Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Regia Mtema Kwa Baba na Mama yake wamepoteza mtoto,kwa dada na kaka zake wamepoteza Dada kwa wanafamilia wamepoteza ndugu yao, kwa marafiki zake wamepoteza rafiki kipenzi,kwa chama chake Chadema wamepoteza Mwanachama na Kiongozi wao, kwa wanasiasa wenzie wamepoteza mshirika, kwa Jamii Forum [JF] wamepoteza mpiganaji na kwa Watanzania wamepoteza binti wa Nchi.

Tukipima siku za maisha yetu hapa dunia ni chache sana kwa kuishi, lakini ni nyingi sana kwa binadamu mwenye kumjua Mungu kwa kuwa Mungu ndiye mpangaji wa maisha yetu hivyo ulefu au ufupi ni kudra zake Mungu.Regia ameondoka lakini kaacha jina na jina hilo tafsiri yake inaonekana kwenye michango yetu ya maombolezo yetu humu ndani ya Jamii Forum, kwa kuwa Mungu anasema usitumaini akili zako bali mtumaini yeye Mungu kwa kuwa ndiye anayejua sababu ya uwepo wetu sisi wanadamu hapa duniani.

Mungu alisema anamuumba Mwanadamu kwa mfano wake,hivyo yaliyosemwa na sisi wote kama Wanajamii forum,Viongozi, Wanandugu na Wananchi wote juu ya Mtoto, Dada, Ndugu, Mwanasiasa, Kiongozi, Rafiki, Askari Mpiganaji huyu ni kielelezo tosha cha Mungu kuongea nasi jinsi gani Mungu alikusudia kuwapa Baba na Mama yake Regia mtoto mwema na ambae kwetu Watanzania alikuwa Mwanasiasa na Kiongozi aliyetutumikia kwa muda mfupi lakini, kwa sauti yenye mwangi mkubwa sana ambayo ilisambaa kwenye nyika na kufikisha ujumbe popote pale ilipostahiki.

Regia kaacha jina lake kwenye vinywa vyetu kwa kuwa katimiza kazi aliyotumwa na Mungu kwetu,ndio maana wanafalsa [Philosophers] wanasema kwa Wanasiasa na Viongozi wazuri duniani ubora na uzuri wa uongozi wao si kuacha mali kwa walithi wao,bali kuacha jina ambalo kila mtu akilisikia na kukumbuka anapata mwamko wa kufuata mazuri ambayo mwanasiasa au kiongozi huyo aliyapigania na kusimamia wakati wa wote wa uhai wake hapa duniani.Ndio maana kwa sisi vijana wa dotcom ambao hatukupata kuushuhudia utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini wanadotcom hao wa sasa wanamjua na kumfuata nyayo zake kuliko wale Mwalimu aliowatumika na kuwafundishawakati wote wa maisha yake hapa duniani.

Hakika napata picha ya kibinadamu lakini ambayonatumani nawe ndiyo unayoijenga.Mungu alipomuita kiumbe wake Regia, wakati anaitikia wito wake kufika mbinguni Mungu nae ananena na mmoja wa makarani wake kwa Nchi yetu Tanzania [Baba wa Taifa] Mwalimu Nyerere.Maneno ya Mungu na mmoja wa makarani wake Mwalimu Nyerere,hakika mimi binafsi nayaona ni kama ifuatavyo:
Mungu: Julius
Julius
: Naaaaaaaaam Bwana
Mungu:
Kuna kiumbe wangu anakuja yuko upande wako wa wanasiasa kampokee
Julius:
Ndio Bwana nitatenda ulivyonena Bwana.
Mungu:
Utanena nae
Julius: Ndio Bwana

Mwalimu anaelekea langoni kule wageni wanakoingilia,naam katika tizama yake kutoka kundi la wageni anawaona kwenye mlango wa wanasiasa anashanga kuwa anaona binti,ambae kwa umri huo anamuona kwenye faili ni mjukuu wake.Kibinadamu Mwalimu amini kuwa binti aliye mlangoni mwake ni mgeni wake toka Tanzania hasa upande wa siasa, Mwalimu anaamua kupiga magoti na kunena na Bwana tena ili apate jibu kwa kuwa ajaamini.
Julius:
Bwana Mungu wangu mbona mgeni ulie nena nami,ninae muona mbele yangu ni mjukuu wangu Bwana.
Mungu:
Julius unaniuliza nini tena fuata nilichokuagiza
Julius:
Ndio Bwana

