Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,035
- 144,387
Kwa wanaoifahamu Dodoma, bila shaka watakuwa wanaelewa eneo hilo la Jeshi ambalo ni pori kubwa na sasa linageuka pori katika ya Jiji la Dodoma baada ya mji huu kuendelezwa kama Makao Makuu ya Nchi.
Kwa sasa, eneo hilo la Jeshi, linakuwa pori linalotenganisha makazi ya watu baada ya viwanja kupimwa kuzunguka eneo hili na pia linatenganisha eneo ambalo uwanja mkubwa wa mpira umepanga kujengwa.
Iwapo huo uwanja utajengwa, na watu wakaendeleza viwanja vilivyo jirani/ vinavyozunguka pori hili, basi hili pori linakwenda kuharibu madhara ya mji huu wa Dodoma .
Tukumbuke ni katika eneo hilo la jirani na hili pori, mji wa serikali ndio unaendelezwa mita chache kutoka yale magorofa ya Jeshi pale Ihumwa na ukienda mbele kilomita chache unasogelea iipo Ikulu ya Chamwino (Ukanda mmoja).
Kwahiyo huko baadae, mtu utakapokuwa unaingia katika jijil la Dodoma kutokea Morogoro/Dar-es-Salaam, utaanza kukutana na nyumba au majumba mazuri ya makazi ya watu na majumba ya serikali kisha unakutana na pori kubwa ambalo ni eneo la Jeshi halafu mita chache unakutana na uwanja mkubwa na wa kisasa wa mpira(iwapo utajengwa).Sasa vita picha ya huo muonekano wa pori katika hayo mazingira.
Binafsi nashauri Jeshi wakabidhi hilo eneo kwa serikali kwa maana ya Manispaa ya Dodoma ili eneo hilo libadilishiwe matumizi na Jeshi litengewe eneo lingine ambalo litakuwa mbali na makazi ya watu. Faida nyingine ya kuhamisha eneo hili la Jeshi mbali na makazi ya watu itakuwa ni kuondoa hatari ya watu kukaa karibu na makambi/maeneo ya Jeshi (tukumbuke mabomu ya Mbagala na athari zake).
Kwa mtazamo wangu, matumizi bora kwa eneo hili itakuwa ni kupima viwanja kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya watu au kutenga eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa majumba ya kibiashara kama vile shopping malls,n.k.Pia sehemu ya eneo hilo wanaweza kupewa National Housing wajenge magorofa na baadae wayapangishe au wayauze.
Sioni logic ya kuzuia wananchi kulima mazao marefu kama mahindi katika ya miji/majiji, halafu tukaruhusu mapori/vichaka katika ya Jiji kisa tu malori hayo yanamilikiwa na Jeshi unless Jeshi litaendeleza hayo maeneo na si vinginevyo.