Nashukuru kwa hilo, ndiyo namfahamu nilikuwa mlimani wakati akifundisha na niliwafahamu baadhi ya rafiki zake ( ambao nadhani unawafahamu waalimu mashuhuri wa kiswahili na theatre Arts pale milmani) siko comfortable kutaja majina yao na hata jina la marehemu dada ya Patrick. Ilijulikana kama angekufa kwa hiyo hao marafiki walikuwa wana huzuni sana siku za mwisho. Alikuwa jasiri sana, alipotoka matibau aliweza sikumoja kushiriki katika moja ya maonyesho ya Paukwa group ( akiwa mmoja wa P.wanasanaa walioonyesha siku hiyo, nadhani mchezo ulikuwa Lina Ubani by P. Mlama)
Huyu mama walikuwa marafiki sana na dada yangu miaka hiyoo. Infact alikuwa kama dada yake/mtani wake kwani wakati marehemu sister akianza kazi Roleza, huyu mama alikuwa hapo tayari. Ila tulipohamia Dar, nilikaa mwaka mmoja na nikarudishwa kijijini huko Sikonge. Kutoka hapo sikufanikiwa kumuona tena. Mikiki ya maisha ilifanya wakapoteana hadi alipokuja kupata PhD na akawa amerudi Tanzania akiwa tayari mgonjwa. Alianza kutafuta contact za rafiki zake wote. Basi wakawa wakiona tena karibu kila siku.
Hivyo, hao walimu wa UDSM kusema ukweli wengi siwafahamu na kwa sababu sikusomea hapo, na sikusoma masomo ya ARTS, siwafahamu. Hiki kitabu chake na cha huyo Mlama kama sikosei tulitumia kwenye Kiswahili mtiani wa form 4. Ilikuwa ni hadithi ya kijana wa Kigogo aitwaye Chonya of Chilonwa.
Turudi kwenye wanamuziki:
Lovi Longomba ni mwanamuziki wa Kikongo ambaye baba yake pia alikuwa mwana muziki kwenye kundi la Franco and TP OK Jazz. Lovi alikuja kuishi Tanzania na baadaye akahamia Kenya na mwisho akarudi tena Tanzania hadi alipokuja kupata ajali na kufariki. Watoto wake ni hawa wanajiita LONGOMBAS na mdogo wake ni Awilo Longomba.
Huyu jamaa alitesa sana wakati wa bendi ya Shika Shika na baadaye kuwa SUPER MAZEMBE. Super Mazembe nilifanikiwa kuja kuwaona walipokuja Dodoma miaka ya 80 mwanzoni. Ilikuwa furaha kusikiliza wimbo wa Kasongo, Nanga, Nabimakate na nyingine nyingi.
lla hawa jamaa nao naona walikuwa waki-copy. Ila copy yao kwa kweli imeniuwa maana walienda wakawacopy THE BEETLES. Hebu sikilizeni wimbo huu...................
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=pzAsLAfqmVk[/ame]