Tuwakumbuke pia Wenge Musica BCBG(Bon Chic Bon Genre) kundi ambalo lilianzishwa tarehe 11 Julai mwaka 1981 na vijana(wakati huo) watanashati tisa(09) Jean-Bedel Mpiana Tshintuka(JB Mpiana-muimbaji),Ngiama Noël Makanda(Werrason-muimbaji),Adolphe Dominguez(muimbaji),Blaise Bula(muimbaji),Aime Bwanga(muimbaji),Didier Masela(mpiga gitaa la besi),Alain Makaba(Mpiga gitaa la Solo),Alain Mwana(Zing Zong-Mpiga gitaa la kati),na Maradona(mpiga ngoma-drums)
Vijana hawa waliishika sana Zaire enzi hizo na Afrika kwa ujumla kwa muziki wao mtamu kabla ya kutokea kutokuelewana na hatimaye kugawanyika mwaka 1997.Tangu kuanzishwa mwaka 1981 mpaka kugawanyika mwaka 1997 Wenge Musica BCBG walitoa Albam nane9kama zinavyoonekana hapa chini:
-Bouger-Bouger ilitokamwaka 1988
-Kin é Bougé ilitoka mwaka 1991
-Pleins Feux hii ilitoka kwa mara ya kwanza mwaka 1992 lakini walikuja kuirudia upya mwaka 1996
-Kalayi Boeing ilitoka mwaka 1993
-Les Anges Adorables 1&2 mwaka 1994
-Pile ou Face (Albam ya solo ya Alain Makaba) ilitoka mwaka 1995
-Pentagone ilitoka mwaka 1996
-Feux de l'amour (albam ya solo ya JB Mpiana ambayo inadaiwa ndo chanzo cha mgogoro mkubwa uliopelekea mgawanyiko wa Wenge) ilitoka mwaka 1997
Hiki ndicho kikosi kizima cha Wenge Musica tangu imeanzishwa mwaka 1981 mpaka ilivokuja kuanza kusambaratika rasmi mwaka 1997 kwa kuondokewa na nguzo zake/waanzilishi kama Werrason,Blaise Bula,Adolph Dominguez na Didier Masela(Aime Bwnaga yeye ndo mwanzilishi wa kwanza kujiengua mwaka 1986 na baadae kuanzisaha bendi ya Wenge Kumbela mwaka 1994).
Waimbaji:
. JB Mpiana, 1981-1997 ;
. Werrason Ngiama, 1981-1997 ;
. Blaise Bula, 1981-1997 ;
. Aimé Bwanga, 1981-1986 ;
. Adolphe Dominguez, 1981-1997 ;
. Alain Mpela, 1985-1997 ;
. Manda Chante, 1986-1993 ;
. Marie Paul, 1984-1991 ;
. Ricoco Bulambemba ;
. Aimélia Liass, 1993-1997 ;
. Ferré Gola, 1995-1997.
Wapiga magitaa:
. Didier Masela (bass) 1981-1997 ;
. Blaise Kembo (rhythm) ;
. Alain Makaba (solo, rhythm, bass) 1981-1997 ;
. Alain Mwanga "zing-zong" (solo, rhythm) 1981-1991 ;
. Djolina (rhythm) 1985-1990 ;
. Patient Kunsagila (bass) 1992-1997 ;
. Ficarré Mwamba (solo,rhythm) 1992-1997 ;
. Aridjana (rhthm)1984-1990 ;
. Burkina Faso (solo, rhythm) 1993-1997 ;
. Christian Mwepu (bass, rhythm) 1994-1997 ;
. Japonais Maladji (solo, rhythm) 1996-1997.
Wapiga ngoma:
. Maradona (drums) 1981-1989 ;
. Titina Mbwinga (drums) 1985-1997 ;
. Djo mbonda (tumba) 1992 ;
. Ali Mbonda (tumba) 1993-1997.
Waimbaji wanaoghani(marapa) :
. Ekokota Roberto 1988-1997 ;
. Full King 1986-1993 ;
. Tutu Caludji 1993
Kudhihirisha jinsi BCBG walivyokuwa bora mpaka sasa kuna makundi karibu kumi na moja(11) yameanzishwa ambayo ni zao la mgawanyiko wa Wenge Musica,makundi hayo ni haya hapa chini:
-Wenge Maison Mère(Werrason)
-Wenge BCBG(JB Mpiana)
-Wenge Reference(Manda Chante)
-Wenge Tonya Tonya(Adolphe Dominguez)
-Wenge Pondération 8(Blaise Bula)
-Wenge Kumbela(Aime Bwanga)
-Wenge El-Paris(Marie Paul)
-Les Marquis de Maison-Mere(JDT Mulopwe,Sergie Mabiala kutoka Wenge Musica Maison Mere)
-Les Marquis de Gaulois(Ferre Gola)
-Les Marquis de Samourais(Bill Clinton Kalonji kutoka Wenge Musica Maison Mere)
-Génération A(Alain Mpela)