Mimi ni shabiki wa Yanga na Juma Ramadhan Mgunda

Lyrics Master

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
470
621
Nimewahi kumuuliza mwandishi na mchambuzi mmoja maarufu, kwanini makocha wengi wa Tanzania hawafundishi soka nje ya nchi, jibu nililopata sikuridhika nalo sana. Alinijibu kuwa ligi yetu imekua sana na ni ligi bora afrika mashariki na kati hivyo makocha wetu wanaona bora wabaki hapahapa nchini kwasababu kuna mpunga mwingi.

Sasa nikaanza kujiuliza hao makocha waliobaki nchini kupiga mpunga mwingi wako wangapi? Nikavuta msimamo wa ligi nikaanza kufuatilia kwenye timu za ligi kuu 16 kuna makocha watano tu wazawa sawa na asilimia 31.25% ya makocha wote, yani hata nusu hawafiki. Kama mzalendo nikasononeka sana. Na nimejaribu kufuatilia kwa nchi za jirani labda nitakuta Kocha mzawa lakini kumbukumbu zikanipeleka kwa kocha Denis Kitambi ambaye mwaka 2018 alikuwa kocha msaidizi pale AFC Leopald pale Kenya chini ya kocha Robert Matano.

Hapo nikahisi kuna shida Mahala either hatuna makocha wenye vigezo au hatuaminiani. Jibu ni hilo la pili. Makocha wenye vyeti tunao ni juzi kati tu hapo TFF ilitoa list ya makocha wenye vyeti vya juu Africa labda pengine kuwa na vyeti na kupata kazi ni vitu viwili tofauti. Kwahiyo hatuaminiani kuna siku nitaelezea hili.

Nimejaribu kufuatilia makocha bora wazawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita pasi kusita jina la Gadiola Mnene wa Tanga, Striker Hodari wa zamani wa Coastal Union, Juma Ramadhani Mgunda ni mmmoja wao, wengine waliokuja haraka haraka ni pamoja na Fred Felix Minziro Katalay Majeshi Baba Isaya, Charles Boniface Mkwasa Selemani Matola na Salum Mayanga.

Kwa muda mrefu kidogo hizi team ‘’kubwa’’ Simba, Yanga na Azam zimekosa Imani na makocha wazawa hasa kwenye mechi za kimataifa. Sasa nahisi ni wakati muafaka wa sisi kama Watanzania kuaminiana. Nasikia Gadiola mnene anapiga deiwaka tu pale Simba na Simba wako kwenye mchakato wa kupata kocha mwingine. Lakini naona sasa ni wakati pekee kwa wanamichezo wote kumpa sapoti anko Mgunda, kocha pekee mzawa kufika fainali za ASFC ndani ya misimu mitatu iliyopita. Kila mtu ni shuhuda ule mpira uliopigwa dhidi ya Yanga kwenye ile fainali.

Mbali na Kenny Mwaisabula ‘’MZAZI’’ ambaye kwa kumbukumbu zangu ni kocha mwa mwisho mzawa (wataalamu watanirekebisha kama nakosea) kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara akiwa na Yanga msimu wa mwaka 2005/2006 anko Mgunda pia ni moja kati ya makocha wenye jicho la kuona wachezaji, kuwaendeleza, kuwajenga hata kuwika, rejea kwa Abdul Sopu, Mtenje Albano, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Ame, Vicent Abubakari, Majimengi, Hance Masoud, Victor Akpan na wengine wengi.

Tazama mechi mbili za kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet kocha Juma Ramadhani Mgunda sio tu ameongeza ubora kwenye team lakini vile vile pia ameongeza hamasa kwenye team na viwango vya baadhi ya wachezaji ambao ilionekana hawako kwenye mipango ya kocha aliyepita.

Huenda ikawa ni mwanzo mzuri kwa makocha wetu kupata deal nje ya nchi. Hii platform inatakiwa Mgunda aitumie ipasavyo, kuna msanii mmoja amewahi kuimba “wafurahishe walio karibu walio mbali watasogea” hivyo basi ni muda sahihi kwa Gadiola Mnene kutufurahisha tulio karibu ili waliombali wapate kusogea na kuulizia kuhusu makocha wazawa.

Najua ipo siku JUMA MGUNDA atafungwa lakini huo uwe muda wa kumpa moyo kuliko kumkatisha tamaa kwamaana kuna mashabiki wa team moja wakifungwa SELE M-baya wakishinda wanakaa kimya. Nawasihi wasirudie kufanya hivyo.

Inauma sana kuona taifa dogo kama Burundi lina makocha wengi ligi kuu ya Tanzania kuliko wazawa. Ni muda sahihi wa kumsapoti JUMA MGUNDA kwa manufaa ya Mpira wetu.



All the best JUMA MGUNDA..



BY LM- shabiki wa Yanga.
 
Waambie utopolo wamchukue minziro au mkwasa wamuondoe nabi ndugu mchambuzi.

Mitano kwanza kwa mgunda.
 
Nimewahi kumuuliza mwandishi na mchambuzi mmoja maarufu, kwanini makocha wengi wa Tanzania hawafundishi soka nje ya nchi, jibu nililopata sikuridhika nalo sana. Alinijibu kuwa ligi yetu imekua sana na ni ligi bora afrika mashariki na kati hivyo makocha wetu wanaona bora wabaki hapahapa nchini kwasababu kuna mpunga mwingi.






All the best JUMA MGUNDA..



BY LM- shabiki wa Yanga.
Usipolewa unakuwa vzr.... tatizo ukilewa daaa!
 
Back
Top Bottom