Bila shaka serikali (TBS, TFDA na FCC) wameshindwa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki nyingi mno kwenye soko. Pia serikali inaonesha dhahiri kuwa haina nia ya kusimamia viwango vya ubora.
Kwa mfano, kuna sheria ya manunuzi inayozuia serikali kununua vitu (mashine kubwa, mitambo, nk) chakavu. Hii sheria iko wazi kabisa na mazingira yaliyopelekea sheria hii kutungwa yanaeleweka kwa kila Mtanzania. Lakini kiongozi wa juu kabisa serikalini anasimama na kusema "sheria isiwe kikwazo" kwa shirika la umma nyeti kununua mitambo chakavu ya kuzalishia umeme. Yote hii wakati kuna mitambo mipya na ya bei nafuu zaidi inayoweza kupatikana katika soko. Katika hali hii tunategemea serikali hiyo hiyo iwajibike kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki kama simu, nguo, pasi, TV, vyakula, madawa, nk?
Maadqam tumebaini serikali haina uwezo/nia ya kulinda wananchi wake, inabidi wanunuzi tubuni njia mbadala za kujilinda kama kupeana habari kupitia JF na social sites zingine. Hii thread imenielimisha sana. Tukiwa na maarifa, hili tatizo litapungua sana.
Hii ishu ya bidhaa hafifu/bandia si mzaha. Tutaangamia WOTE kama taifa.