Mwalimu anampokea Regia na kuanza kuelekea nae makazi ya Mwalimu,mazungumzo ya Mwalimu na Regia yanaanza kama ifuatavyo
Regia:
Shikamoo Babu
Julius:
Marahaba ujambo,karibu sana umefika hapa ndio kwenu nyumbani kwa maisha ya milele.
Regia:
Asante Babu, nimepapenda kuzuri sana sijapata kuona mfano wake natamani Watanzania wangepaona.
Julius:
Mshukuru Bwana Mungu aliyekufanya mteule kuja huku.

Baada ya mapumziko na kupumzika,jioni Mwalimu anamazungumzo na mjukuu wake huyo:
Julius: Regia mjukuu wangu ujambo na heri ya safari yako njema na salama,japo najua ugenini uko ulikotoka wanakulilia.
Regia:
Babu Umekosea kule ndio Nyumbani,
Julius:
Aaaaaaaaah mjukuu wangu Regia, kule sio kwenu huku ndio kwenu kule ni ugenini huku ndiko nyumbani kwenu.
Regia:
Kumbe !!!!!!!,natamani hata walioko kule wangekuona kulivyo kuzuri.
Juliis:
Baba na Mama yako, Bibi zako akiwemo Maria Nyerere natumai ni wazima ila najua wanakulilia
Regia:
Wazima Babu.
Julius:
Eeeeeeeeeeh Nchi yenu ikoje manake mimi mwenyewe,nimestuka sana pale Bwana aliponena nami na kuniagiza nikapokee mgeni,lakini wewe katika makarabrasha yangu ya wanasiasa niliowafundisha na kuwaagiza kufuata maadili ya UTU NA KUTENDA HAKI, HASA KWA MASKINI NA WANYONGE nakisha nikawaachia jukumu la kuongoza maisha ya Watanzania na vizazi vyao, viumbe wa Bwana, wewe ulikuwa kichanga tena wakati mimi naaawachia madaraka wao wewe ulikuwa na umri wa miaka mitano.
Regia:
Mmmmmmh Babu kwani wewe ujui!!!!!!!!!.
Julius:
Regia mimi nitajulia wapi mjukuu wangu,kwa kuwa kuna ukuta mkubwa sana kati yangu mimi na watu walioko Duniani,na mwenye funguo za mawasiliano hayo ni Bwana, ambae nyie duniani mnamuita Mungu.Sana sana taarifa ya mwisho kuhusu huko kanipa Babu yako Rashid tena alitoka hapa asubuhi, karibu ataludi.
Regia:
Aaaaaaaaah Kumbe!!!!!!!!. Na mimi nataka kumuona Bwana Mungu.
Julius:
Aahhhhhhaaa Regia Bwana Mungu unae hapa hapa ulipo anakujua, anakusikia anakugusa wewe hata kabla ujafikiliwa utazaliwa na kwenda kuishi ugenini huko duniani na kisha yeye kukuita tena kwake,anakujua wewe tangu alivyokuumba yeye.
Regia:
Babu mbona duniani walinimbia wanaokuja huku wanamuona Bwana Mungu.
Julius:
Ndio hawakukosea unamuona Bwana Mungu yeye ni Alpha na Omega yani mwanzo na mwisho kwa kuwa wewe kuja kwako uku tayari umemuona ndio maana mimi na wewe tumeonana,na tunaongea, kwa kuwa yeye ndie aliyeyafanya haya yote.

Mara mlangoni aningia Sokoine, Mwalimu anamkaribisha ndani,
Sokoine:
Shikamoo Mzee
Julius:
Marahaba Edward karibu,tuna mgeni, kwani nilinena na Bwana akaniagiza nikampokee anaitwa Regia
Regia:
Shikaamo nafurahi kukuona Baba
Sokoine:
Aaaaaaaha Marahaba Regia,karibu sana Nyumbani. Kisha Sokoine anataka kutoka,kumuacha Mwalimu aendelee na maongezi yake na mjukuu wake Regia,Mwalimu anatoa kauli
Julius:
Edward,usitoke ebu,twende hapo kilimani na mgeni huyu manake kaniuliza swali la mwisho hapa wakati wewe unaingia kumuhusu Bwana Mungu,ya kuwa anataka kumuona !!
Sokoine:
Sawa Mzee

