Kichuguu,
Ndiyo maana nikauliza kwa sababu moja kubwa sana. Nilikuwa sifahamu/sikumbuki ni mwaka gani hizo nyimbo zimepigwa. Inawezekana kabisa jamaa wakawa wameiga wao kama walichukua baada ya miziki ya Tanzania au hata wote wakawa waliiga kutoka kibendi fulani kidogo sana.
Ule wimbo wa Mayasa vs Byron nilisema ni kile KIPANDE CHA MWANZO tu kama 20 seconds za mwanzo. Kule mbele hazifanani kabisa kabisa.
Wimbo ambao hadi leo nina uhakika Koffi Olomide ali-copy ni huu aliimba Max Bushoke sina uhakika na bendi gani ila anaimba "Kiu ya jibu mamaa, ndiyo inisumbuaayo. Natafuta jibu litakalonirushia? furaha, nimechoka kulala macho na kuota ndoto za alinacha...." Huu pekee nina uhakika kuwa ulipigwa kwanza Tanzania na baadaye Koffi akaja akapiga.
http://www.youtube.com/watch?v=jfoxX7jZwtc&feature=related
(Anzia 0:20. Beats zake ni sawa kabisa na huo wa Chidumule. Labda ni bahati mbaya).
Kwa Koffi Olomide, hii album yenye wimbo huu
(Noblesse Oblige) kwangu inbaki milele kuwa THE BEST OF KOFFI OLOMIDE. Ila kila album kulikuwa na wimbo wa kukata na shoka. Kama Civilise, Coucou, Loi, etc////