Ni kwanini serikali imeshindwa kuwaajiri wahitimu wa fani za mafuta na gesi pamoja na uchache wao?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,317
8,228
Fani za mafuta na gesi zilianza kufundishwa Tanzania mwaka 2013.

Mara serikali ikaanzisha shahada ya kwanza ya kemia ya petroli (BSc. Petroleum Chemistry) (wanafunzi 25), Shahada ya kwanza ya uhandisi wa petroli (BSc. Petroleum Engineering) (Wanafunzi 25) na Shahada ya kwanza ya jiolojia ya petroli (BSc. Petroleum Geology) (wanafunzi 15).

Mwaka 2017, wanafunzi wa kwanza wanahitimu. Lakini serikali inashindwa kuwaajiri pamoja na uchache wao.

Ajira zinatoka TPDC na PURA. Zinaajiri wahitimu wasiozidi sita kwa mwaka. Sasa najiuliza maswali ni jambo gani linazuia kuwaajiri wahitimu wote waliosomea fani hizo.

Ulikua ni mpango wa serikali wa kuandaa wataalamu wa fani hizo katika taifa letu. Tuweke ubinafsi pembeni tuwaajiri wahitimu wote mimi sidhani kama inashindikana. Sio halali mwanafunzi anapata division one ya 5 form six combination ya PCM, na chuo kikuu GPA ya 4.4 taifa linashindwa kumtumia anaamua kuwa auditor kwenye mambo ya uhasibu. Na kwa inavyoonekana ni wengi wala sio mmoja. Tunapaswa kuweka mikakati kama kuna sehemu tumefail tusisite kurudi nyuma na kuanza upya.

Lakini pamoja na kuajiriwa swala la kujiajiri kwa wahitimu wa fani yoyote ni la lazima na hicho ndio kipimo pekee cha kujua kama muhitimu alielewa darasani.

Huu ndio ukweli mhitimu ambaye hawezi kujiajiri maana yake hakuelewa darasani pengine alikua anakalili maarifa bila kuelewa.

Lakini kujiajiri kwa muhitimu kusiwe kisingizio chakutotengeneza ajira katika taifa letu. Bado sisi kama watanzania tunakazi ya kuhakikisha tunatengeneza ajira. Hicho ni kipimo cha ukuaji wa sekta yoyote. Sekta isiyoweza kutengeneza ajira maana yake imesimama kukua.

Hitimisho langu: Sekta ya mafuta na gesi imeshindwa kutimiza malengo iliyojiwekea. Imeshindwa kutengeneza ajira hasa za wahitimu wa gesi na mafuta. Waliokalia viti kwenye sekta ya mafuta na gesi bado hawajafanya kazi vya kutosha. Wanapaswa kuangalia walipoyumba na kufanya marekebisho.

Mwaka 2012 hadi 2013 makampuni ya mafuta na gesi yalijaa Tanzania na yalikua yanajaa vyuoni kuajiri wanafunzi hata kabla hawajamalza vyuo.
Kuna haja ya kubadili uongozi kwenye sekta ya mafuta na gesi ili kurudisha kasi ya kipindi cha nyuma.

Hizi ni baadhi ya hoja ambazo bunge letu lilipaswa kuzizungumzia bungeni na kuwahoji wakuu wa taasisi zinazohusika na mnyororo mzima wa sekta hii. Bunge halipaswi kukaa kimya na kukubali matokeo kasi ya sekta inapokua inashuka.

PENDEKEZO LANGU KWA VIONGOZI:

Pendekezo langu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wizara ya Nishati

Mimi nashauri tungeanzisha wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas). Wizara ya nishati igawanywe mara mbili kuwa wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas) na wizara ya nishati (Ministry of Energy).

Wizara ya nishati (Ministry of Energy) ishughurikie usambazaji na uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo mbalimbali mfano maji, gesi, joto ardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari n.k. TANESCO iwe chini ya Wizara ya nishati. Ateuliwe waziri wa nishati muda wote awaze umeme tu ili kuharakisha na kuboresha uzalishaji na usambazaji wa umeme Tanzania.

