Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 14, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hii ni kwa ajili ya tributes za Regia; kama unalo zuri la kusema kumhusu yeye au kumbukumbu yako njema tushirikishe.  Nyota Imezimika  Ni pigo limetufika
  Nashindwa la kutamka
  Ilikuwa inawaka
  Sasa nyota yazimika
  Nabaki natetemeka
  Machozi yanadondoka!
  Namlilia Regia, ni nyota imezimika!

  Mwanga ametuachia
  Mbele ametangulia
  Kaitwa kaitikia
  Japo tulitamania
  Aishi kitambo pia
  Tuijenge Tanzania
  Namlilia Regia, ni nyota imezimika!

  Ee Mola nakuabudia
  Utukufu nakurudishia
  Kwa maisha ya Regia
  Jinsi ulimtumia
  Tupe na nguvu Jalia
  Mfanowe kufuatia
  Namlilia Regia, ni nyota imezimika!

  Nashindwa kuendelea
  Majonzi yamelemea
  Pema ninamuombea
  Rafiki nilimzoea
  Mwanga utaendelea
  Mapambano yanaendelea
  Namlilia Regia, ni nyota imezimika!​

  Nimepokea kwa masikitiko makubwa, kutokuamini na mshtuko taarifa za msiba wa Mhe. Regia Mtema. Kifo chake kimekuja wakati ambapo moto wa mabadiliko nchini umekuwa ukipamba kwa kasi zaidi na nyota yake ikizidi kuangaza kila kukicha. Regia alikuwa ni mmoja wa vijana ambao wametupa matumaini kuwa kuna vitu vinawezekana nchini na vinaweza kufanywa na vijana.

  Msimamo wake, uthabiti wake na kujiamini vilikuwa ni tunu ambazo zilimsimamisha bila woga kutetea kila alichoamini. Kwa baadhi yetu ambao tumepata nafasi ya kuzungumza naye nje ya mitandao hii na wale ambao tumemjua kwa muda mrefu kabla ya kuibuka na kuwa mwanasiasa tunaweza kusema kuwa Regia alikuwa ni mwanasiasa aliyesukumwa sana na moto wa mabadiliko. Moto ambao alitamani kuwa sehemu yake katika kuona cheche zake zinawafikia wengi zaidi.

  Alitamani kuiona Tanzania ikiwa bora zaidi na ambayo watu wake wanafurahia matunda ya nchi yao kwa haki, usawa na umoja. Tunaposema alikuwa ni mwanaharakati hatutii chumvi. Wengi tumeshuhudia jinsi ambavyo amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa ambao wamekomazwa kwenye mitandao hii. Amekuwa jasiri kuliko wanasiasa wengi wakongwe kuja na kupitishwa kwenye tanuru la maoni ya JF na kila wakati ambapo ulifikiria kuwa labda amekwazika na hatorudi tena Regia alirudi na alirudi akiwa mpya kabisa. Aliweza kusimama katika moto bila kuungua na kama aliungua haikuwa rahisi kujua!

  Kwa upande wangu, Regia alikuwa ni mshiriki mkubwa wa mambo mengi ambayo nimeyafanya na yeye ameyafanya. Aliponiomba wakati wa kampeni ya 2010 kumsaidia kupitia Ilani yake kwa Wana Kilombero niliona ni heshima ya pekee. Mapema mwaka huu tulikuwa tumeanza kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo tungeweza kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na wengine katika Bunge lijalo. Bahati mbaya mbingu imebadili mipango hiyo. Ninaamini hata hivyo huko aliko anatutie shime ya kuendelea kutekeleza mipango mbalimbali.

  Regia alikuwa mchangamfu, mcheshi, mwenye kupenda utani, na kwa hakika kabisa alikuwa makini. Kitu kimoja ni kuwa hakuogopa kusema alichokuwa anafikiria au kilichomgusa moyoni. Alisema hisia zake na na mawazo yake pasi ya kutaka kuonesha kumwogopa mtu au kumpendelea mtu. Aliamini katika kutetea msimamo wake na akishawishiwa kuona mapungufu hakuchelewa kujirudi. Kwa kweli haikuwa rahisi kuzungumza naye bila kujikuta unatabasamu. Alikuwa amejaliwa kipaji cha kujenga urafiki na watu wengi na hata kuwa kwake Mbunge hakukuwa kwake kiuzizi cha kuwa karibu na marafiki zake. Hakujiona ni "kigogo" wa aina fulani aliyependa kutukuzwa au kuogopwa. Alijiona yeye ni mwanasiasa na kweli alikuwa hivyo. Lakini alikuwa ni zaidi ya mwanasiasa - alikuwa ni binti wa Kitanzania aliyejaliwa vipaji vingi na mwenye njozi nyingi kwa nchi yake!

  Rambirambi zangu nyingi - na labda nawasemea wengine vile vile - ziwaendee familia yake ya Mzee Estelatus Mtema pamoja na tena kwa namna ya pekee kwa pacha wake Remija Mtema. Remija kuliko mtu mwingine yeyote duniani amepoteza sehemu yake na mzigo huu ni mkubwa kupita kiasi. Wakati kwa wengi wetu tumepoteza rafiki, mwanaharakati, mwanasiasa na mshirika wa mabadiliko kwa ndugu zetu hawa wamepoteza binti, dada, shangazi na ndugu yao wa karibu. Ni msiba mkubwa kwao. Nawaombea faraja wote hawa na wale wote ambao wameguswa na msiba huu mkubwa.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu Regia pema peponi na atujalie sisi wengine dhamira na kiu ya kuendeleza na kusimamia kile ambacho dada yetu alikisimamia na kukipigania. Namna sahihi ya kuenzi maisha ya Regia ni kuendelea kuipigania Tanzania na Watanzania bila kujali jambo jingine lolote linalowatofautisha kama mtu mmoja mmoja.