Wanatoka na kuelekea kilimani,wakati wakielekea huko Regia anavutiwa na uzuri wa maua na hali ya hewa ya mazingira ya wenyeji wake na sauti nzuri za ndege,wenye rangi nzuri za kuvutia kupita Tausi wa Ikulu, Regia amepapenda sana.Ghafla wanafika kilimani Regia anaona kwa mbali mwanga mkali wa moto na miale mikali ambayo kwa macho yake hakuna athari zozote anazopata ila inatisha kwa kuangalia.Mwalimu anatumia muda huo kumwelimisha Regia kuhusu swali lake la awali.
Julius:
Regia unaona kule?
Regia:
Ndio!!!! Babu Nyerere,mbona kunatisha sana? ,sitamani hata kuangalia, nasikia sauti za vilio na mayowe yasiyoisha pia sauti za kuomba msaaada,si mgeenda kuwasaidia.
Julius:
Regia mama ulichouliza kule tulipokuwa, ya kuwa yuko wapi Bwana Mungu na ungependa kumuona .Jibu langu kwako kwa ufahamu wangu Bwana Mungu yuko Upande huu mimi na wewe tulipo na kule unakosikia wanapiga kelele za kilio cha mayowe ndio kwa shetani na wafuasi wake ambako wana mateso ya milele.Hatima ya uwepo wako hapa ulishaichagua wewe mwenyewe toka ulipokuwa huko ugenini yaani duniani kwa kuwa tiketi ya kusafilia uliyochagua ya ujio wako huku ndio iliyokuchagua wewe kuja huku aliko yeye.Matendo yako na maisha yako duniani ndio yamempendeza Mungu akakuchagua wewe ukaja upande huu wa Bwana Mungu, ulipotamani haki kwa wote ulimpendeza Bwana Mungu wako, ulipotamani kutatua shida za wengi na matendo mengineyo yaliyokusukuma kukufikisha kuwa mwanasiasa wa kujali watu na kuthamini utu wa mwanadamu ndio umempendeza Bwana Mungu wako, kwa kuwa hesabu ya maisha yako anayo yeye toka alivyokuumba wewe kwa mfano wake.
Regia:
Aaahaa Sasa nimeelewa Babu Nyerere,siuniombee ruksa kwa Bwana Mungu niende nikawaambie niliyoyaona huku.Ili wajifunze wasije wakaenda kule kwenye lile bonde linalowaka kwa kunakoitwa kwa Shetani na wafuasi wake.
Julius: Aaaaaaah Regia unanichekesha kweli mjukuu wangu!! Kwani wewe nani alikwambia?Wewe umetimiza kusudio la Bwana kwa wanadamu. Na Bwana kawaachia uamuzi wao wenyewe kuchagua kama wewe uklivyomaliza uchaguzi wako.Umetimiza nao waache watimize wajibu wao kwa Bwana kwa kuwa aliwaaumba kwa mfano wake ambao ni mimi, wewe na baba yako Sokoine hapa tulio tulishatimiza huko ugenini.Na kwa kuwa wakati nilipokuwa nimetumwa na Bwana Mungu huko ugenini nikawa Rais wao wa kwanza wa Taifa lao niliwaachia mwongozo kwa kuunda na kulinda Taifa lenye kusamini UTU WA MTU, HAKI SAWA KWAO WOTE NA KUTHAMINI WANYAONGE WASIO NA SAUTI.Na wewe Regia pia umetimiza wajibu wako hivyo hawana wa kumlalamikia cha msingi umewaachia jina lako.
Regia:
Jamani Babu Nyerere jaribu kuongea nae hata sekunde chache tu kisha narudi.
Julius:
Polepole utanielewa najua unawapenda sana kwa kuwa nilipotumwa mimi kuja huko nilichotumwa nilifundisha na Wananchi walio wengi walinielewa, watu wa aina yako ndio wanakazi ya kusimamia mafundisho hayo ya utu na haki, lakini kama ni kuwafundisha na kuwakumbusha kuhusu kumtumikia Bwana Mungu siku zao za maisha yao duniani basi Makanisa, Misikiti na Imani zote zinazojua Mungu mmoja zipo wanazo tele zinawakumbusha kila siku. Kwenye hayo Makanisa ,Misikiti, Madhehebu na Jadi zao wana Maaskofu,Mapadre,Wachungaji,Masheikh na Wazee wao wa Jadi.Kwa kuwa Bwana Mungu aliwapenda ndio maana akawatumia mkombozi Yesu kristu kwa ajili yao kwa wale walio wakristu na kwa Waislamu alimtuma Mtume Muhamad kwa ajili ya mafundisho ya kiimani,kuwajenga kumtumikia Mungu katika sura ya uwanadamu.Na nyie Wanasiasa wajibu wenu kusimamia na kuongoza ustawi wa jamii katika misingi ya haki na utu kwa kuwa Bwana Mungu awezi kushusha Malaika kuja kuwaongoza na kuonyesha jinsi ya kuishi bali Mungu kwa kutumia wanadamu anatoa baraka za binadamu kujiongoza na kuendesha maisha yao.

