Fundi Mchundo:
Unajua tunapenda sana mambo superficial. Kuna watu wanakwenda pale kupiga picha za harusi. Eti picha zitoke vizuri. Sioni mantiki yoyote.
Afadhali wangekuwa wanakwenda kwenye beach na ku-spend money hili kufanya mzunguko wa pesa kuwa mkubwa na kuingiza mapato.[/QUOTE
Lakini kwa upande mwingine huu ni uthibitisho kuwa hatuna sehemu za nje zinazopendeza katika jiji letu. Hatuna parks kama walizo nazo wenzetu ( Central Park, n.k.) ambamo wananchi wangeweza kwenda kujifurahisha na kupiga picha za nje zinazopendeza. Tulichobaki nacho ni fukwe zenye kila aina ya uchafu. Oysterbay beach imejaa vipande vya chupa, makaratasi na uchafu mwingine. Hapo Sea view ndiyo maji yameishachafuka kutokana na jiji kumwaga kinyesi kisichokuwa treated baharini! Tumesahau public spaces na kukazania maghorofa. Iko kazi.
Amandla......
Fundi Mchundo:
Hivyo vitu haviji kama manna, chakula kutoka mbinguni. Ni lazima watu wafanyie kazi.
Huwezi kutegemea misaada ya wahisani na baadaye uwe na park za kupumzikia.
Kuna siku nilikwenda Tanganyika library kuangalia ramani za jiji la DSM. Ramani mpaka za miaka ya 70 zilikuwa zinaonyesha sehemu za kupumzikia, mashule, viwanja vya michezo.
Lakini toka Mafundi Mchundo washike nchi, sehemu nyingi zimejengwa nyumba.