Freeman Mbowe anamiliki jumba la kifahari Dubai!

Freeman Mbowe anamiliki jumba la kifahari Dubai!

TUNTEMEKE

Platinum Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
4,587
Reaction score
581
Niliipenda CHADEMA ya kipindi cha akina Chacha Wangwe lakini hii ya kikanda zaidi sina imani nayo maana iko kijasiliamali zaidi.

Kama Mbowe, ananunua nyumba Dubai halafu anaandamanisha watanzania ili kikinuka yeye fasta Dubai.
Kutokana na mjadala ambao tayari umeshawekwa hapa na kujadiliwa kwa siku mbili mfululizo , nimeona kuwa kuna watu wanafanya propaganda badala ya kujaribu kuutafuta ukweli wa jambo lenyewe na kuangalia rationale ya jambo linalojadiliwa .

Mimi niliamua kufanya jambo moja la kujaribu kuangalia nini alichokua amedeclare Mbowe kwenye Tume ya maadili ya viongozi kwa mujibu wa Sheria ya maadili ya viongozi wa umma , nimekuwa mambo yafuatayo na kama yupo ambaye anaweza kunichallenge na aje a seem hapa na sio kuhangaika na Gutter politics ,

Mbowe Freeman , kwenye fomu zake alideclare kuwa anamiliki nyumba kwenye nchi zifuatazo,USA, UK, SOUTH AFRICA , DUBAI NA NAIROBI . Nyumba zote hizo alionesha alizinunua lini na zipo maeneo gani kwenye nchi hizo ,

Aidha, kuhusu kumiliki Akounti ya Benki nje ya Nchi alionesha kuwa anamiliki Akaunti iliyopo London Barclays Bank na nyingine iko Hull City, na Benki moja USA .Ila hana Akaunti katika nchi ya Uswisi wala kwenye offshore nyingine zozote zile .

vyote hivyo vipo kwenye fomu ya maadili ya viongozi , pia alionesha kuwa Ana madeni kwenye mabenki mbalimbali ndani nanje ya nchi , na hii ni kwa mujibu wa sheria .

Sasa hapo nimeona nisaidie kutoa ufafanuzi huu, na kama mtu unataka unaweza kwenda pale tume ya maadili ya viongozi wa umma na unalipia kiasi cha shilingi 1,000 tu na unapewa fomu hizo ila huruhusiwi kuondoka nazo wala kupiga picha au kutoa nakala ya fomu (photocopy) .

hivyo , jukwaa kuendelea na kujadiliana kuhusu nyumba moja ya DUBAI , ni vyema jukwaa likarudi kwenye heshima yake ya siku za nyuma ya kuwa mbele ya waandishi kwa kwenda hatua moja mbele katika kuutafuta ukweli wenyewe na sio kuendelea kulifanya jukwaa kuwa kama sehemu ya udaku.

Hivyo, basi badala ya kusubiria wakina Ezekiel Kimwaga , kuandika taarifa za upande mmoja wanaotaka wao kuwa ni Mbowe, Rostam Na Ngeleja tu ndio ambao waliombwa kusaidia timu hiyo katika kutafuta ukweli wa fedha za Uswisi, ni kuwa wabunge wote walioongea siku ya mjadala huo walihojiwa akiwemo Zitto Kabwe ambaye alihojiwa kwa saa nane na timu hiyo, pamoja na wabunge wengine wengi na wafanyabiashara wakiwemo mameneja wa Benki mbalimbali na wamiliki wa maduka ya fedha .

Ni Imani yangu kuwa kwa hili nimeweza kulisaidia jukwaa kuwa na mjadala ambao ni focused , na turejee historia yetu ya kubwa mbele ya media nyingine na sio kama ambavyo leo tunakuwa .........
 
Chadema wanahangaika na wanahamasisha watu wajitolee halafu pesa ya ruzuku mnakwenda kujengea nyumba na hati ya nyumba unaandika jina la mchumba wako hivi kweli ni akili au matope mwakani mtarudisha nyumba na gari chama anayotumia slaa.
 
