WanaJF,
Nilieleza hapa jukwaani kuwa hatuhitaji propaganda. Hatua ya kwanza ni 1) mtupatie taarifa ya ukaguzi mliyofanya kwa Eecretariat ya Maadili ya Umma. Gharama ya ukaguzi haizidi 1,500. lipeni hizo fedha, kagueni file lake, ndiyo muwe na uhalali wa kupiga propaganda hapa. Hili si swala la " nadhani", oh sijui nini. Fsnyeni homework yenu, ndipo watanzania watawaelewa. Vinginevyo, tutawaonya wachochezi, wazushi, watu wadioitakia nchi hii mema, kwa kujaribu kutuondoa kutoka kwa mapambano halisi ya ufisadi na kutuwekea mapambano feki.
2. Wameisha kusema wengi, kuwa na nyumba nje ya nchi, au akaunti siyo kosa, kosa ni ufisadi hasa wa kutumia fedha za umma au kuziiba na au kuhukumu na kuzificha kwenye benki za nje, na hasa Offshore Banks Kama walivyofanya Mafisadi wa ccm kwa fedha za EPA, Tangold, Meremeta ambazo mpaka CCM na Serikali yake wameshindwa kuzitolea Taarifa, siyo humu jamvini, lakini hata Bungeni ambapo Serikali inapaswa kuwajibika. Haya hapa ni propaganda tu, na Kama nilivyosema kwenye post nyingine, hizi propaganda zimefeli hata kabla hazijaanza. Upotoshwaji wowote, ni lazima ujibiwe, tena kwa hoja, na Kama hoja Great Thinkers msiingie kwenye mtego wa kishabiki, jibuni kwa hoja Kama wana nia njema watawaelewa, kama hawataki " hata ukimpigia Gitta Mbuzi haitasaidia".