  Hata kama nyota imezimika, mwanga tulioushuhudia unatupa matumaini kuwa zipo siku njema mbeleni!

  Mpaka Tuonane tena Paradiso!

  MMM
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama watu wakifa hua wanaona waliobaki huku wanareact vipi kwa kuondoka kwao basi atakua anatabasamu sasa hivi huku machozi yakimtoka.

  RIP RM.
   
 3. H

  Haruna Batenga Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuchukua nafasi hii nikiwa mjumbe wa H/kuu ya CCM wilaya ya ilala kuwapa pole Viongozi,wanachama na wapenzi wa Chadema kwa msiba wa Mbunge wao wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe R.Mtema,Mwenyezi mungu awpe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  asante kwa niaba ya Wana Chadema woote ila kwa kukurekebisha tu sera za CHADEMA zinasema kwenye mambo yenye maslahi ya Taifa siku zote hamna utani kwa hiyo usirudie kutuita Watani!
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Yaani ni kama ndoto BJ......Regia pamoja na kupata ubunge hakuitenga/kuiacha JF......Daima alikuwa nasi katika shida na raha na alijitahidi kuutumia muda mchache anaoupata kuja humu kutujuza mambo mbalimbali yanayojiri bungeni na katika medani za siasa kwa ujumla......She was born for JF na JF tutamlilia daima....

  Yeye ni tofauti sana na wanasiasa wengine ambao waliitumia JF kama daraja la mafanikio yao kisiasa na mara baada ya kufanikiwa kisiasa wanaacha kabisa kuingia JF,Regiia/GS hakuwa hivyo........Yeye daima tulikuwa nae JF,hakuchagua jukwaa....Jukwaa la siasa utamkuta,MMU kama kawa, kule kwetu kwenye Michezo na Burudani kulikuwa kwake pia.....Chit Chat ndo usiseme, yaani alikuwa anaingia kila jukwaa tofauti na wanasiasa wengine ambao wao kila siku ni SIASA tuuuu.....

  Kwangu mimi Regia alikuwa zaidi ya ndugu,sikujuana na Regia tangu utotoni wala sehemu yoyote nyingine, nimekutana nae JF na tangu tumefahamiana nae tumekuwa zaidi ya ndugu.......Kwa hakika hili ni pigo,sisi tumempenda lakini Mungu amempenda zaidi....

  Upumzike kwa amani dada yangu mpendwa Regia...

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Amen.

  Kwa niaba ya wanachadema, tunashukuru kwa kuguswa na kujali kwakuwa pamoja na utofauti wa itikadi za kisiasa lakini mwisho wa siku sote ni waTanzania.
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sisi si watani wa magamba,any way concern yako imepokelewa
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata mimi nimeshangaa! Tatizo lililo nje ya uwezo au mamlaka ya kibinadamu kama misiba linapotokea, pole kutoka kokote kule haikataliwi. Lakini kwamba CHADEMA na Magamba ni "watani" sikuwahi hata mara moja kufikiria - hii kwangu ni habari mpya na ya "ajabu". Yaani imenishangaza sawa sawa na msiba wa Mh. Regia ulivyoniduwaza!
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  tunashukuru kwa kuungana nasi kwenye maombokezo ya mpendwa wetu, jembe letu, shujaa wetu REGIA MTEMA. ila hatuko kwenye utani hapa na wala chadema si watani wenu, badili heading haraka au uondoe hii thread, KUWA NA HAYA WEWE SI ULETE MAMBO YA AJABU KWENYE MAJONZI
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,536
  Trophy Points: 280
  ...Pamoja na nia yako nzuri lakini hakuna swala la utani katika kutetea maslahi ya nchi. Natumai MODS watarekebisha kichwa cha bandiko lako.
   
 11. L

  Luiz JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa salam za rambramb, ila utan na nyie hatuna huwa tunawapnga kwelkweli so sisi sio watan wenu, watan wenu ni Cuf
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Asante kwa niaba ya wana CDM ingawaje havipoi aisee! Inauma mno! Daaah!


  RIP Regia, tulikupenda lakini Mungu kakupenda zaidi.
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  R.I.P. Mpiganaji wetu!
  Aluta continua!
   
 14. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  will miss you Regia!
   
 15. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  Tutakukumbuka daima Regia...hadi hapo tutakapokutana tena.......
  Ulale kwa amani mpendwa......
   
 16. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  Ameenda mpiganaji, Mungu amemwita angali tunamuhitaji. May God rest her soul in peace.

  Shocking news indeed :(
   
 17. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Too young to go!
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Regia ...
  alikuwa mbuge wa watu
  mheshimiwa lakini very humble
  alikuwa mtu wa kila mtu....

  licha ya kuwa mlemavu
  hakujiweka nyuma wala kuogopa kujitokeza
  alipigana kwa ajili yake na wengine
  na zaidi alikuwa yuko tayari kujifunza kila siku
  vingozi wengi wanapaswa kuiga mengi kutoka kwake
   
 19. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  aaah, basi tena................ Mungu akisema "njoo" nani ataweza kukataa???.......................

  RIP Regia Mtema (Gender Sensitive) ......................... ukiulizwa huko nani akupendaye ulioyemuacha duniani.................. sema .................. kwa sauti kubwa..................... Akili Kichwani....................... bye bye bye byeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee...................... aaaghr......................... dunia hii???!!....................... kweli tunapita jamani.......................
   
 20. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #20
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Toka moyoni mwangu Nasikitika sana,

  Rest in Peace beloved Regia.:shock:
   
Loading...