Wizara ya mafuta na gesi ishughurikie mambo ya utafutaji wa mafuta na gesi (exploration), uzalishaji wa mafuta na gesi (production), usafishaji wa mafuta na gesi (refining), usambazaji wa mafuta na gesi (distribution), uuzaji wa mafuta na gesi (marketing), uingizaji mafuta kutoka nje ya nchi (import), na uuzaji wa gesi nje ya nchi (export), . TPDC, GASCO, PURA, EWURA upande wa mafuta na gesi ziwe chini ya wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gesi). Ateuliwe waziri wa mafuta na gesi aharakishe na kuiboresha sekta ya mafuta na gesi nchini. Waziri huyo akiwa ofisini kwake awaze mambo ya gesi na mafuta tu, hakika tutapata matokeo kama ya Qatar.

Maeneo muhimu ambayo ningependa hii wizara ihusike nayo ni haya yafuatayo.

1. Utafutaji (Exploration) wa rasilimali za mafuta na gesi asilia (methane na helium)

2. Uzalishaji, usambazaji, na uuzaji wa rasilimali za mafuta na gesi aina zote.

3. Viwanda vya kusafisha mafuta, vilainishi vya mashine, na viwanda vya kuchakata gesi asilia, gesi za vimiminika (LNG na LPG).

4. Matumizi ya gesi asilia kama malighafi ili kupata bidhaa zenye thamani kama mbolea, kemikali, plastics, mafuta n.k; Matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani, kwenye magari nk.

5. Mipango, uendelezaji na udhibiti na usaidizi kwa sekta zote zinazoshughulikiwa na Wizara ya mafuta na gesi (Ministry of Oil and Gas).

6. Mipango, maendeleo na udhibiti wa huduma za mafuta na gesi.

7. Usimamizi wa Sheria mbalimbali zinazohusu Petroli na Gesi Asilia

Ninahisi ikiwa hivi tutaipunguzia wizara ya nishati mzigo, na tutaongeza ufanisi na ukuaji katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.
 
Tatizo hatuna dira ya taifa,
Kila kiongozi anaingia na lake
Nimependa hiyo phrase "dira ya Taifa".

Wenyewe wana kauli yao eti kila Kitabu na zama zake, wakimaanisha kwamba kila Kiongozi wa nchi anakuja na mipango yake, hii siyo sawa hasa kwa Taifa linaloendelea kama Tanzania.

Hata hii Katiba mpya inayopigiwa kelele inaweza isiwe mwarobaini wa haya mambo ya hovyo yanayotokea nchini.

Mwl Nyerere akizungumzia ubovu wa Katiba tuliyonayo na umuhimu wa kuwa na Katiba mpya aliwahi kutoa angalizo kwamba bila DIRA ya Taifa hata tukiwa na Katiba mpya nzuri kiasi gani, uozo utakuwa ni uleule, akatolea mfano wa Germany kwa Adolf Hitler by then, kumbe kwa kipindi kile Germany ndiyo ilikuwa na Katiba bora kabisa duniani ila Hitler akapenyeza Udikteta, Hitler alifanikiwa kwasababu Germany haikuwa na dira ya Taifa pamoja na kuwa na Katiba bora.

All in all, muda ndiyo mwamuzi mzuri. Ngoja iendelee kunyesha tuone panapovuja.
 
Hongera kwa andiko zuri.
 
Fani za mafuta na gesi zilianza kufundishwa Tanzania mwaka 2013.

Mara serikali ikaanzisha shahada ya kwanza ya kemia ya petroli (BSc. Petroleum Chemistry) (wanafunzi 25), Shahada ya kwanza ya uhandisi wa petroli (BSc. Petroleum Engineering) (Wanafunzi 25) na Shahada ya kwanza ya jiolojia ya petroli (BSc. Petroleum Geology) (wanafunzi 15).

Mwaka 2017, wanafunzi wa kwanza wanahitimu. Lakini serikali inashindwa kuwaajiri pamoja na uchache wao.

