FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Ndoto ya Philippe Coutinho kucheza Barcelona imetimia. Nyota huyo wa Liverpool amekamilisha uhamisho wake kwenda Camp Nou kwa rekodi ya mchezaji ghali zaidi kuuzwa na ligi ya Uingereza baada ya klabu hizo mbili kuthibitisha kuwa zimeafikiana kufanya biashara baada ya muda mrefu wa tetesi.
Tangu Neymar alipoondoka Barca majira ya joto, Coutinho amekuwa shabaha kuu ya Blaugrana sambamba na Ousmane Dembele. Mmoja alifanikiwa kutua Barca kwa €150m, lakini mwenzake alilazimika kusubiri kwani Liverpool hawakulegeza.

Mazungumzo yaliendelea hadi siku ya mwisho ya kufungwa dirisha lakini Reds walikataa. Miezi michache baadaye mazungumzo yaliendelea na ilionekana kuwa Coutinho angepatikana, na imekuwa ingawa hataweza kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa hadi msimu ujao kwani tayari ameshaiwakilisha Liverpool katika michuano hiyo msimu huu.
Sasa, Je! Atacheza nafasi gani Barcelona? Je! Atatumika kama mshambuliaji kwenye nafasi aliyoiacha Neymar? Atacheza mfumo wa 4-3-3? Au atacheza nafasi ya Andres Iniesta? Au atacheza kwenye safu ya kiungo cha watu wanne kwenye klabu hiyo ya Catalan?

Jawabu linaweza kuwa, "Ndiyo" kwa maswali yote hayo. Bosi wa Barca Ernesto Valverde ametumia mifumo mingi hadi sasa msimu huu, ikiwa ni pamoja na 4-3-3. 4-2-3-1, 3-5-2 na zaidi ya yote 4-4-2, na anaamini Coutinho ni mchezaji anayeweza kucheza katika mifumo yote hiyo.
Ikiwa atapangwa kuziba nafasi ya Neymar kama mshambuliaji wa kushoto, Coutinho ataanza pembeni mwa Luis Suarez na Lionel Messi. MSN yaweza kuwa ilifana zaidi, lakini safu ya mashambulizi itakayomjumuisha Coutinho itakuwa tishio Messi akichezeshwa mbele zaidi na Dembele atacheza kulia, iwe Suarez yupo au hata bila yeye.

Coutinho huwa anacheza upande wa kulia kwa Brazili kumruhusu Neymar kucheza nafasi anayoipenda, lakini mshambuliaji huyo wa Liverpool anapenda kucheza kushoto na bado anaweza kucheza kama mbadala wa nyota huyo aliyetimkia PSG.
Neymar alibainisha mwezi Septemba kuwa Coutinho alikuwa katika kipindi cha huzuni baada ya mpango wake kwenda Barcelona kushindwa kutimia na nyota mwingine wa zamani wa Brazili na Blaugrana, Rivaldo alimbashiria nyota huyo wa Liverpool kung'ara Camp Nou.

Coutinho ni mchezaji mzuri sana na ikiwa atasaini Barcelona atafanikiwa kirahisi sana," alisema gwiji huyo. "Nadhani ni mchezaji mwenye tabia ambayo watu wakienda Barcelona wanafanikiwa. Uchezaji wake unawavutia mashabiki na nadhani utamsaidia kuzoea haraka mazingira. Naamini atafanikiwa."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom