Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Jamani jamani,why had she to go when we need her so much, aaaaa machozi machozi machozi
 
Kazi ya Mungu haina makosa.Regia sijui niseme nini.Mara ya mwisho kupata mshtuko kama huu ilikuwa ni tarehe 18.5.2007.Siku hii ndipo alifariki mama yangu.Hakika msiba wa Regia Mtema umenitikisa kama nilivyotikisika alipofariki mama yangu.Niseme nini basi! Maneno yameniishia na machozi yananilengalenga. Oh Mungu wangu.Pumzika kwa amani Regia.Tutakutana Paradiso siku hiyo!
 
Pumzika kwa amani mpendwa. Kazi uliyokuwa ukiifanya kwa watanzania, hali ya nchi uliyokuwa ukitamani tutaitimiza.
Tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi.
Tuonane siku ile Paradiso.
 
KWAHERI DADA REGIA
Umma wa Watanzania Tumepata mshituko
Wa kuwa Dada Regia Pamoja nasi hayuko
Tunalia na kulia Simanzi na sisimko
Ghafla bila mwaliko Umetutoka Regia

Watanzania wenzako Regia twakulilia
Wanafamilia yako Msiba umewachia
JF nyumbani pako Napo umetukimbia
Wengi tunakulilia Watanzani wenzako

Umetutoka Regia Bali tuko nyuma yako
Ni kazi yake Jalia Yametimu Maandiko
Kuwa hapa twapitia Mbinguni ndio mashiko
Tutakuwa nawe huko Siku saa kitimia

Katu huko peke yako Nasi tutakufatia
Ingawa sasa hauko Mpendwa wetu Regia
Busara, matendo yako Yote ulopigania
Tutayafuatilia Tuliopo nyuma yako

Yote ulioanzia Kwenye mikakati yako
Yale yaliyotimia Twakupa hongera zako
Mengine yalosalia Tutafanya wenzako
Kukidhi dhamira yako Hadi yatapotimia

Tunojivunia kwako Wema na zako tabia
Moyo na juhudi zako Wanyonge kusimamia
Ari ujasiri wako Daima twajivunia
Hukupenda kutulia Kututetea wenzako

Yamenisha maandiko Namaliza nikilia
Nalilia watu wako Pengo ulotuwachia
Wana JF wenzako Regia twakulilia
Tuli twakuhitajia Regia leo haupo

Kaditamati natia Kwa kumwomba Mola wako
Akusafishie njia Pepo iwe Nyumba yako
Mola atakujalia Kurehemu roho yako
Kwaheri tu nyuma yako Kwaheri wetu Regia

MAMMAMIA
 
The more i open JF kuanzia jana the more i feel sad kwa huyu dada kutangulia

We are born to Die
MTM,

Mkuu wangu,kweli hali hii inaumiza sana....post yangu imenikumbusha siku ile tulipokuja nae kuwaona wewe pamoja na wakuu wengine wa JF,mkitoa nasaha kwetu wanasiasa .Ulipobadili ID ya hapa JF nikawa confused hadi nimemuuliza Mwanajamii0ne......
 
SIRI ZA MUUMBA HAKUNA AWEZAYE KUTEGUA KITENDAWILI, MPIGANAJI AMEONDOLEWA KATIKATI YA MAPAMBANO,
"...Oooh God, It was not Fair for Tanzanians.....we respect your will...Please Almighty GOD, May you rise another stronger activist especially for now when the future of our Country is Questionable..."
 
Wanasema mwanamume huwa hali,

Lakini kwa hili la Regia machozi yanatoka tu sijui kwanini!

Ni matumaini yetu kuwa amelala kwa utulivu huko aliko.
 
Maneno yamenipotea. Kwa ufupi, sikuwahi kukutana naye ana kwa ana lakini nilipomuona siku ya kwanza akichangia hoja bungeni nilijua thamani yake. Hata nilipoomba awe rafiki yangu fb haikuchukua muda alikubali. Tangu wakati huo tumekuwa na mawasiliano kwa njia ya mtandao yaliyoniweka karibu naye kiasi cha kujihisi tumeshawahi kuonana.

Kifo chake kimenistua na kunisikitisha. Mungu aliyeruhusu hili litokee na atufariji na kututia nguvu sote! RIP Regia Estelatus Mtema.
 
Nakosa cha kuandika kwa kweli, Kamanda is gone.
May God rest ur soul in peace. Kamanda,mwanahakati,mtetezi wa wanyonge Regia E Mtema.
 
And now you hear my songs the radio is playin'
Oh I can't believe my ears
And what everybody's sayin'

And boy I'll tell you
Folks don't know the half
I would give it all up
Just to take one ride

(With you)
How we used to chat on JF siasa page
(With you)
And how we used to argue on different matters
(With you)
And all the little basement party joints we'd do
Now I'm just missing you
How I wish

I wish that I could hold you now
I wish that I could touch you now
I wish that I could talk to you
Be with you somehow
I know you're in a better place
Even though I can't see your face

I know you're smiling down on me
Saying everything's okay
And if I make it out this thug life
I'll see you again someday

I wish, I wish, I wish
I wish, I wish, I wish

............
............
Your family called the morning of the tragic end
Damn, my condolensces

(Modified lyrics from R. Kelly's song I wish)

RIP Regia.
 
Ninazidi kulia nikimkumbuka Regia.Wema wake,Ucheshi wake,Uchangamfu wake,Upiganaji wake na kila kitu.Mungu wangu nitaendelea machozi na huzuni vikipungua.RIP Kamanda na Jemadari wangu.
 
Regia umeishi muda mfupi sana lakini umetoa mchango mkubwa sana kwa nchi yako ya Tanzania, wapo walioishi muda mrefu sana na bado wanaishi wakiwa wameihujumu na kuibaka Tanzania bila huruma, hivi ndivyo asili(nature) ilivyo. La msingi ni kwamba mchango wako kwa taifa utakumbukwa daima.
 
Sina cha kusema, maneno yamenikauka. Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi, tulikuwa bado tunakuhitaji bt Mungu ameona ni vema upumzike. We will miss you Regia. Pumzika kwa amani dada!!
 
..........We will always miss you Regia!! Gone too soon! You were such a strong woman, I admire everythings you achieved. What an amazing woman she was!!...........Ohhh God, that hurts so much!!

I know you're looking down on all of us right now, from your place in heaven. R.I.P Regia Mtema.
 
Back
Top Bottom