Chadema wanahangaika na wanahamasisha watu wajitolee halafu pesa ya ruzuku mnakwenda kujengea nyumba na hati ya nyumba unaandika jina la mchumba wako hivi kweli ni akili au matope mwakani mtarudisha nyumba na gari chama anayotumia slaa.

mwakani?hamuwezi kutegemea kuichafua chadema na kujifanya mna uchungu na chama.kama huna vielelezo kwa haya kaeni kimya
 
Ni wale ambao wapo tayari kumtuhumu mtu yeyote hata kama anatimiza wajibu wake. Leo raia mwema wanalaumiwa kisa wameandka mbowe ana jumba dubai. Sasa hapo tatzo lipo wapi hadi raia mwema liitwe kibaraka? Mbowe ana uwezo wa kumiliki nyumba hata london

Kitila kasema msigombane na kila mtu. Hyo ndo point. Msiwe mnabebwa kirahs na hisia kuwa mnahujumiwa kila mda. Raia mwema limekuwa upande wenu kwa muda mrefu.halistahl kufanyiwa hivi. Chungeni wanachama wenu wanaoendeshwa na hisia kuliko ukweli.
 
Hujitambui wewe inabidi nikupe pole kwakuwa hata ukisoma kilichoandikwa huelewi.
Jaribu kushughulisha zaidi akili yako ili uubaini ukweli.
Kama ungekuwa makini ungeona kuwa ni magazeti matatu yaliyotajwa kuwemo katika hiyo project chafu na hatitamuonea aibu mtu yoyote hata kama Una mahaba naye.
 
Kitila kasema
msigombane na kila mtu. Hyo ndo point. Msiwe mnabebwa kirahs na hisia
kuwa mnahujumiwa kila mda. Raia mwema limekuwa upande wenu kwa muda
mrefu.halistahl kufanyiwa hivi. Chungeni wanachama wenu wanaoendeshwa na
hisia kuliko ukweli.

mkuu, ipo siku CHADEMA watakuja kulikana hata gazeti lao Pendwa la Tanzania Daima
 
Hujitambui wewe
inabidi nikupe pole kwakuwa hata ukisoma kilichoandikwa huelewi.
Jaribu kushughulisha zaidi akili yako ili uubaini ukweli.
Kama ungekuwa makini ungeona kuwa ni magazeti matatu yaliyotajwa kuwemo
katika hiyo project chafu na hatitamuonea aibu mtu yoyote hata kama Una
mahaba naye.

we ndo umeandika point? ndo maana jana mlianzisha mada ili kumtetea mhalifu. mwenzenu anapiga mpunga wa maana nyie mnabaki kung'arisha viatu vyake
 
-Mbowe ni Mfanyabiashara anayelipa kodi kwa Mujibu wa Sheria

-Kuna kasumba mbaya imeibuka inayojenga Taswira hasi kwa kila mfanyabiashara.Hatuwezi kujenga Taifa kubwa kwa mentality hizi

Sera ya CHADEMA kulingana na Mrengo wetu kiitikadi ni kuwa Mazingira mazuri ya Biashara na mfumo wa soko uendeshe uchumi ambapo individual efforts zinakua rewarded.

Umaskini si jambo la kujivunia.CHADEMA kimeweka msimamo wake very Clear.Kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na kukuza uchumi kupitia uboreshaji wa maisha ya mtu mmoja mmoja.Tungefuata sera sahihi za kiuchumi na kibiashara basi nchi hii ingekua na mabilionea wengi zaidi na turnover ya wafanyabiashara tunaowaona leo hii ingekua tofauti na turnover zao kwa sasa.

Leo hii kutokana na kuwa na sera ya 'Kuchanganyikiwa" ya kiuchumi na kijamii hatuwezi hata kuweka estimation ya kuwa tutakua na Mamilionea au mabilionea wangapi in 5-15 years baadae.Tunapiga ramli kama waganga wa Kienyeji badala ya scientific forecasting

Hizi mentality za Kimaskini tunazoona zimejengwa kwa muda mrefu na kupaliliwa na mfumo na zinajenga chuki kwa kila mfanyabiashara lakini cha ajabu wanasiasa wezi wezi na waroho wa mali za Umma wanakua celebrated na kushangiliwa kuwa fulani ni Noma.Tunajenga taifa dogo la ovyo lenye uwezo wa kupiga reverse kimaendeleo tu na sio zaidi ya hapo.

Kuhusu Malicious intent kwa kuandika story zenye malengo mabaya kisiasa ni.jambo la hatari sana

Raia Mwema nimekua nikiliheshimu na hadi sasa nawapa benefit of doubt ili niwe rational.