Ajira zinatoka TPDC na PURA. Zinaajiri wahitimu wasiozidi sita kwa mwaka. Sasa najiuliza maswali ni jambo gani linazuia kuwaajiri wahitimu wote waliosomea fani hizo.

Ulikua ni mpango wa serikali wa kuandaa wataalamu wa fani hizo katika taifa letu. Tuweke ubinafsi pembeni tuwaajiri wahitimu wote mimi sidhani kama inashindikana. Sio halali mwanafunzi anapata division one ya 5 form six combination ya PCM, na chuo kikuu GPA ya 4.4 taifa linashindwa kumtumia anaamua kuwa auditor kwenye mambo ya uhasibu. Na kwa inavyoonekana ni wengi wala sio mmoja. Tunapaswa kuweka mikakati kama kuna sehemu tumefail tusisite kurudi nyuma na kuanza upya.

Lakini pamoja na kuajiriwa swala la kujiajiri kwa wahitimu wa fani yoyote ni la lazima na hicho ndio kipimo pekee cha kujua kama muhitimu alielewa darasani.

Huu ndio ukweli mhitimu ambaye hawezi kujiajiri maana yake hakuelewa darasani pengine alikua anakalili maarifa bila kuelewa.

Lakini kujiajiri kwa muhitimu kusiwe kisingizio chakutotengeneza ajira katika taifa letu. Bado sisi kama watanzania tunakazi ya kuhakikisha tunatengeneza ajira. Hicho ni kipimo cha ukuaji wa sekta yoyote. Sekta isiyoweza kutengeneza ajira maana yake imesimama kukua.

Hitimisho langu: Sekta ya mafuta na gesi imeshindwa kutimiza malengo iliyojiwekea. Imeshindwa kutengeneza ajira hasa za wahitimu wa gesi na mafuta. Waliokalia viti kwenye sekta ya mafuta na gesi bado hawajafanya kazi vya kutosha. Wanapaswa kuangalia walipoyumba na kufanya marekebisho.

Mwaka 2012 hadi 2013 makampuni ya mafuta na gesi yalijaa Tanzania na yalikua yanajaa vyuoni kuajiri wanafunzi hata kabla hawajamalza vyuo.
Kuna haja ya kubadili uongozi kwenye sekta ya mafuta na gesi ili kurudisha kasi ya kipindi cha nyuma.

Hizi ni baadhi ya hoja ambazo bunge letu lilipaswa kuzizungumzia bungeni na kuwahoji wakuu wa taasisi zinazohusika na mnyororo mzima wa sekta hii. Bunge halipaswi kukaa kimya na kukubali matokeo kasi ya sekta inapokua inashuka.
Njaa itakuua, kudadadeki unakaribia kuchanganyikiwa Sasa.
 
Waajiliwe wapi sasa?serikali haichimbi mafuta wala gesi,tipper imejaa watunga sera tu,hakuna exproration yeyote inayofanywa,
Makampuni yanayochimba gesi na mafuta,ni ya nje,yanakuja na wataalamu wao,sasa hawawezi kuchukua Hawa ambao hawana hata uzoefu,kwa kijana wa bongo,nyakati hizi anza kutafuta kazi nje ya mipaka,enzi hizo naanza kazi,nilikuta kaka zangu wapo vodacom,Tena wazee,lakini mpaka leo wapo voda huko,wanazidi kupanda vyeo,sasa wewe kijana utapata nafasi wapi,
Nilikuwa SA,Kwenye makampuni ya Scania,Emerson,caterpillar nilikuta wakenya,Nigeria,na wacongo kibao,
Mkenya haoni shida kuzamia SA akaoa mwenyeji Ili apate uhuru wa Kupiga Mishe Mishe zake,mbongo mgogo ukimuambia aende akaishi na kuoa Mtwara,au kagera anaona tabu
 
Ahsante kwa ushauri mzuri. Sasa wewe mfano ukipewa uongozi kwenye hiyo sekta maana yake hutoweza kufanya mabadiliko yeyote kwasababu wengine wameshindwa?
 
Back
Top Bottom