Epukeni bidhaa za Game Mlimani City!

Epukeni bidhaa za Game Mlimani City!

Daima vya bure vina gharama............wanajipamba kwa punguzo la bei kumbe wana lao jamboo.
 
tatizo kubwa liko kwenye vyakula, kuna watu maalumu kazi yao ni kufuta expire dates na kuzirekebisha ili bidhaa ionekane bado hipo kwenye muda wake, tuwe waangalifu sana especially mwisho wa mwezi kwenye hizo wanazoita promotion ambazo lengo lake ni kuflush out expired au low quality product(reject)
 
Very Interesting,but i have already buy a shampoo from Game it is just fine. So we should be aware with eating staff or those items which are promoted in their every week magazine??
 
mimi nilishasema kuhusu pale lakini watu eti wakata ushahidi, pale ni full usanii, kuanzia kwenye contract ya wale jamaa wa chuo na huyo mwarabu wao. mtu mna mpa eneo lote lile afanyie biashara kwa miaka 50 nd' arudishe.............. natamani hata niandamane
 
Hata cinema pale ni feki ... juzi nimeangalia moja tu sasa hivi jicho langu moja limevimba, linauma kinoma.

Kuna mshakaji wiki iliyopita ametoa pesa ATM, baadaye anajikuta na feki tupu...
 
Wanunuzi wa bidhaa pale GAME Mlimani Sity jihadharini na bidhaa hizo.Kuna tetesi kuwa bidhaa nyingi hapo dukani ni mbovu na zina matatizo.Mimi mwenyewe nienunua karibu bidhaa tatu ambazo ziliharibika kipindi kifupi tu baada ya matumizi.These items are used and repacked!!!

Umesha wahi kununua duka lolote kubwa zaidi ya game kabla? Nadhani hii sio jambo sahihi kibiashara kununua mara moja kitu ukaona kibovu ukatoka na matangazo kuwa duka lile lina bidhaa feki. Niliwahi kununua computer Media Market Amsterdam wakati fulani, ikafika home ikagoma ina two days nikarudisha nikabadirishiwa nyingine nayo after one week ikafaa, nikaipeleka service centre yao wakaikarabati bado ikawa inachemsha, baadaye wakanipa nyingine, ipo makini na inachapa kazi miaka inaenda hakuna cha kuchechemea wala nini.

Maduka kama Super Spar UK kwa vyakula (utaona kadosari sehemu), maduka makubwa kama walmart huwa lazima yana tujidosari sehemu fulani lakini huwezi kucondemn biashara ya mtu kuwa ina mali feki, unahitajika utafiti wa kina kufikia azimio hilo. Na hapa naomba mkuu nikuambie unaambie sample yako ilikuwa kubwa kiasi gani, methodology yako na umefanyaje analysis yako. Tuwe tunaongea kwa data sio madam kitu cha mgeni basi tunakikandia.

Anayejaza fedha kwenye ATM nani? kumbuka pesa za ATM ni zile zile tunazoweka wateja Benki, kwa hiyo kama kuna mteja mmoja alipeleka note feki benki, na teller hakuwa makini akapokea na utaratibu mzima wa uhakiki na upakiji haukufuatwa basi hapo utapokea note feki kwenye ATM.

watu wamekatikiwa Umeme wakati kadi imetoka na pesa bado hawajachukua na ATM ikasoma pesa zilichukuliwa, lakini bado huwezi kulaumu ATM au sehemu ilipo. Naomba Data zaidi kwanini conclusion yako iko hivyo ilivyo?
 
Hata cinema pale ni feki ... juzi nimeangalia moja tu sasa hivi jicho langu moja limevimba, linauma kinoma.

Kuna mshakaji wiki iliyopita ametoa pesa ATM, baadaye anajikuta na feki tupu...

Mkuu kwenye site yako ya kupima kama umependana kweli na mpenzi wako kwanini umeweka option tatu? inamaana umehalarisha watu kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja. Ngoja nikufungulie thread sehemu wewe.
 
tatizo kubwa liko kwenye vyakula, kuna watu maalumu kazi yao ni kufuta expire dates na kuzirekebisha ili bidhaa ionekane bado hipo kwenye muda wake, tuwe waangalifu sana especially mwisho wa mwezi kwenye hizo wanazoita promotion ambazo lengo lake ni kuflush out expired au low quality product(reject)

sio nia yangu kuwatetea Game, lakini nachotaka kueleza ni kuwa utaratibu wa kupunguza bei vitu vinapokaribia ku-expire sio upo hapo game tu, maduka makubwa yote karibu hufanya hivyo. Unajua kwenda kutupa vitu vilivyoexpire ni gharama kwao, kwa hiyo wakati mwingine unakuta duka kwa mfano wanauza makopo ya mitindi kama sita hivi kwa bei ya kopo moja, wanachotaka wateja mchukue kama huna watu wa kula wakamaliza ukiwa home mzigo unakufia. Huu ni utaratibu wa kawaida. lakini kwa vile tulishazoea kununua mabandani (utumbo wa ngómbe hata ujui umetokana na Ng'ombe kweli) na nyanya zetu zakupangwa chini hata mifereji ya wenye kutapisha inapita hapo hapo sasa tunaona shida sana kuzoea huu utaratibu wa maduka makubwa.

Ushauri wa bure: kama imetushinda ni bora kurudi kule kwenye magenge na wamachinga tulikozoea ambako hata bei unaweza kubishana wakakupunguzi mara mia ya bei harisi (kama unaamini) kuliko hizo promotion za kununua kwa kadi sijui za VISA mara tunapoke Master card. Itatuchukua muda sana wadanganyika mpaka tuje tuwe sawa na dunia ya wenzetu.
 
sio nia yangu kuwatetea Game, lakini nachotaka kueleza ni kuwa utaratibu wa kupunguza bei vitu vinapokaribia ku-expire sio upo hapo game tu, maduka makubwa yote karibu hufanya hivyo. ...

....Itatuchukua muda sana wadanganyika mpaka tuje tuwe sawa na dunia ya wenzetu.

Mimi naona Game safi tuu. Mnunuzi lazima ujue unacho nunua ni nini? ukiingia mkenge ukanunua TV inaitwa lasonic ukifikiri ni Sony usilaumu....

We have to become educated consumers. Kama huna uhakika, uliza hata hapa forum kabla ujamwaga pesa. mafundi ninao watumia huwa nawauliza kwanini hamnunulii vifaa vyenu hapo Game? Jibu: "tunasikia bidhaa zao nifeki." Anasema hivyo wakati anatumia drili yangu nilio inunua Game two years ago !!
 
jamani lisemwalo ..... kama halipo basi laja......

Basi tungesubiri lifike kwanza. Ukienda kariakoo vile vibanda vya ndugu zangu wakinga i mean maduka, unanunua bidha feki tupu hakuna hata Guarantee, hapo Gnae jamaa angalau hata wanatoa guarantee kwa bidhaa nyingi tu bado tunawalaumu. Nimefanya shoppings kwenye games za SA na Botswana inawezekana shida ni manegement ya TZ ndio imeoza, lakini nachojua haya maduka ya chain (Franchise) lazima yawe na standard moja. Kwa hiyo sitegemei Game ya Mlimani iwe tofauti na game ya Mgodisane (Gaborone). Huyo mwendesha sinema sidhani kama ni game, unachotakiwa kujua kuwa Game ana duka lake humo ndani na wengine ni wapangaji tu, hata wewe na mimi tunaweza tukapanda pale na kuendesha biashara yetu, kwa hiyi tukichemsha sio Game, yeye ni Baba Mwenye Nyumba tu. Sina uhakika kama sinema ni mali ya game city.
 
Asante kwa taarifa yako ila ingependeza kama ungesema ni bidhaa gani wewe umenunua ukakuta mbovu ikawa kama mfano kuliko kutoa taarifa ya ujumla kuwa bidhaa nimbovu
 
Mkuu kwenye site yako ya kupima kama umependana kweli na mpenzi wako kwanini umeweka option tatu? inamaana umehalarisha watu kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja. Ngoja nikufungulie thread sehemu wewe.

Lol

Sijahararisha ufisadi kwenye mapenzi mkuu.

Kumzimika mtu na kufanyia kazi huo mzimiko wako ni vitu viwili tofauti.

Ukikataa kwamba hata unapokuwa na mpenzi wako wa dhati kunakuwaga na wengine wanaokuvutia, basi utakuwa unahararisha unafki.

Tatizo ni pare unapovutiwa halafu unaammua ku-take action wakati tayali unawako.
 
taja bidhaa zilizo na matatizo, kwani kariakoo na samora hazipo?!! kama ni chakula na madawa then tujue! kwani lazima TFDA watusaidie.....jamani!! cant you do anything? hauwezi kuinunua na kuwashitaki? or go public? kuna magazeti na redio kibao, najua mtandao ni watu wachache wanao-access.
 
Kwa kweli walatini waliwahi kusema caveat emptor -buyer beware.tunapaswa kuwa na macho mia moja tunaponunua ilhali muuzaji anahitaji jicho moja kuhakiki fedha(huu ni msemo maarufu nadhani ujerumani)wandugu tuwe makini tudai warranty tusitupe receipt zenye warranty. Hii itapunguza kero.upande mwingine kuna taasisi zenye kudhibiti viwango,kama tbs lakini uwezo na umahiri wa watuaalamu wetu unatia shaka.basi ukiathirika isiwe siri yako.rafiki yangu uwe mteja mzuri -complain and complain and publish ur complaints!baadaye itakuwa caveat vendor-let the seller beware kwa maana ya kuwa ama abadilishe viwango ama awe mufilisi!samahani kwa swahienglish, lugha zote mbili zinanitatiza!
 
Mlimani city [game] ni sehemu ya kisasa kabisa 'KUUZA VITU VIBOVU' haibu kubwa wahusika wako wapi? RUSHWA I wish I were President naunda tume ikithibitika NAIFUNGA.
 
Lol

Sijahararisha ufisadi kwenye mapenzi mkuu.

Kumzimika mtu na kufanyia kazi huo mzimiko wako ni vitu viwili tofauti.

Ukikataa kwamba hata unapokuwa na mpenzi wako wa dhati kunakuwaga na wengine wanaokuvutia, basi utakuwa unahararisha unafki.

Tatizo ni pare unapovutiwa halafu unaammua ku-take action wakati tayali unawako.


Wewe mwenzetu kiswahili kwako ni lugha ya ngapi? Nashangaa ndani ya hiyo blog yako kuna nini hata kabla sijakiona kilichomo!
 
Game wana bidhaa za aina mbalimbali, from low, good, and perhaps high quality.
Kuna saa za mkononi pale za shilingi elfu 10, ila pia zipo za laki 150, n.k; zote kwenye shelf moja.

Wana marketing tactics zinazoweza kukutia hasira, ila ni fursa nzuri kwangu (nimegundua hilo sasa) kujifunza kuhusu sales, marketing and customers behavior.
 
Back
Top Bottom