Ukweli wa jambo lolote ni suala la Muda.Sidhani sasa kama Raia Mwema wamebadili dimension ya Legacy yao waliojenga kwa muda Mrefu kwa kuamua kwenda Gutter na irresponsible Journalism.

Jenerali Ulimwengu ana heshima kubwa nchini kitaaluma na katika weledi.Sidhani kama anaweza kuruhusu mambo haya

Wakati huo huo hatuwezi kupuuza kila lisemwalo maana kuna mambo mengi.Uchaguzi ndani ya CHADEMA unakaribia,Hoja ya Kuficha Mabilioni nje inaweza kuwa diluted kwa mbinu mbalimbali na pia kwa kuwa kuna wanasiasa wanahusika na hoja hii wanaweza kuitumia kisiasa kujinufaisha na kuwalenga maadui zao kwa sababu wanazozijua ambazo no doubt ni za Kisiasa

Najua wanapita wahariri hapa,Sasa sote tujiulize ;

Je,Tunapokubali kutumia vyombo vyetu kwa maslahi ya kisiasa ya watu wachache tunaitendea haki jamii?Je,misingi ya Demokrasia na mhimili wa media tunautendea haki?Tunakuza au tunafifisha tasnia ya Habari?
 
Ni wale ambao wapo tayari kumtuhumu mtu yeyote hata kama anatimiza wajibu wake. Leo Tanzania Daima wanalaumiwa kisa wameandka kikwete ana jumba dubai. Sasa hapo tatzo lipo wapi hadi raia mwema liitwe kibaraka? Kikwete ana uwezo wa kumiliki nyumba hata london

Kitila kasema msigombane na kila mtu. Hyo ndo point. Msiwe mnabebwa kirahisi na hisia kuwa mnahujumiwa kila mda. Raia mwema limekuwa upande wenu kwa muda mrefu.halistahl kufanyiwa hivi. Chungeni wanachama wenu wanaoendeshwa na hisia kuliko ukweli.
 
kuna wanachama wengine wanatembea na sumu mifukoni!inabidi wabadilike kabisaa maana wana sera nzuri ila tabia zao ni chafu hazina mfano,wengi wao top leaders and mp's hawana maadili ya kuongoza nchi,i wonder watu wanawashangilia kumbe hawajui kushika dola kuna hitaji watu waadilifu ambao hiki chama wapo wachache sana
 
Mwandishi Wetu

Novemba 24, 2010

Polisi Uingereza wamchunguza mwanawe

MTOTO wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa anayeitwa Frederick Lowassa anachunguzwa na Kitengo Maalumu cha Polisi wa Kimataifa wa Uingereza wanaofuatilia utata wa uhamishaji fedha kutoka Tanzania, Raia Mwema limedokezwa.

Fedha hizo zinahusishwa na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya pauni za Uingereza 475,000 (takriban Shilingi bilioni moja) katikati ya Jiji la London.

Hata hivyo, watu walio karibu na Frederick wameelezea kwamba kijana huyo hakuwahi kununua nyumba; bali aliwahi kutaka kupanga kwa ajili ya kuishi akiwa masomoni nchini Uingereza na fedha nyingine alizituma kwa ndugu yake aishie nchini humo.

Nyumba ambayo inatajwa katika maelezo ya awali iko mtaa wa Leinster Gardens, jijini London.

Hata hivyo, hakuna ofisa yeyote wa Serikali ya Tanzania aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo, pamoja na kuwapo taarifa kwamba tayari vyombo vya dola vya Tanzania vimekwisha kuhusishwa katika uchunguzi huo.

Maofisa wa Polisi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) wanaohusika na uchunguzi wa fedha haramu, wamekwepa kuzungumzia suala hilo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, hakuweza kupatikana, na alielezwa kuwa nje ya nchi kikazi.

Ofisa wa CID aliyeelezwa kuongoza kitengo kinachochunguza makosa ya uhalifu wa fedha na nyaraka, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Samson Kasala, alikanusha kufahamu chochote kuhusiana na suala hilo, kabla ya kukata simu alipohojiwa na Raia Mwema kuhusu taarifa hizo.

Taarifa zinaeleza kwamba Kitengo cha Ufuatiliaji wa Fedha Haramu (Financial Intelligence Unit-FIU) kilichopo chini ya Wizara ya Fedha nchini, kilipokea taarifa kutoka Polisi wa Kimataifa wa London, Uingereza, wakitaka taarifa muhimu kuhusiana na Frederick, kabla ya kitengo hicho kuomba msaada wa polisi.

