MM umenena yote,kwa kweli tumepoteza mtu makini sana,hasa hapa JF..hoja zake nzito zenye kuhitaji kusugua kichwa na kufikiria kwa dhati kabla ya kuchangia tutazikosa,tutazikosa comments zake,tutamkosa pale bungeni wakati wa kuchangia hoja kwa maendeleo ya nchi yetu...tutamkosa Regia! Ni jambo lisilovumilika kirahisi,nitamkosa Dada Regia,nitamkosa mum Regia!! Nani wa kutuzibia hili pengo,tutampata wapi mtu mvumilivu na makini kama Regia jamani? Tutayapata wapi mawazo yake chanya ya kujenga chama chetu wakuu? Regia hayupo jamani,nani? nani? nani? oh!! mum Regia mbona umetuacha wenzio,hapana naumia wakuu!!