NEWSINKP

Member
Sep 26, 2016
77
92
Watanzania wenzangu na viongozi wa Nchi hii, hebu tufanye tafakari ya kina juu ya sheria ya mifuko ya jamii na kauli za viongozi Wetu juu ya ajira nchini.

Nitoe nadharia ili kila mmoja Wetu asome atumie kama base ya tafakuri.

''Mwezi uliopita kuna taasisi moja hapa nchini ilipunguza wafanyakazi takribani 25 sababu ikiwa ni kuzorota kwa biashara kwa taasisi hiyo.

Vijana hawa 25 wakiwa katika hali ya kupoteza huko ajira wanakutana na kauli ya viongozi kua vijana mjiajiri maana ajira hakuna.

Vijana hawa wanaenda NSSF ambako kuna mafao yao wanakutana na sheria kua watapatiwa 33% ya salary waliyokua wakipokea kila mwezi kwa miezi Sita tu. Kwa nini?

Kwa sababu waliotunga hiyo sheria wana imani kua katika kipindi cha miezi hyo Sita utakua umepata ajira.

Ajira ipi na serikali imesema hakuna ajira? Basi kujiajiri, najiajiri vipi na hamtaki kunipa hiyo hela yangu yote nikafanye mtaji? Sisi tunafuata sheria.

WATANZANIA WENZANGU! Uongozi tuwape viongozi, UONGOZI tusiwape wanasiasa.
 
Watanzania wenzangu na viongozi wa Nchi hii, hebu tufanye tafakari ya kina juu ya sheria ya mifuko ya jamii na kauli za viongozi Wetu juu ya ajira nchini...
Pole sana
Afu na baada ya hiyo miezi sita kuisha ukienda kuomba kilichobaki uchukue chote wanakwambia uje baada ya miezi 12

Ni shida tupu.
 
Hivi ukiachichwa kazi,ili upate hela zako zote ulizokuwa unachangia unapaswa kudali fao lipi?
 
Duuuuh hii ni hatari sana. Af viongozi wamefumba macho na masikio kama hawaoni haya mateso.
 
Tatizo hapa ni mfume aliyeshiba hamjui mwenye njaaa, kama hela za wachangiaji zinatumika mpk kuzamini harusi kisa harusi ya wasanii maarufu, huu si upuuzi wajati watu wana mashida maswahibu kibao, inapofika mchango ya wanachama wanaanza kuruka ruka ifike mqhqli kufanyike mqpinduzi katika mifuko hii kuondoa wote nq kuweka wengine
 
Back
Top Bottom