Rose Muhando kwenye mmoja ya wimbo wake anasema Regia hayumo katika miongoni mwa wajutao,hayumo miongoni mwa wenye mashaka, hayumo miongoni mwa wasitao, amemtumaini yeye Bwana Mungu kwa sasa yuko kwa Mungu ana nguvu tele.RIP Regia.
 
Nimelia sana, jana mchana na nimeshindwa hata kuandika makala kwa wasomaji wangu wa magazeti. Kijana aliyetutoka alikuwa kiongozi wa mabadiliko ya kweli katika Chama chetu.

Ni pigo kweli kwa watanzania lakini kwa wanaCHADEMA tumepoteza zaidi. Alivyo Regia Mtema kwa sasa ndivyo tutakavyokuwa na sisi siku moja, na tulivyo sisi kwa sasa na yeye alikuwa jinsi tulivyo.

Cha Msingi tuzidi kumwombea. Raha ya Milele umpe ee bwana, na Mwanga wa milele umwangazie-Apumzike kwa amani. Amina
 
Deo Filikunjombe
It's, with deep sorrow and tears today, I've received the untimely death of our fellow, MP and fighter - Regia Estelatus Mtema who was a special seats MP (chadema) for Kilombero.

Regia was a Ludewan, by default, as she grew up and went to Lufumbu and Madilu Primary Schools - both schools in Ludewa - that time, Regia's mother worked in Ludewa District, as a teacher.

Hata alipopata ajali ya ule mguu wake, marehemu Regia alipata matibabu katika hospitali ya mission ya Lugarawa. Tutakukumbuka daima na milele, mpiganaji wetu, Regia.


Gone too soon, R.I.P.

Mnyika
CHADEMA inatoa pole kwa familia ya marehemu Regia Mtema, wanachama wote na wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Jimbo la Kilombero kutokana na msiba huu wa ghafla katika wakati ambapo mchango wake ukihitajika kwa chama na kwa taifa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za maziko, itatolewa mara baada ya kukamilisha majadiliano baina ya familia ya marehemu, chama na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mipango ya mazishi ya marehemu inapangwa nyumbani kwa Baba wa Marehemu Regia Mtema, Ndugu Estelatus Mtema, Tabata Chang'ombe. Ratiba ya maziko itatolewa baada ya kukamilika kwa taratibu zinazopangwa na familia ya marehemu, Ofisi ya Bunge na chama.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Regia Mtema, mahali pema peponi. Amina.
 
Nilikuwa bado sijui kama hayati Regina Mtema alipata ulemavu kutokana na ajali, nilikuwa nafikiria kama ilikuwa ni ulemavu wa kuzaliwa.

Mungu amjalie tulizo na faraja pekee baada ya kumaliza safari yake ndefu ingawa wengi wetu tunaona kama imekuwa fupi.

Mungu ameona alichokifanya kwa sasa utume wake umekamilika na anastahili pumziko la amani milele akiwa nyumbani kwa baba wa milele. Amen.
 
The more i open JF kuanzia jana the more i feel sad kwa huyu dada kutangulia

We are born to Die
 
Hamna jinsi ya kueleza weledi na wasifu wa Regia jamani, sitaki hata kuamini kama kweli hatunaye.
She was real people centred.
 
Tunajua kwamba siku hiyo ikifika, tutarudi mavumbini tulikotoka!! Ingawa huu ndo uhalisia wenyewe lakini bado natamani ingekuwa ni ndoto ambayo ingekwisha baada ya kutoka usingizini na kunipa nafasi ya kuendelea kumuona dada Regia akiwa bado yu nasi!!