Hata hivyo, Kamishna wa FIU, Herman Kessy, hakuweza kupatikana wiki iliyopita akielezwa kuwapo nchini Afrika Kusini kikazi, lakini hata aliporejea wiki hii Raia Mwema ilikosa ushirikiano kutoka kitengo hicho Jumatatu wiki hii.

FIU imeanzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (Anti-Money Laundering Act-2006) kwa kuundiwa kanuni mwaka 2007, lakini hadi sasa kitengo hicho kimekuwa kikiendeshwa na maofisa watano tu, Kamishna Kessy, mchambuzi mmoja, mtaalamu wa mawasiliano na wasaidizi wawili wasio wataalamu, kitengo kilichopaswa kuendeshwa na watu wengi zaidi kutokana na unyeti wake.

Habari zinaeleza kwamba hata ofisa wa Polisi aliyewahi kuhamishiwa FIU kwa kazi maalumu alijikuta akitengwa na kutopangiwa kazi na maofisa hao ambao wengi wanatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya kuwa ‘wameaminiwa' sana na uongozi wa juu wa serikali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo bado zinafanyiwa kazi, Frederick ambaye baba yake alijiuzulu Waziri Mkuu kwa kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyokabidhiwa kwa kampuni tata ya Richmond Development LLC, anadaiwa kufanya mawasiliano kupitia kampuni ya uwakala iliyotajwa kwa jina la ‘Mishcon'.

Nyaraka alizowasilisha, zilidai kuwapo ubia kati ya mtuhumiwa huyo na kampuni tatu ikiwamo Integrated Property Investment(T) Ltd na Barare Ltd Company.

Mkataba huo unaonyesha kuwa Frederick Lowassa ana hisa kwenye kampuni hizo, na kwamba fedha za ununuzi wa nyumba hizo zinatokana na fedha za malipo ya hisa anazopata kutokana na kampuni hizo.

Hata hivyo, mkataba huo unaonyesha kusainiwa Machi 25 mwaka 2009 siku moja baada ya Frederick Lowassa kusaini mkataba kati yake na kampuni ya Mishcon kama wakala wake katika ununuzi wa jengo hilo.

Pia aliwasilisha nyaraka zinazoihusisha kampuni ya Alphatel kama moja ya kampuni ambayo pia yeye ni mkurugenzi wake ambayo pia ni chanzo chake kingine cha fedha anazotumia kununua jengo hilo.

Taarifa zimedokeza kuwa ununuzi huo ulikwama baada ya kushindwa kutoa malipo hayo kwa mujibu wa mkataba kati yake na wakala wa ununuzi wa nyumba hiyo (kampuni ya Mishcon) ambao ulimtaka awe amekamilisha kulipa fedha hizo kabla ya Aprili 14, mwaka 2009.

Hata hivyo, siku chache baadaye ndani ya mwezi huo wa Aprili, Frederick aliipelekea Mishcon kiasi cha pauni za Uingereza 199,940 zikitokea kwenye kampuni ya ununuzi fedha ya Wall Street Exchange.

Aidha kiasi cha pauni 100,000 kiliingizwa kwenye akaunti ya kampuni hiyo hiyo ya Mishcon kwa fedha taslimu katika mikupuo 12 tofauti zikitokea kwenye matawi tofauti ya benki ya NatWest Bank plc iliyoko Kaskazini mwa Jiji la London.

Raia Mwema limeelezwa kuwa mazingira ya kuingizwa fedha hizo kwenye akaunti ya wakala huyo ( Mishcon) ndiyo yameifanya Taasisi ya SCD 6 Economics and Specialist Proceeds of Corruption Unit ya Uingereza inayosimamia uchunguzi wa sakata hilo kuwa na mashaka makubwa kuhusu uhalali wa fedha hizo.

Kutokana na mazingira hayo, SCD 6 Economic and Specialist Crime Proceeds of Corruption Unit yenye ofisi zake Victoria Block, New Scotland Yard, London, ililazimika kuwasiliana na FIU ikitaka maelezo ya awali kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi kuhusu fedha hizo.

