Naomba niseme yafuatayo kutokana na Game ya jana
1. Sijawahi kushuhudia Chelsea wakicheza ktk attention kubwa kama mechi ya jana dhidi ya Barcelona.
Chelsea walijua kuwa uzembe wowote ule ungewagharimu, na ni kweli, uzembe wa beki ulipelekea Messi akafunga, Chelsea waliamini heri matokeo ya kufungwa 2-0 pasipo kufungwa na Messi kuliko matokeo ya 1-1 na 1 lenyewe kufungwa na Messi.
2. Barca tunapaswa kusajili winga ya kushoto, tunapaswa kushoto kuwa na mtu makini wa kazi kama Hazard na sio wauza sura kama Neymar. Hazard jana kacheza mpira mmoja mzuri sana, alitulia na kupiga chenga na kutumia nafasi vizuri.
3. Goal la Chelsea kila mmoja wetu alivyoona Willian kapokea mpira alijua tu kuwa lile ni goli, Willians alionekana mara mbili akiachwa huru anapiga mipira kuelekea golini na zote kagongesha mwamba, mara anapokea mpira tena bila kukabwa anaachwa apige mpka anafunga, huu ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
Solution Wakuu tupate Winga ya kushoto na kiungo mchezashi mmoja wa timu wa kueleweka, hawa akina Paulinho bado sana, walau Rakitic anajitahidi sana.