Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

kWELI taa ya mshumaa hata kama itawaka kwa ukali mkubwa...itakuja wakati itazimika, vivyo hivyo, uhai wa mwanadamu huweza kuisha mara moja tuuu....na sio zaidi.

Dada Regia Mtema, kweli wewe ulikuwa jasiri na mpiganaji wa kweli na dhati, tulipenda uendelee kupigana kwaajili yetu watanzania, lakini umauti wako umekuwa ni waghafla sana, hakuna aliyejua na kuelewa kuwa safari yako ya kuishi duniani ilikuwa ni leo..!!!! Mungu wa AMANI NA UPENDO akupokee na kukupa pumziko la milele ukiwa na malaika wa amani.

eeh.Bwana....raha ya milele umjalie eee...Bwana, na Roho ya Regia Mtema uilaze mahali pema peponi...Amin.

Kwa Maana "imeandikwa kuwa binadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi sio nyingi, na kwa kuwa tuliumbwa kwa udongo na mavumbini tutarudi milele na milele.....Amin"

Kila kiumbe na akiri moyoni mwake kuwa Bwana ni mwema...."
Wanadamu tukumbuke kujiandaa kwa safari ya kwenda mbinguni...maana hatujui saa wala siku ya kiyama...tusitende yasiyompendeza Mungu...bali tutenda mema kwa utukufu wake.
 
There are no exact words at this point of time to explain her death, BUt i can just wish her to rest in peace.
 
Mungu kwanini umeliruhusu hili litokee?? kwa nini BABA? kwa nini tusononeshw kiasihiki??...dada yangu umemwita leo katika makazi ya milele....Naomba baba umpemwanga wa milele umuangazie...na raha ya milele nakusihi baba umpe....

dada yangu alishiriki kifo cha krstu kwa ubatizo basi baba nakuomba ashirikipia na ufufuko wake...siku hiyo Mwili wake utakuwa kama Mwili wakoMtakatifu.....
dada yangu umeeenda...nenda dada yangu na pumzika salama......kwa kuwa Munguamekupenda zaidi mimi sina jinsi isipokuwa kukuombea zaid........

 
Dada Regia, May Almighty God Rest Your Soul In Eternal Peace.

Regia was one of a kind and Tanzania is at a loss.
 
Pumziko la Milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele,Marehemu Regia Mtema apumzike kwa amani,Ameen.
 
Regia ni mshumaa uliokuwa umeaanza kuwaka na kuangaza ndani ya nyumba ghafla ukazimika.Ni mengi mazuri aliloyaasisi na kuyasimamia. Hivyo ni jukumu letu kuyaenzi na kuyasimamia pia.
 
Kweli wema hawana maisha, Rest In Peace Reggia wote tuko nyuma yako. Sitakosa kukukumbuka kila ninavyofungua Jamii Forums


 
Last edited by a moderator:
Im still dumbfounded........................

Regia,we weren't prepared for you to go
You were too full of life to be
Taken away from us so soon
It's still hard to believe that you are no more!

How much we'll miss you

And your commitment to our country

Your absence leaves a hole in us
We're filling with our tears

R.I.P Regia.....Adios!
 
Nilikuwa nimepotea JF lakini leo nimefungua na kukuta RIP Regia...sikuamini nini nasoma...Mungu iweke roho ya Mpendwa wetu Regia Mtema.....Tutakukumbuka sana hapa JF kwa michango yako yote....

RIP Our Beloved Regia Mtema.
 
Rest in Peace Regia Mtema. This forum has made you someone I know. I'm mourning with your closest. Am crying for you. I now know what you said" JF imekua nyumbani na darasa kwangu" rest in peace great thinker and thanks for all and each contribution and coment you Made to our Home JAMIIFORUMS
 
It has been too long since am lost without, so wat am gona, since av bin nidin u and wantin u? R.I.P
 
Japokuwa sijawahi kuonana na Regia ana kwa ana au hata kuongea naye, lakini nimemfahamu mpiganaji huyu kupitia magazeti. Na hasa ilikuwa wakati wa kampeni za uchaguzi na baada ya hapo hapahapa JF. Rest in Peace Regia, japokuwa umeondoka haraka kuliko tulivyotarajia.
 
Ni vigumu kuamini japo imetokea.Namkumbuka Regia kwa mambo matatu ya msingi kwangu na kumwona ni mwana siasa komavu.

Moja ya mambo yanayonikumbusha juu ya Regia,alipohudhuria ufunguzi wa tawi la chadema Udom akiambata na mlezi wa tawi Mh.Lema na wabunge wengine.Marehemu aliwafurahisha wanafunzi na wanakijiji kwa kutaja koo(clans)saba za ndani ya CCM.

Namkumbuka Regia pia alipokua anauliza swali la papo kwa hapo kwa Mh.Pinda bungeni juu ya serikali kufuatilia mavmizi ya fedha ya mbunge yanayotolewa na serikali kuona kama yanatumika ipasavyo ama la.Pinda alimjibu kama endapo mbunge yeyote atakwenda kinyume cha matuzi sahihi atakua anajihukumu mwenyewe kwa wapiga kura wake.

Tatu,namkumbuka Mh.Regia nilipokutana nae pale Ifakara na kuonge nae nyumbani kwake kipindi cha mwezi wa 9 mwaka jana na kubadilishana namba za simu na aliniomba kushiriki uchaguzi wa Igunga kuongeza nguvu.

Ama kwa hakika mama yule alikua mtu wa watu kamwe hakua mwenye dharau.
Mungu aipokee roho ya marehemu mahali pema peponi.

Amina.
 
raha ya milele imwangazie na apumzike kwa amani. amina. kidogo marehemu alikuwa anagusia gusia courage ya mama margareth thatcher. Hivyo tanzania tumempoteza dada yetu Iron lady mtarajiwa. kifo kinauma sana hiki!
 
Poleni sana wafiwa
Poleni sana wana CHADEMA
Poleni sana wakazi wa Kilombero
Poleni sana wana Jamii Forum wenzagu

Kwa heri Dada REGIA MTEMA
 
Back
Top Bottom