Raia Mwema iliwasiliana na Fred ambaye alikana kununua nyumba Uingereza lakini alikiri kuwahi kutuma fedha huko. Aliliambia Raia Mwema pia kwamba hajawahi kuhojiwa na yeyote kuhusu suala hilo, na pia kwamba hana taarifa kuwa polisi wa Uingereza wanampeleleza.

Hata hivyo kwa upande mwingine, gazeti hili limebaini kuwa, maelezo ya awali ambayo yalitakiwa kutoka Tanzania na makachero hao wa Uingereza, ni pamoja na kutaka kufahamu kama kweli Frederick Edward Lowassa amezaliwa Agosti 26, 1977, Mwanza Tanzania na anamiliki hati ya kusafiria yenye namba AB 109402 iliyotolewa Tanzania na kwamba anwani yake nchini Uingereza ni 71 Hendrix Drive, Milton Keynes, MK8 0DY.

Pia makachero hao waliitaka Serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi wakitaka kujua kama Frederick Lowassa ni mbia katika kampuni za Alphatel Partnership (Tanzania) Barare Ltd na Intergrated Tanzania Limited, kampuni ambazo zimefahamika kumilikiwa na familia ya Lowassa.

Asasi hiyo ya Uingereza pia imeomba kujua kama FIU wana taarifa zozote za uhalifu dhidi ya Frederick Lowassa na kama baba yake Edward Lowassa anachunguzwa kwa tuhuma yoyote ya rushwa na mamlaka za uchunguzi wa rushwa nchini Tanzania kuhusu fedha haramu.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na vyombo vya dola, ulielezwa na taarifa hizo kwamba Frederick Lowassa si mbia katika kampuni hizo na kwamba Barare Ltd wenye hisa ni Edward Ngoyai Lowassa mwenye hisa 500 na Regina Mumba Lowassa mwenye hisa 500 huku wakurugenzi wakiwa ni hao hao.

Ofisa wa Uingereza anayesimamia uchunguzi huo, George Simpson, ameliambia Raia Mwema kupitia barua pepe kwamba kanuni za uchunguzi kuhusiana na kesi zenye mguso wa kisiasa huwazuia kukanusha au kuthibitisha kuhusu uchunguzi unaoendelea hadi pale wanapofikia hatua ya kukamata mtuhumiwa ama anapofikishwa mahakamani.

CHANZO: Raia Mwema
 
Mkuu si huyu yupo ukoo ule ule,nyani haone kundule,mbowe hachafuki kwa tope la handeni wala kisesa,acha tucheze nao tu kila sound wanayotuletea ila siku mziki ukizima tutatafutana
 
watu wanamikakati ya muda mrefu, na muda mfupi, kwa hiyo nyumba ya dubai, kikinuka tu, huyoo anaishia zake kupumzika, sasa wanaachwa wale wasiojitambua kuonja joto ya jiwe, hii si sawa, watu waamke sasa..wanasiasa kama hawa hawana mema na nchi
 
nampongeza Mbowe kwa kuwa na nyumba nzuri, sawa na JK na viongozi wengine... nasikitikia mangula wa watu, kachoka hadi aavaa suti na adidas sijui nae kama ana jumba au ndio anajenga
 
Duh mjasirimali Ben Saanane kama kawaida upo kumtetea lezi wako Mbowe!

mbowe na familia yake ni wafanya biashara wa siku nyingi na kila mtanzania anajua hilo ,isipokua maccm bongo lala
kama munawasi wasi naye nendeni mkamuchunguze muumbuke wenyewe .kuhusu mafisadi mulioficha pesa ulaya hamuta salimika msitumie issue ya mbowe kua na nyumba dubai kutuondoa kwenye hoja ya msingi
Niliipenda CHADEMA ya
kipindi cha akina Chacha Wangwe lakini hii ya kikanda zaidi sina imani
nayo maana iko kijasiliamali zaidi.

Kama Mbowe, ananunua nyumba Dubai halafu anaandamanisha watanzania ili
kikinuka yeye fasta Dubai.
 
Last edited by a moderator:
Chadema wanahangaika na wanahamasisha watu wajitolee halafu pesa ya ruzuku mnakwenda kujengea nyumba na hati ya nyumba unaandika jina la mchumba wako hivi kweli ni akili au matope mwakani mtarudisha nyumba na gari chama anayotumia slaa.

Zaha ndio TUNTEMEKE?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom