nakubaliana na wewe kwenye yote uliyoandika, isipokuwa ubora wa bidhaa kuwa za Game zina nafuu kwani zinatoka SA.
Issue ya ubora wa bidhaa nafikiri ni tatizo linaloanzia kwetu, yaani TBS na TDFA. Sina uhakika kama tuna viwango kwa bidhaa zote zinazoingizwa nchini, na hata kama tuna viwango, je kuna uthibiti wa kutosha. Ulaya na hata SA wanapata vitu vya kutoka China/Thailand, lakini kwa vile wana viwango basi ubora wa bidhaa zao siku zote unakidhi viwango.
Kuna wakati mimi nilinunua bidhaa fulani ya umeme hapo Game, kufika nyumbani ndiyo nikaona kuwa sehemu ya kuchomeka kwenye soketi si wa viwango vya kwetu. Nilipiga simu TBS kuuliza inakuwaje duka kubwa kama Game linauza vifaa ambayo si vya viwango vya kwetu, majibu niliyoyapata huko siwezi kuandika hapa, kwani yanaonyesha ni kwa kiwango gani hakuna umakini.
Nini tufanye? Kwavile TBS, TDFA, FCC zinaonyesha kushindwa kufanya kazi yao sawasawa, basi nguvu ya umma itumike kuwalazimisha kutenda kazi yao. Kwa wenzetu wanaojua kuhusu mapungufu yaliyopo kwenye bidha mbalimbali zinazoingizwa kwenye soko wasikae na taarifa hizo badala yake wajitahidi kuwafikishia watu wengi kadiri inavyowezekana. JF, nakala kwenye magazeti, nk kuwataarifu waTZ.