Eti Pisi (Wanawake) wa JF ni wabovu? 🙆🏿‍♂️

Eti Pisi (Wanawake) wa JF ni wabovu? 🙆🏿‍♂️

Ndomana nikisema humu JF kuna wachawi watu wanabisha.

Huyu jamaa ana element zote znazo ashilia ni mchawi na mtu wa kufwatilia maisha ya watu.

Haiwezekani unashinda humu kufwatilia ID gani inalala mda gani na kutoka online mda gani.
Bwana steve! Kunywa hata asali nipe lipa namba chaaapp🤸🏽‍♂️

People are really sick! Yani niamkie jf au nilale we inakuhusu nini? Nakula kwako! Dumb ass mahfAcka🙄
 
Tatizo watu wana matarajio makubwa sana juu ya watu walio mitandaoni bila kujua kwamba tuliomo humu ndio tupo na mitaani. Wanatamani member wa jf tuwe wazuri kama malaika😌😌😌.

Ila ule uzi wa selfika ufutwe tu. Ukisoma ule uzi sio wanaume tu, hata wanawake kutwa nzima kutukana na kudhalilisha wanawake wenzao. Unakuta mwanamke kila siku ni ku body shame wanawake wenzao. Sasa kama sisi tu tunadhalilishana namna hiyo ndio iwe kwa wanaume?
Asante
Cc Moderator Maxence Melo
Kabla mambo hayajawa mengi mzingatie ushauri , futeni
 
Bahati mbaya huenda hajakutana na mdada hata mmoja, ni assumptions zake tu, hasa baada ya kukataliwa huko piemuni. Hasira za kuwa rejected ni mbaya sana, mbinu zake za kuwapata hawa watu hata kuonana tu zimekuwa butu sana huyu kijana...
😁😁
 
Wasalaam wakuu,

Kumekuwa na tabia mbaya humu JamiiForums ya baadhi ya vijana wa kiume kuanzisha nyuzi au kutoa comments za kuwakejeli na kuwabeza wanawake baada ya kuona picha zao kwenye jukwaa la Selfika.

Kwa kweli hii inasikitisha na inatufedhehesha wanaume.

Kaka, kama hujapendezwa na mwonekano wa dada fulani, pita tu. Si lazima kila unachokiona ukikosoe. Huna jukumu la kuwa jaji wa sura, miili au thamani ya wanawake wa JF.

Jiulize: Unapata faida gani kumdhalilisha mtu? Maisha yako yanabadilika? Unakuwa mwanaume bora? Au unajisikia tu vizuri baada ya kumuumiza mtu ambaye hakukufanya chochote?

Mwanaume mwenye kujitambua anajua tofauti kati ya preference na disrespect. Unaweza kusema “si aina yangu” bila kumdhalilisha mtu.

Na kabla hujaandika comment ya kumkejeli mwanamke kwa mwonekano wake, kumbuka nyumbani kwako kuna mama, dada, shangazi, mke au binti. Je, ungefurahia mwanaume mwingine akiwadhalilisha kwa namna hiyo?

Uhuru wa kuandika sio ruhusa ya kukosa staha.

Kijana, tafuta KISUDI cha maisha yako. Fanya kazi zako, biashara yako, familia yako na akili yako. Dunia ina mambo mengi ya kutatua kuliko kukaa nyuma ya keyboard kuwavunjia wanawake heshima.

Kumshusha mwanamke hakukufanyi uwe mwanaume zaidi.

Kama picha haikupendezi, scroll down.
Kama sio type yako, endelea na maisha yako.
Lakini heshima ibaki.

JamiiForums ni sehemu ya mijadala, sio uwanja wa kuwavunjia watu utu

Mwanaume wa kweli hahitaji kumdhalilisha mwanamke ili ajisikie yeye ni mwanaume
Pisi za Jamii forum ni

🔹 Dada zako

🔹 Mama yako, shangazi zako

🔹 Mliosoma darasa Moja

🔹 Majirani zako

🔹 Wafanyakazi wenzako

Kila Mmoja akoingia kwa akaunti feki lakini ni Jamii iliyokuzunguka
.JF sio Kijiji, nyumba Wala shimo. Hawa Hawa waliopo Jf ndio hili aliopo Twitter ,Facebook inster ,club house, TikTok, discord nk ana swichi tuu dakika hii yupo Je dakika inayofuata yupo Twitter kwa uhusika na majina tofauti. Hivyo chukua tahadhari utakujan kumtongoza mama. yako au Binti yako ukiamini ni pisi kali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom