Kampuni ya LG Electronics yashusha duka jingine jipya Mlimani City DAR

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kampuni ya LG Electronics imezindua duka jingine jipya la pili na la kisasa katika eneo la Mlimani City Mall jijini Dar kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kupata vifaa vya kampuni hiyo kwa urahisi ambavyo ni rafiki kwa mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar na kushuhudiwa na umati wa watu mbalimbali waliohudhuria kujionea baadhi ya bidhaa hizo za kisasa na za kiteknolojia ambazo ni pamoja na friji, televisheni, mashine za kufua nguo na vifaa vingine.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim alisema duka hilo ni pili hapa Tanzania baada ya jana kuzindua duka la kwanza katika mitaa ya Posta karibu na Mnara wa saa jijini Dar.

“Posta na Mlimani City ni maeneo mwafaka kabisa kwa sababu ya wateja wengi wanatembelea maeneo hayo na tumejionea namna mazingira ya biashara Tanzania yalivyochangamka.

Tunaahidi kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa nzuri ili wajisikie fahari wakati wanafanya manunuzi kwani watahudumiwa na wafanyakazi wetu wenye utaalamu wa hali ya juu” “Katika miaka michache iliyopita, tumekuwa tukitanua wigo na uwepo wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

" Tuna mpango wa kuendelea kukuza bidhaa zenye hadhi ya premium na kuwapa wateja wetu bidhaa wanazotarajia wao binafsi na kama biashara kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa zaidi ya daraja la kwanza".

"Tutawapa wafanya biashara wa Tanzania fursa nzuri ya kufanya kazi na sisi mfano mzuri ukiwa ni MeTL ambaye ni msambazaji mkuu wa bidhaa zetu za LG hapa Tanzania pamoja na dealers kama F&S ambaye ni mfanyabiashara wa kwanza katika mpango wetu wa thamani wa Tanzanite Club Tanzania” alisema Kim.

Aidha, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya MeLT, Fatema Dewji ametoa wito kwa Watanzania kutumia vifaa vya kielektroniki kutoka kampuni ya LG kwa kuwa ni vifaa ambavyo rafiki kwa mazingira.

Dewji ametoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa duka la pili la kampuni hiyo ya LG Electronics lililopo Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alisema MeTL inashirikiana na LG katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki kutoka LG hapa nchini ambavyo ni pamoja na runinga, mashine za kufua nguo, friji na vifaa vingine.

“Vifaa hivi vina ubora wa juu lakini pia vinatumia teknolojia mpya ambayo inatumia umeme mdogo na rafiki kwa mazingira ndio maana hata sasa tunaona kuwa Watanzania wamekubali bidhaa za LG hii ina maanisha kuwa Tanzania kuna soko kubwa” alisema.

Kauli hiyo ya pia iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji ambaye alitoa wito kwa Watanzania kutembelea maduka hayo ya LG ili kujionea bidhaa bora na kufanya uamuzi sahihi katika ununuzi wa bidhaa za majumbani mwao.

Kwa upande wake Henry Chami ambaye ni mwakilishi kampuni ya F&S inayojishughulisha na uuzaji na usambaji wa bidhaa za kielekroniki, alisema katika kipindi cha mwezi mmoja Watanzania watapa fursa ya kununua bidhaaza LG katika dula hilo la Mlimani City kwa bei punguzo hadi asilimia 25.

“Ofa hiyo inalenga kutoa motisha kwa Watanzania kupata bidhaa bora za LG kwa sababu mbali na ubora na teknolojia ya hali ya juu iliyotumika kutengeneza pia upatikanaji wake ni wa urahisi zaidi,” alisema.

CAPTION1. Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa vya kielektroniki vya kampuni hiyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.

2. Mwakilishi wa kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kielektroniki-F&S, Henry Chami (katikati), akikata utepe kuashiri uzinduzi wa duka la pili la vifaa vya kielektroniki kutoka Kampuni ya LG Mlimani City jijini Dar.

Kulia ni Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim na kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji.3. Meneja Masoko kutoka kampuni ya LG Electronics, David Kessy (wa kwanza kushoto), pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo. 4. Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji ambao ni washirika wa usambazaji wa vifaa vya LG, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa hivyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.
IMG-20210609-WA0012.jpg
IMG-20210609-WA0013.jpg
IMG-20210609-WA0014.jpg
IMG-20210609-WA0011.jpg

IMG-20210609-WA0013.jpg

IMG-20210609-WA0011.jpg

IMG-20210609-WA0014.jpg
 
Picha za duka zi wapi?