Mpaka hapa nimeshaumia vya kutosha kwa sababu najua hatuwezi kuubadili ukweli zaidi ya kuupokea kama ulivyo! Ujasiri wake katika harakati za kuleta mabadiliko pamoja na kiu ya haki alokuwa nayo ni vitu ambavyo sitavisahau kwake kwani kila ninapovifikiria ndio nazidi kuumia zaidi!

PUMZIKA KWA AMANI DADA, PUMZIKA KWA AMANI MPENDWA....PUMZIKA KWA AMANI YA BWANA NA MWENYEZI MUNGU AKUANGAZIE MWANGA WA MILELE.....AMINA!
 
Hakika JF si "virtual life"! Ni ukweli hasa kwa sababu tunaongea mambo yanayo-tutatiza na kutugusa kila siku. Regia sikumfaham popote zaidi ya humu JF.

Hata hivyo nilijua kuwa huyu alikuwa ni mwanamke "independent" na mwenye uthubutu hasa! Haya yote niliyajua kupitia humu JF na niliposikia kuwa kuna mbunge wa viti maalum wa Chadema amefariki nilikimbilia humu. Kumbe ni Regia!!! aaaah, too bad.

Ni mbunge pekee aliyeitumia JF sana tu na kuwasiliana na watu hapa. Kwa ukweli pamoja na kuwa JF ni online tu, na hapa wengi tukitumia majina yasiyo halisi, lakini maisha yetu ni halisi. Tunachokiandika wengi ni halisi na kinawakilisha maoni na mitazamo yetu ya ndani kabisa. Regia alikuwa wazi sana hapa JF!

Bila shaka JF inatuuunganisha kuliko vile tunavyofikiria na kuamini. Najisikia kama huyu ni mtu niliyekuwa namfaham na kufaham alichokuwa akisimamia na kukipigania, naam haki na usawa kwa watanzania. JF ilimfungua kwetu, naye alijifungua kupitia JF.

Sikuwahi kumuona kwa macho, ila picha yake hasa ile aliyoitumia pale alipoamua kutumia jina lake halisi humu, inaacha lasting memory akilini mwangu. Life online is REAL than we believe. Regia has taught me this!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
tunamshukuru mungu kwa hili pia maana maandiko yanatuambia tushukuru kwa kila jambo hata liwe linauma kiasi gani, tulimpenda sana dada yetu regia lakini mungu amempenda zaidi amekamilisha kazi yake anatakiwa kupokea taji, tutamkumbuka sana hasa kwa mchango wake na jitihada za kuwatetea walemavu though yeye hakuwa mlemavu wa kuzaliwa, poleni sana chadema kwa kupoteza mpiganaji ila na imani tutapata mwingine maan awapiganaji tunao wengi sana. REST IN PEACE REGIA MTEMA.
 
Kwa kweli wote tufuata njia aliyoipita MH. R. Mtema! Mungu ailaze roho ya marehemu mpendwa wetu Regia Mtema mahali pema peponi! Amen!
 
Ukisikia bahati mbaya kwa Watanzania basi ni kuondokewa na binti,kiongozi na
Mbunge huyu. Tangulia Regia, kaungane na Mwl. Nyerere kutuombea. Mwambie Nchi imezingirwa na mafisadi. Tumezidiwa. Tuombeeni kwa Mungu.
 
Ni masikitiko makubwa kwangu na kwa taifa kupoteza kijana mahili na mpambanaji aliyekuwa anasimamia anachokiamini, mungu ailaze roho ya dada regia mahali pema peponi- amen
 
Its unbelivable but already happen, may her soul rest in eternal life amen
 
ningeomba condolences zisitishwe,the more they post the sadder i become(pardon my english)
 
Wana JF,

Wakati wa uhai wake ndugu yetu Mh Regia (RIP) aliwahi kuonyesha uchungu wake juu ya watoto wenye ulemavu wa mwili wanaokosa fursa ya kupata elimu. Napendekeza tumuenzi kwa kuanzisha REGIA MTEMA MEMORIAL FUND ili iweze kusomesha watoto wenye ulemavu kwa utaratibu utakaokubaliwa.

Naomba kutoa hoja.
 
Back
Top Bottom