Familia za wavivu wengi zimesababisha soko la wanawake wa kuolewa na wanaume wa kuoa liwe gumu sana. Watu wanaogopa kupata wakwe na mashem wategemezi

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,870
6,278
Habari wadau.

Ukweli mchungu soko la mwenza wa ndoa limekuwa gumu sana Tanzania hasa kwa watu wanaojielewa na waliojipata.

Mtu kuoa ama kuolewa anatazama mwenza wake yukoje , kwao anapotoka pakoje, na ndugu zake ama ukoo wake ukoje? Je wana maisha ya kujitegemea.

Yale mambo ya kuoa mwanamke kisha wadogo zake wote wanaamia kwake na wazazi wanataka wajengewe hapo hapo na nyinyi familia changa watu hawayataki

Now days wanawake wanaotoka familia mambo safi zenye maisha ndio wana soko kubwa la kuolewa

Pia wanaume wanaotoka familia zenye maisha na mambo safi wana soko kubwa la kuoa wanayemtaka.

Career ya mtu pia ni factor kubwa kwenye soko la kuoa ama kuolewa.

Mfano Mc wa harusi namba moja Tanzania jina Kapuni alikuwa na mchumba wake waliefikia stage ya kuzaa mtoto kabisa mwanzoni mwa miaka ya 2010s. ila kwenye kuoa aligoma kumuoa huyo binti sababu kwao na binti hapaeleweki kumejaa wavivu.. wategemezi wapo wengii . Akaona hawezi kujitishwa mzigo wa majukumu.

Akaenda kusaka demu anaetoka mambo safi, mtoto wa Dr wa chuo kikuu cha taifa akaoa.

Huo ni mfano mmojawapo ila ipo mingi sana.

Soko la ndoa zama hizi kila upande unaogopa wategemezi wengi.

Wakaka na wadada tujitahidi kubebana familia zetu kupunguza utegemezi. La sivyo mabinti zetu ndoa watakuwa wanaziona kwa wenzao tu.

Nowdays ngumu sana kuona mtoto wa baba CEO kama kimei anaoa mtoto wa mkulima.

Wenye maoni mnaweza ongezea mawazo yenu.
 
Kwani huyo mc namba moja katokea familia mambo safi?

Nahisi Hapana..ila alioa akiwa tayari ameshajipata mambo safii yeye mwenyewe.. kama ni Anaetajwa ni MC Garab alioa akiwa tayari ameshakuwa na hela nzuri tu.

Labda kama mtoa mada anamuongelea MC mwingine.
 
Huyo garab alimzalisha mtoto wa watu na kumuacha kisa kwao hawajiwezi?
 
Habari wadau.

Ukweli mchungu soko la mwenza wa ndoa limekuwa gumu sana Tanzania hasa kwa watu wanaojielewa na waliojipata...
Kama unaoa kwa sababu anatoka familia inayojiweza hapo umeoa mtu tegemezi ambae alikua anategemea uwezo wa mzazi wake na sio yeye mwenye uwezo, wengi wa wanawake wa aina hii huwa wana gharama kubwa kuishi nao, hawajazoea na wala hawajui maisha ya shida,,,na pia uwezekano wa watu kuhamia kwako upo itategemea na huyo mzazi wao ambae ndie mwenye uwezo ana misimamo gani kwenye malezi ya familia yake.
 
Kama unaoa kwa sababu anatoka familia inayojiweza hapo umeoa mtu tegemezi ambae alikua anategemea uwezo wa mzazi wake na sio yeye mwenye uwezo,,wengi wa wanawake wa aina hii huwa wana gharama kubwa kuishi nao,,,hawajazoea na wala hawajui maisha ya shida,,,na pia uwezekano wa watu kuhamia kwako upo itategemea na huyo mzazi wao ambae ndie mwenye uwezo ana misimamo gani kwenye malezi ya familia yake.
Good.
 
Habari wadau.

Ukweli mchungu soko la mwenza wa ndoa limekuwa gumu sana Tanzania hasa kwa watu wanaojielewa na waliojipata.

Mtu kuoa ama kuolewa anatazama mwenza wake yukoje , kwao anapotoka pakoje, na ndugu zake ama ukoo wake ukoje? Je wana maisha ya kujitegemea.

Yale mambo ya kuoa mwanamke kisha wadogo zake wote wanaamia kwake na wazazi wanataka wajengewe hapo hapo na nyinyi familia changa watu hawayataki

Now days wanawake wanaotoka familia mambo safi zenye maisha ndio wana soko kubwa la kuolewa

Pia wanaume wanaotoka familia zenye maisha na mambo safi wana soko kubwa la kuoa wanayemtaka.

Career ya mtu pia ni factor kubwa kwenye soko la kuoa ama kuolewa.

Mfano Mc wa harusi namba moja Tanzania jina Kapuni alikuwa na mchumba wake waliefikia stage ya kuzaa mtoto kabisa mwanzoni mwa miaka ya 2010s. ila kwenye kuoa aligoma kumuoa huyo binti sababu kwao na binti hapaeleweki kumejaa wavivu.. wategemezi wapo wengii . Akaona hawezi kujitishwa mzigo wa majukumu.

Akaenda kusaka demu anaetoka mambo safi, mtoto wa Dr wa chuo kikuu cha taifa akaoa.

Huo ni mfano mmojawapo ila ipo mingi sana.

Soko la ndoa zama hizi kila upande unaogopa wategemezi wengi.

Wakaka na wadada tujitahidi kubebana familia zetu kupunguza utegemezi. La sivyo mabinti zetu ndoa watakuwa wanaziona kwa wenzao tu.

Nowdays ngumu sana kuona mtoto wa baba CEO kama kimei anaoa mtoto wa mkulima.

Wenye maoni mnaweza ongezea mawazo yenu.
Usiseme wavivu kuna ukosefu wa ajira kumbuka halafu kuoa mwanamke ambaye kwao kuna uwezo naye ni tegemezi pia hapo kwao muhimu ni kuangalia mtu ambaye anajiudumia mahitaji yake yeye mwenyewe.
 
Maisha sometimes Yana shangaza ...
Mnaweza itwa wavivu kisa kipato kidogo huku mnachakarika Ile mbaya.....nawajua watu wengi masikini lakini sio wavivu Kabisa...

Mnaweza onekana wachakarikaji kumbe Baba alikuwa mwizi Tu "Serikalini" akanyoosha maambo yakawa mepesi .. investment za uhakika...basi waswahili wanawaona ..."familia Fulani inajielewa"...

Binafsi naona familia zenye maadili ndo umebahatika hata kama ni masikini.... Maadili Tu ...yanatosha...pesa na Mali Wengi huja kuzipata baadae.
 
Kuna jamaa mmoja alioa kwenye familia mambo safi kwa matarajio kuwa naye atanusanusa mali za ukweni, badaye alipotaka kusogeza pua shemeji yake mkubwa akamwambi ulimuoa fulani hukuoa familia kaa mbali na mali za kwetu, jamaa yupoyupo tu matarajio yote kwishaaaa.
 
Naam naam mkuu well said perfect kabisa
 
Kuna jamaa mmoja alioa kwenye familia mambo safi kwa matarajio kuwa naye atanusanusa mali za ukweni, badaye alipotaka kusogeza pua shemeji yake mkubwa akamwambi ulimuoa fulani hukuoa familia kaa mbali na mali za kwetu, jamaa yupoyupo tu matarajio yote kwishaaaa.
Ndio maana mimi nimetangulia kumwambia huko juu atuoi familia au ukoo
 
Back
Top Bottom