Mashabiki wa barca bwana 😂😂
Mtu anajitapa ka dominate mchezo, kwani wote si tunajua kwamba inter approach yao ni kukuachia mpira wao utawakuta kwenye counter?
Mtu anakwambia Inter wamefunga magoli ya kona hawana lolote, kwani hamuoni kwamba inter hapo wame exploit weakness ya barca kwenye set pieces?
Mbona mifano ipo mingi sana ya timu zenye mpira wa kihuni ambazo zilizitoa timu zilizokua zinacheza soka safi na ku dominate michezo (Mfano mzuri ni chelsea ya kuungaunga 2012 anawatoa prime barca ya kina messi, xavi, iniesta, busquet ambao walikua ni monsters kuliko hii ya sasa).
Sasa nyinyi endeleeni kujitapa mmecheza vizuri wakati jana kazi yenu ilikua ni kuchomoa tu(mlipigwa kamba ya 4 msisahau) wenzenu wanaangalia weakness zenu ndogondogo wanapiga hapohapo, this is knockout stage bro.