauti kubwa kabisa kiasi kwamba kunakuwa hakuna kabisa utulivu na wenye dhamana hawachukui hatua yoyote.

na A.S. Mbweni, DSM, - 29.05.08 @ 10:27 | #14021

Hapo Mh.Pinda afadhali umesema ukweli hakuna kuuza na tena akijenga bomoa kama masaki na hakuna fidia. Ili waelewe serikali ina mkono mrefu.

Hapa naendelea kuunga mkono kauli ya Mh. Mkono kwamba haya mambo ya kuuza viwanja mara mbili au maeneo ya wazi wanasambabishwa na elimu mbovu inayoeleta mtazamo finyu juu ya mipango miji. Wataalum wetu je huo sio wakati wakupanua Bunju ,Boko, Mbagala na kigamboni hapo city pabaki hivyo ukiweka usafiri mzuri tena wa usalama wa kufika Bunju na Boko kupitia kwenye bahari na huku kigamboni ukaweka Daraja unafikiri kuna mtu ataagalia hako kacity kwa mtazamo finyu. Hebu tafuteni miradi mkubwa ya kupanua jiji tuacha kuinga wote mjini kwa wakati mmoja na kutoka kwa wakati moja. Kazi kwenu watu wa mipango miji kama kweli mlisoma au kuchugulia mithani pale Ardhi Institute.

na linambasha, Hongkong, - 29.05.08 @ 10:38 | #14026

HIVI NA SWALA LA ROSE GARDEN LIMEISHIA WAPI WAKATI ILE BAR INAJULIKANA KABISA HATA NA MTOTO MDOGO KABISA IKO KATIKA ENEO LA BARABARA????MADIWANI MANFANYA NINI NA MKUU WA MKOA MPO AU MLEWESHWA NA BIA ZA ROSE GARDEN MNASHINDWA KUFATA SHERIA YA MIPANGO MJI??????????????****** ZENU

na munir, dar, - 29.05.08 @ 08:07 | #14036

Nimeshaona kuwa waziri mkuu,amewaona hawa watu wa halmashauri ,niwahuni na ma fi sa di wa haliya juu.Ameamua kiukwe.Na asikomee hapo awafuatilie kuona undai, nilazima watu wa halmashauri wamepewa hongo.Tumechoshwa kusoma taaria za mambo ya halmashauri ,mara kubomoa mara hamishahamisha.Watu wanaishi kama wako kwa makaburu.Maana hujui halmashauri kesho itaropoka nini.Heko Mh WAZIRI MKUU KWA KUWASAIDIA WNYONGE.

na mtzmwenyeuchungu, tz, - 29.05.08 @ 08:27 | #14044

Andikeni majina yenu halisi ili hoja zenu zifanyiwe kazi! tumielewana akina mtzmwenyeuchungu na wenzako!

na mhariri, tanzania, - 29.05.08 @ 09:08 | #14058

kinachotakiwa humu ni hoja na siyo kujua ni nani kaandika, utawajua watu wote wewe? au unataka kuwafanya nini?

na mwenzake na mtzmwenye uchungu, dar, - 29.05.08 @ 09:34 | #14065

Mhe MIZENGO KAYANZA PINDA kama nilivyosema ni chaguo letu wote mungu
amlinde na na mafisadi na atashinda tu
na mimi nipo nyuma yake

na Daniel mugassa, DAR/Tanzania, - 29.05.08 @ 09:42 | #14069

oooh sawa waandishi wa habari muwe wabunifu katika kutatua matatizo ya miji yetu. asilmia kubwa ya matatizo ya Dar es salaam yanatokana na mfumo mbovu wa utwala wa ardhi.

kinondoni wanaongoza kwa rushwa hasa kitengo cha ardhi. kwa nini waandishi hamjafanya uchambuzi wa haya na kuyaweka bayana. Hebu sasa mufanye hivyo na hapo mtakuwa mmesaidia maeneleo ya jiji
letu.

na emanan, germany, - 29.05.08 @ 09:47 | #14071

Dar es Salaam ni Tanzania hii hii. Maamuzi mazuri na ya haraka kama haya yafanyike sehemu zote kuliko na migogoro kama huu wa Dar.

Tunategemea leo au kesho waziri wetu utatoa tena maamuzi kama haya kuhusiana na uwanja wa Nyamagana kule Mwanza. Wananchi hawataki uuzwe na wana sababu nzuri tu wameshazisema,viongozi hawataki kusikia. Wanasubiri mpaka damu imwagike ndiyo waje kukubaliana nao!

Viongozi wanawajibika kwa wananchi. Hivi hawa viongozi wa Mwanza wanawajibika kwa nani? Wakome kutuburuza wananchi maana sie ndiyo tumewafikisha hapo walipo.Watusikilize basi na watambue nasi tuna uelewa wa kutosha pengine hata kuwazidi wao.

Viongozi tujifunze kuwasikiliza wananchi hata walio chini!

na Pius - 29.05.08 @ 10:18 | #14080
[
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom