FMES: Tuwakumbuke Wanamichezo Africa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FMES: Tuwakumbuke Wanamichezo Africa!

Discussion in 'Jamii Photos' started by Field Marshall ES, Dec 27, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Wakuu wote JF heshima mbele sana,

  Ni vyema wakati mwingine tukawakumbuka wanamichezo wetu Africa, unajua majuzi nilienda huko Broadway NYC, kuona ile play maarufu sana sasa hivi ya Fela, ambayo iko sponsored na P'Didy akishirikiana na Jay-Z, what a play inayomuhusu Marehemu Fela Ramson Kuti mwanamuziki wa zamani maarufu sana huko Nigeria, na dunia nzima.

  - Ndio nikaona kuwakumbuka wanamichezo wetu ni halali na hasa wanamichezo wote waliowahi kuwika zamani na sasa, katika Tanzania na hasa bara letu zima la Africa.
  sana.

  Respect.

  FMEs!
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mbaraka Mwinshehe RIP: Tanzania Music Legendary.

  [​IMG]

  Respect.

  FMEs!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Patric Balisidya RIP: Another Tanzania's Music Icon.  [​IMG]


  Respect.

  FMEs!
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Wanamuziki wetu wenye asili ya ki-Zaire, kushoto Marehemu Freddy Ndala Kasheba "Supreme" na kushoto ni Kikumbi Mwanza Mpango au "King Kiki" wakiwa pamoja. Wanamuziki hawa wakongwe ambao waliwahi kupiga kwa pamoja ujanani huko kwao, katika bendi moja iliyojulika kwa jina la Nkashama Nkoy, walikuja kuwa maadui wakubwa walipohamia Tanzania, ambapo Kiki alihamia bendi ya Marquis Du Zaire ya Chinyama Chiyanze.

  - Baadaye wanamuziki hawa walikutana tena kwenye bendi ya Mzee Hugo Kissima, kule Safari Resort, yaani Orch. Safari Sound ambapo Kiki ndiye aliyekua ametangulia baada ya kumpokea mwanamuziki mwingine Mbombo wa Mbombo Kamunembu na mtindo wake wa "604", Kiki alianzisha mtindo wa "Masantula" ambao uliwika sana enzi hizo za 80s, na hasa vibao kama "Mimi msafiri bado niko njiani" na "Emergey Marie Jose", lakini baadaye maelewwano yake na mmiliki wa bendi yalianza kupungua ndipo Freddy Ndala Kasheba akaja na hapo hapo Kiki akaondoka na kuanzisha bendi yake mpya ya " Orch. Double O".

  - Mpaka walipofikia umri ulioenda kidogo, ndipo masoko yao kimuziki yakaanza kupungua, lakini akatokea Captain Komba na kuwapatia vyombo vya kisasa ambapo wakongwe wote wa muziki kutoka Zaire waliowahi kuwa maarufu sana nchini wakajiunga kwa pamoja na kupiga muziki kila weekend pale Oysterbay Officers Mess. Waliojiunga ni pamoja na Kiki, Kasheba, Kassongo Mpinda, Nguza Viking, Asossa Tshimanga na wengineo. Kibao chao maarufu kilikuwa "Nainua mikono Mama Kitambaa cheupe", ambacho mpaka leo bado ni lulu kubwa sana kwa shuguli zetu hasa za maharusi.

  - Mungu amuweke mahali pema peponi Marehemu Ndala Kasheba, ambaye kwa mara ya mwisho nilimuona kijijini Mvumi kwenye harusi ya Mama Kilango. Muziki wetu Tanzania, kihistoria unachochewa sana na hawa wa-Zaire katika kuendeleza utashi wake technically, na siku hizi Kiki bado anapiga muziki kama kawaida.

  [​IMG]

  Bravo!

  Respect.


  FMEs!
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Marijani Rajab RIP: Another Tanzanian Music Icon.

  [​IMG]  Mungu amuweke mahali pema peponi.

  Respect.


  FMEs!

   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Shaaban Dede & Hassan Bitchuka: Tanzania's Music Icons.


  [​IMG]


  Wanamuziki kuchoto Shabaan Dede "Sauti ya zege" na Mkongwe Hassan Rehani Bitchuka "Stereo", hawa nao ni moto wa kuotea mbali sana na wamekuwa wakipiga katika bendi mbali mbali nchini na kuweza kujipatia umaarufu mkubwa sana.

  - Shabaan Dede, aliwahi kupigia bendi ya Sikinde, halafu Bima Lee na Sikinde tena, Bitchuka amepigia bendi ya Msondo Ngoma na Sikinde, wote wameweka histrotia nzito sana kumuziki kutokana na umahiri wao wa kumiliki sauti nyororo sana.

  Respect.


  FMEs!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Previous post jamaa alipomtaja Shaban Marijani nadhani alimaanisha Jabali la Muziki Marijani. Nami najipanga nitoe wasifu wake ukiwemo wimbo wa Georgina ambao ni kisa cha kweli cha binti alikisoma Zanaki na Marijani Tambaza miaka ya 70p. Marijani alimpenda binti wazazi wake walipogundua, wakamhamishia boarding kimzobe mzobe ndipo Marijani huku amekunja madaftari yake ameyakunja na kuyasunda mfuko wa nyuma wa kaptula ya shule huku shati amechomolea akipita kwenye coridors na kupandisha ngazi kuelekea summit huku akilakamika kwa kujiimbia 'umeondoka Georgina , umeniachia masikitiko....
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  TRIO MADJESI
  et
  ORCHESTRE SOSOLISO

  TRIO MADJESI - Ainsi MAtadidi Buana Kitoko Mario (Angola) , DJEskain Loko Masengo (Congo Brazzaville) , SInuku Saak-Saakul (Zaire)

  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  - Wakuu naomba kutoa tribute zangu kwa hawa wakulu wa Orch. Sosoliso kutoka Zaire, ambao sidhani kama wapo tena katika uliwengu wa muziki, lakini hawa siku zote wamekua my inspiration kwani zamani nikiwa dogo nilikuwa ninawazimia sana na mpaka leo nimeweza kuwa na collections zao zote. Siku zote nimekwua ninazimishwa sana na vibao vyao kama "Photo madjesi" na ule wimbo wao wa kusifia timu ya mpira ya Zaire National Team, iliyokuwa timu ya kwanza Africa kutuwakilisha World Cup Final.

  - Kwa wale mnaokumbuka basi mnajua jinsi tulivyokuwa tukijazana pale kwenye banda la West Germany, kule uwanja wa maonyesho ya saba saba in the 80s, kuangalia video za mechi zao, kina Kazadi Mwamba, Mayanga Maku, Lobilo Mavuba, Kiliniki wa kiliniki, Lofombo, Mweku na wengineo kama kina Moseka, aaahhhaagarrr! ingawa walifungwa sana lakini it was nice to see katika nchi ya bongo.

  - Long live Sosoliso, chini ya uongozi wa Matadidi Mabele Mwana-Kitoko!

  Respect.


  FMEs!
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Mwanamuziki, maarufu sana marehemu TX-Moshi William ambaye alianzia Polisi Jazz, na kuishia Msondo Ngoma, hapa akiwa kwenye mazoezi.


  Respect.


  FMEs!
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  fmes..
  thanx a lot.
   
 11. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,784
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280

  unanikumbusha mbaaali sana!
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Francois Luambo Makiadi


  <!-- contentHeader --> [​IMG]
  Respect.


  FMEs!
   
 13. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sama Field marshall hasa hasa kwa wasifu wa Patrick Balisidya. Nillikuwa napenda sana jinsi muziki wake ulivyokuwa na asili ya Kitanzania, hakuwa naiga mziki wa Zaire kama baadhi ya wanamuziki wa kitanzania wa miaka ya 70. Siku hizi hatuna hayo utafikiri hatuna utamaduni wetu, hakuna mtu mwenye guts za kuanzisha kitu original ( Naelewa naelewa kuwa labda ukianzisha mziki kwa ajili ya art hutapata pesa lakini wakati mwingine ni vizuri kujitoa mhanga)
  Wimbo mwingine mzuri wa Balisidya ni ule aliomtungia dada yake siku ya harusi. ( kuoana ni jambo lasifa nafikiri ulikuwa ukianza hivyo)
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Wilson Peter & Peter Kinyonga; Simba Wanyika Original.

  Simba Wanyika Biography
  Respect.


  FMEs!
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Dah,yaani hapa tuko pamoja kabisa mkuu.,Thread nzuri sana hii mzee.Nami naja na mchango wangu soon..Binafsi daima navutiwa na hawa jamaa wa Les Wanyika..Na kwa nyumbani pale ni Jabali la Muziki Marijani Rajab bila kuwasahau Vijana Jazz wana Chakachua-Air Pambamoto-Saga Rhumba..Ingekuwa vipi Hemed Maneti angekuwa bado hai???...Pamoja sana mkuu
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Verkys Kiamwangana Wazela Mbongo Mateta: Orh. Veve Intern.