Halafu hao kina Dewji, mbona kama nao ni washindani wa LG kwenye electronics sababu wana products zao ikiwemo TV wanaziita sijui MO electronics vile
 
Ni wale wale tu.
 
Kampuni ya LG Electronics imezindua duka jingine jipya la pili na la kisasa katika eneo la Mlimani City Mall jijini Dar kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kupata vifaa vya kampuni hiyo kwa urahisi ambavyo ni rafiki kwa mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar na kushuhudiwa na umati wa watu mbalimbali waliohudhuria kujionea baadhi ya bidhaa hizo za kisasa na za kiteknolojia ambazo ni pamoja na friji, televisheni, mashine za kufua nguo na vifaa vingine.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim alisema duka hilo ni pili hapa Tanzania baada ya jana kuzindua duka la kwanza katika mitaa ya Posta karibu na Mnara wa saa jijini Dar.

“Posta na Mlimani City ni maeneo mwafaka kabisa kwa sababu ya wateja wengi wanatembelea maeneo hayo na tumejionea namna mazingira ya biashara Tanzania yalivyochangamka.

Tunaahidi kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa nzuri ili wajisikie fahari wakati wanafanya manunuzi kwani watahudumiwa na wafanyakazi wetu wenye utaalamu wa hali ya juu” “Katika miaka michache iliyopita, tumekuwa tukitanua wigo na uwepo wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

" Tuna mpango wa kuendelea kukuza bidhaa zenye hadhi ya premium na kuwapa wateja wetu bidhaa wanazotarajia wao binafsi na kama biashara kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa zaidi ya daraja la kwanza".

"Tutawapa wafanya biashara wa Tanzania fursa nzuri ya kufanya kazi na sisi mfano mzuri ukiwa ni MeTL ambaye ni msambazaji mkuu wa bidhaa zetu za LG hapa Tanzania pamoja na dealers kama F&S ambaye ni mfanyabiashara wa kwanza katika mpango wetu wa thamani wa Tanzanite Club Tanzania” alisema Kim.

Aidha, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kampuni ya MeLT, Fatema Dewji ametoa wito kwa Watanzania kutumia vifaa vya kielektroniki kutoka kampuni ya LG kwa kuwa ni vifaa ambavyo rafiki kwa mazingira.

Dewji ametoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa duka la pili la kampuni hiyo ya LG Electronics lililopo Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alisema MeTL inashirikiana na LG katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki kutoka LG hapa nchini ambavyo ni pamoja na runinga, mashine za kufua nguo, friji na vifaa vingine.

“Vifaa hivi vina ubora wa juu lakini pia vinatumia teknolojia mpya ambayo inatumia umeme mdogo na rafiki kwa mazingira ndio maana hata sasa tunaona kuwa Watanzania wamekubali bidhaa za LG hii ina maanisha kuwa Tanzania kuna soko kubwa” alisema.

Kauli hiyo ya pia iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji ambaye alitoa wito kwa Watanzania kutembelea maduka hayo ya LG ili kujionea bidhaa bora na kufanya uamuzi sahihi katika ununuzi wa bidhaa za majumbani mwao.

Kwa upande wake Henry Chami ambaye ni mwakilishi kampuni ya F&S inayojishughulisha na uuzaji na usambaji wa bidhaa za kielekroniki, alisema katika kipindi cha mwezi mmoja Watanzania watapa fursa ya kununua bidhaaza LG katika dula hilo la Mlimani City kwa bei punguzo hadi asilimia 25.

“Ofa hiyo inalenga kutoa motisha kwa Watanzania kupata bidhaa bora za LG kwa sababu mbali na ubora na teknolojia ya hali ya juu iliyotumika kutengeneza pia upatikanaji wake ni wa urahisi zaidi,” alisema.

CAPTION1. Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa vya kielektroniki vya kampuni hiyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.

2. Mwakilishi wa kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kielektroniki-F&S, Henry Chami (katikati), akikata utepe kuashiri uzinduzi wa duka la pili la vifaa vya kielektroniki kutoka Kampuni ya LG Mlimani City jijini Dar.

Kulia ni Mkurugenzi Mtendji wa LG Electronics Afrika Mashariki, SaNyoung Kim na kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji.3. Meneja Masoko kutoka kampuni ya LG Electronics, David Kessy (wa kwanza kushoto), pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo. 4. Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji ambao ni washirika wa usambazaji wa vifaa vya LG, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa hivyo katika eneo la Mlimani City jijini Dar.View attachment 1813274View attachment 1813276View attachment 1813277View attachment 1813278

View attachment 1813272

View attachment 1813273

View attachment 1813275
Wabongo wanajaa mule ndani kubadilisha line za simu tu
 
Back
Top Bottom