Reginald L. Ishala
JF-Expert Member
- Jun 18, 2011
- 3,810
- 6,801
Mtuze na viongozi wengine katika hiyo Tume Ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Unarudia yaleyale hakuna
ambaye hajasema Mbowe sio mfanyibiashara kinachoangaliwa na uhalali wa
upatikanajia wa pesa na kama taratibu za nchi zilikiukwa; pesa nyingi
zinazohifadhiwa Uswisi ni magumashi matupu ndio maana hata wao wenyewe
Uswisi wanazisaidia serikali za Afrika kukamata hizo pesa.
Mkuu.....kirahisi kabisa.
Mbowe ni mfanyabiashara sku nyingi kitambo. Ana kampuni nje ya nchi - Dubai, ana nyumba SA, Uingereza na US.
Tatizo ni kwamba, ana tuhuma za wizi wa mali ya umma? ana mashtaka ya ukwepaji kodi au kavunja sheria ya kodi? yeye au makampuni yake?
Kama hapana, basi tuwe na reserve ya maneno.
Watanzania tumezidi wivu na maneno maneno tu.
ni kweli kabisa, tunataka kulinganisha Mbowe na public servants wanokwiba mno
sio lazima sana...wangeweka hata picha moja tuzione.
nampongeza Mbowe kwa kuwa na nyumba nzuri, sawa na JK na viongozi wengine... nasikitikia mangula wa watu, kachoka hadi aavaa suti na adidas sijui nae kama ana jumba au ndio anajenga
TUNTEMEKE, wajua dhahiri kwamba hata Biblia inasema kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima.Chadema wanahangaika na wanahamasisha watu wajitolee halafu pesa ya ruzuku mnakwenda kujengea nyumba na hati ya nyumba unaandika jina la mchumba wako hivi kweli ni akili au matope mwakani mtarudisha nyumba na gari chama anayotumia slaa.
nampongeza Mbowe kwa kuwa na nyumba nzuri, sawa na JK na viongozi wengine... nasikitikia mangula wa watu, kachoka hadi aavaa suti na adidas sijui nae kama ana jumba au ndio anajenga
Chadema wanahangaika na wanahamasisha watu wajitolee halafu pesa ya ruzuku mnakwenda kujengea nyumba na hati ya nyumba unaandika jina la mchumba wako hivi kweli ni akili au matope mwakani mtarudisha nyumba na gari chama anayotumia slaa.
hahaha! Mwanangu mangula ndo kiongoz mwenye moyo wa kitajiri kuliko wote ccm, amejiridhikia na hicho kidogo alichonacho.
mwizi tu naye. Kumiliki nyumba nchi za watu ni ufisadi
Kubwa kinga
Baba yako aliwahi kuwaamhia watu 'go to hell'. Na mimi nakuambia 'go to hell' kama ukishindwa kuthibitisha Mbowe ana majumba lukuki.
mwizi tu naye. Kumiliki nyumba nchi za watu ni ufisadi
kwa ufafanuzi huu uliokwenda shule na unaorudisha heshima ya JF, Invisible tunaomba muongozo wako huyu mzushi Tuntemeke au hii taasisi inayotumia Id ya Tuntemeke wanapewa adhabu gani?TUNTEMEKE, wajua dhahiri kwamba hata Biblia inasema kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima.
Ndugu yangu Maxence husema daima ficha upumbavu wako, onesha hekima zako.
Sasa, kwa heshima na taadhima, ngoja nikujibu ulichoandika hapo maana ni UPUMBAVU uliokithiri.
1. Hivi NANI ambaye anawajua wafanyabiashara hapa Dar (au Tanzania) asiyejua kwamba Freeman Mbowe ni mfanyabiashara makini ambaye alianza ZAMANI kazi zake hizo KABLA ya kuingia CHADEMA? Unadhani hakuwa na malengo? We unakurupuka kwa kusema CHADEMA wanatumia pesa za ruzuku kujijengea majumba ya kifahari, una USHAHIDI GANI?
2. Unaonesha akili zako za matope kwani unasema wanaandikisha majina ya wachuma wao; UMEZIONA?
3. Magari wanayotumia Dr. Slaa na wenzake, UMEONA KADI ZAKE?
Siku hizi kila kitu kiko documented. Kama wataka kujua, si unaenda tu pale Tume ya Maadili? Unalipia ada yao, buku tu, kisha unapewa faili, unasoma, unachukua kalamu na karatasi, unanakili, waondoka zako.
KWA TAARIFA YAKO, NA HILI NI KWA KUWA NINAMFAHAMU VEMA FREEMAN MBOWE, NA SI KWAMBA NAMSEMEA, hizo nyumba alizipata SIKU NYINGI kabla ya kuingia CHADEMA. Hakatazwi, na hakuna sheria inayomkataza Mtanzania kuwa na nyumba nje ya nchi; kama ipo, siijui. SI UTOVU WA MAADILI kufanya hivyo. Utovu huo ni pale unapochukua pesa ambazo SIO ZAKO na kuzifanyia kazi YAKO.
Mapato na matumizi ya Vyama vya Siasa yanakaguliwa. Mbowe hana shida na hizo pesa za ruzuku kama walivyo baadhi ya wanasiasa wa CCM. Hana shida hiyo, hajawahi kuwanayo, hatakuwanayo.
ELEWA FIKA KWENYE HIZO AKILI ZAKO WEWE ZA TOPE!
Usikurupuke kuwahukumu watu bila ya kuwa na ushahidi. Na ninawaambia Moderator na Invisible wakupe warning, ukirudia upuuzi huu UNAPIGWA BAN ya miezi 3, ushike adabu yako!
Mbona Samuel Sitta alitumia fedha NYINGI - Bilioni Moja - kujijengea Ofisi yake pale Tabora Mjini, huku mji ule ukiwa UMEDORORA KUPITA KIASI, na HAMKUSEMA? Watu wana shida Jimboni, yeye ajiwekea ufahari. Hajaitwa na Kamati Kuu ya Maadili ya CCM na HATAITWA!
mwakani?hamuwezi kutegemea kuichafua chadema na kujifanya mna uchungu na chama.kama huna vielelezo kwa haya kaeni kimya