Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,592
- 56,832
Wasalaam wakuu,
Kumekuwa na tabia mbaya humu JamiiForums ya baadhi ya vijana wa kiume kuanzisha nyuzi au kutoa comments za kuwakejeli na kuwabeza wanawake baada ya kuona picha zao kwenye jukwaa la Selfika.
Kwa kweli hii inasikitisha na inatufedhehesha wanaume.
Kaka, kama hujapendezwa na mwonekano wa dada fulani, pita tu. Si lazima kila unachokiona ukikosoe. Huna jukumu la kuwa jaji wa sura, miili au thamani ya wanawake wa JF.
Jiulize: Unapata faida gani kumdhalilisha mtu? Maisha yako yanabadilika? Unakuwa mwanaume bora? Au unajisikia tu vizuri baada ya kumuumiza mtu ambaye hakukufanya chochote?
Mwanaume mwenye kujitambua anajua tofauti kati ya preference na disrespect. Unaweza kusema “si aina yangu” bila kumdhalilisha mtu.
Na kabla hujaandika comment ya kumkejeli mwanamke kwa mwonekano wake, kumbuka nyumbani kwako kuna mama, dada, shangazi, mke au binti. Je, ungefurahia mwanaume mwingine akiwadhalilisha kwa namna hiyo?
Uhuru wa kuandika sio ruhusa ya kukosa staha.
Kijana, tafuta KISUDI cha maisha yako. Fanya kazi zako, biashara yako, familia yako na akili yako. Dunia ina mambo mengi ya kutatua kuliko kukaa nyuma ya keyboard kuwavunjia wanawake heshima.
Kumshusha mwanamke hakukufanyi uwe mwanaume zaidi.
Kama picha haikupendezi, scroll down.
Kama sio type yako, endelea na maisha yako.
Lakini heshima ibaki.
JamiiForums ni sehemu ya mijadala, sio uwanja wa kuwavunjia watu utu
Mwanaume wa kweli hahitaji kumdhalilisha mwanamke ili ajisikie yeye ni mwanaume