FT: Yanga 0-1 Azam | VPL | Benjamin Mkapa | April 25, 2021

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Ni mechi muhimu kwa Yanga kuendeleza matumaini kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara na kurejea kileleni ikiwa imeshinda mechi zake mbili zilizopita. Azam baada ya kusuluhu mechi iliyopita na Dodoma jiji itajitahidi kushinda mechi ya leo.

Yanga yenye alama 57 na michezo 26 itaikaribisha Azam yenye alama 51 na michezo 27 dimba la Benjamin Mkapa kipute kitachopigwa kuanzia saa mbili na robo usiku.

Karata yako unaiweka wapi? Tukutane 2:15 usiku....

=======

00' Mpira umeanza

13' Almanusura Lyanga aiandikiae bao la kwanza lakini anachelewa kuufukia mpira

16' anapewa kadi ya njano

16' Farooq Shikalo anaugusa mpira wa free uliopigwa na Agrey Morris na kuzaa kona ambayo haijazaa matunda kwa Azam

33' Mudathir anapewa kadi ya njano, free kick ya Yanga haijazaa matunda

44' Greyson anaachia shuti kali kuelekea lango la Yanga lakini linagonga mwamba

45' Aggrey Morris anapewa kadi ya njano

45+1' Mpira Mapumziko

=====

45' Mpira umerejea

85' Dubeeee, shuti lake kali kutoka nje ya 18 linaiweka Azam mbele

90' Mpira umeisha kwa Azam kuongeza alama tatu muhimu na Yanga inashindwa kurudi kileleni



Screenshot_20210425-182351~2.png

2753466_175990207_141581277975754_6146913775044064269_n.jpg
 
Back
Top Bottom