  Huyu ndiye Mwanamuziki mashuhuri sana zamani nchini Zaire, ambaye alianzia bendi ya Lwambo Makiadi, Franco kama mpiga Tarumbeta na uimbaji. Baadaye alijitoa bendi hiyo na kuanzisha bendi yake ya Orch. Veve Intern, ambayo iliweza kuteka hisia za wapenzi wengi wa muziki duniani na hasa upigaji wake wa tarumbeta.

  - Kwa wale mnaokumbuka vibao kama "Muanamburu", "Nakoma Juste", "Vivita", "Mikolo Mileki Mingi", na "Bi-Mazena" ilikuwa ni miziki ya moto wa kuotea mbali sana. Baadaye Verkys alifanikiwa sana kimuziki na kuanizsha bendi nyingi under his banner, kwa mfano Orch. Lipua Lipua ya Nyiboma & Mbumbi Malanda, Orch. Kamale ya Kizunga & Mulembu, Orch. Kiam ya Muzola Ngunga & Memi, na pia aliweza kufungua recording studio yake ambayo anaimiliki hadi leo na ku-control karibu 75% ya muziki unaotoka Zaire sasa hivi.

  - Pia wapenzi wengi wa muziki mtakumbuka wimbo wake mmoja maarufu sana alioupiga akishirikiana na bendi yake ya Orch. Lipua Lipua ambayo ilikuwa na mpigaji maarufu sana wa Rythm kwa jina la Vata Mombassa Jujuman, wimbo wa "Yanini" ni wimbo ambao ulikuwa unapatikana kwa taabu sana katika masoko ya muziki kutokana na kupendwa sana na hata leo ni wachache sana walionao katika maktaba zao. Pia Verkys aliwahi kupiga kibao cha moto sana kwa kushirkiana na Papa Johnnie Bokelo Isenge RIP, kwa jina la "Engunduka" ambacho kilitungwa na mwanamuziki wa Orch. Veve kwa jina Matalanza.

  - Binafsi ninazo collections za Verkys na bendi zake zote ambazo ninazitunza kama dhahabu, maana ni kiburudisho kikali sana, enzi zile za Boarding School, tunasikiliza Radio Bukavu, ambao ilikuwa inashika saa za usiku tu kwenye zile Radio zetu za shule National 177, I mean longtime ago!

  [​IMG]

  Album ya "Baluti", nafikiri mnaukubuka ule wimbo maarufu sana wa Verkys, akisema

  " Saki baluti lelo babote lingai baboloko ya bana yo tikelangai mama yeyeee, na ndimakite lelo mama na ndimi mamate nyoso salaki ngai na vanda na ndako, motema makasi saki ohh pamelingai, oboswani lelo na mama na ndako ooh! nabeli na mama na yo ooh
  saali papa, ooh sali papa, ohh sumbelinayo lisengo ya mokiri balutiiii"

  Respect.


  FMEs!
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mkuu heshima sana, dada yake Patric Balisidya alikua ni mke wa baba yangu mkubwa yaani kaka wa baba wangu, kwa hiyo ujanani I was very close to him na muziki wake, alipofariki nilipatwa na pigo kubwa sana wakati wa mazishi nilimuahidi kumuenzi as long as I live na ndio hasa motivation yangu kuanzisha hii thread, ninashukuru sana kupata feed back kama yako kwamba tupo pamoja sana, sawa sawa weka vitu tu hapa tuburudishane na kukumbushana tulikotoka wakuuu!

  Respect.


  FMEs!
   
 18. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Pamoja sana mkuu..Ona sasa umemtaja Ptrick umenifanya niikumbuke Afro 70 Band..dah,bendi yangu nyingine hii niliyoipenda..Patrick(R.I.P) alikuwa kichwa hasa mkuu
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  bwana mkubwa fmes,NIMEFURAHI SANA LEO.
  unajua huyo patrick balisidya nyimbo zake nimezipiga sana kipindi fulani.....

  kuna huu wimbo wa KUOLEWA NI JAMBO LA SIFAA...!dah
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Baba Gastone Ilunga wa Ilunga  - Wakulu naamini mnakumbuka kile kibao maarufu cha huyu mzee mashurui sana cha "Kakolele Noel Kritsmas" hasa kule migombani sehemu za Kaskazini mwa Tanzania.

  Respect.


  FMEs!
   
Loading...