Hivi unajua Messi ni zaidi ya mchezaji wa Barça?
Hivi unajua La Liga nzima kwa sasa inabebwa na Messi?
Hivi unajua dunia nzima Inamwangalia Messi?
Yaani upuunzi wa Uongozi kufanya sajili za Kibuuzi mzigo umwangukie Messi
Ubinafsi wa Messi upo wapi? Kuendelea kubaki kwenye team ndo ubinafsi?

Messi anayeongoza kwa Assists unawezaje sema Mbinafsi...
Pamoja na ubovu wa Barça Messi bado yupo kwenye Performance nzuri, unawezaje sema yeye ndo sababu?
Ninadhani tuendelee kuchambua mipira ya bongo ya simba na Yanga..

kwa ninavyomfahamu
Don Clericuzio hawezi kuhoji kiwango cha mtakatifu messi kwa sababu anafahamu fika ya kwamba bado jamaa ana uwezo wa kucheza timu kubwa yeyote licha ya kwamba takwimu zake za kiufungaji zimeshuka sana msimu huu ila bado contributions yake kwenye sekta nyenginezo zimeendelea kuiweka kwenye ramani ya kiushindani klabu ya barcelona.
nadhani hoja yake ya kwanza ipo kwenye ishu ya umri alionao lionel messi pamoja na wachezaji wenzake ambao wamedumu pamoja kwa takribani miaka 10 ya mafanikio, mpaka mchana wa leo kikosi cha kwanza cha barcelona kinaundwa na Pique (33), Alba (31), Busquets (31), Rakitic (32), Vidal (33), Messi (33), Suárez (33) na muongezee Pjanic (30)
kabla ya corona pato la barcelona limekuwa likiongezeka mara kwa mara mpaka wamefikia hatua ya kushika nafasi ya kwanza kwa mujibu wa deloitte (barcelona wanahesabu pato la klabu mpaka kwa dili za mauzo ya wachezaji, pia barcelona inasemekana wanazalisha jezi zao wenyewe) lakini pia deni la barcelona limeendelea kuongezeka na hata cash reserves hairidhishi, yawezekana barcelona wanakusanya revenue kubwa sana lakini operating cost kwa upande wao imekuwa ikiongezekana na sababu kubwa ya kwanza ni wage bill structures inayokula asilimia kubwa sana ya net profit.
hao wachezaji wote saba niliokutajia wanavuta hela ndefu sana kwa mwaka wakiongozwa na huyo
lionel messi ambaye inasemekana pale barcelona anakusanya €1.3m per week, Griezmann €850k per week, Suarez €450k per week, De Jong €300k per week, Busquets €300k per week, Coutinho, Rakitic, Pique, Dembele na Umtiti wanakusanya €250k per week each, Roberto €200k per week, Vidal €180k per week, Alba na Ter Stegen €165k per week na wote hao wana mkataba wa muda mrefu (vyanzo vya taarifa vinatofautiana hivyo basi naruhusu masahihisho)
Njia pekee ya kuondokana na tatizo hilo ni kubana matumizi kwa kufanya overhaul ya kuwaondoa wachezaji ambao upo uwezekano mkubwa wa kuzibwa nafasi zao kwa hali ya soko lilivyo kwa cheap price and salary au kupandisha wachezaji kutoka academy, kinyume chake barcelona watakuwa wanakaribisha hali ngumu ya kifedha ambayo imeshaanza kujionyesha (nakukumbusha kwa mujibu wa raisi wa barcelona msimu huu walichukua mkopo kwa dhumuni la kumsjaili griezmann)
Bartomeu says, as quoted by Samuel Marsden: "Paying Griezmann's €120 million release clause was a complex deal. Barcelona have had to take out a loan of €35m to pay the fee outright."
ukija kwenye sera yao ya usajili wa galacticos nayo pia imekuwa ni kituko kwa miaka hii ya karibuni, unalipaje paundi milioni 100 au zaidi kwa wachezaji watatu ambao huna uhakika wa kuja kufiti kwenye mfumo wa team yenu (dembele, griezmann na coutinho), zipo stori za chini ya kapeti zinadai ya kwamba hata team captain messi amekuwa na nguvu kwenye ishu ya usajili (huu unabaki kuwa ni uvumi uliokosa uthibitisho)