Elimu ya Uzazi wa Mpango bado ni mtihani mgumu kwa Watanzania (World Contraception Day)

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kupata Mtoto ni kitu kizuri sana na binadamu wengi wanaishi wakiwa na ndoto hiyo, lakini ni vizuri kiumbe huyo akija wakati muafaka.

Ujio wa mimba wakati huo ukiwa na mtoto mwingine mchanga au katika mazingira ambayo hujajipanga kiuchumi kuhudumia ujio mpya huwa ni mtihani kiafya na kiuchumi pia.
contraceptio2884-1.jpg

Ndio maana kuna kitu kinaitwa Uzazi wa Mpango, hii inahusu walio kwenye ndoa, wasio kwenye ndoa, walioanza kuzaa na ambao bado hawajaanza.

Kujua na kupanga lini unatarajia kupata mtoto hilo ni jambo muhimu sana, ndio maana kila ifikapo Septemba 26 kila mwaka huwa kunakuwa na maadhimisho ya Siku ya Uzazi wa Mpango Duniani ili kuamsha ‘awareness’.

Siku ya Uzazi wa Mpango au World Contraception Day lengo lake ni kuleta mkazo wa kuamua kwa uhuru na kuwajibika kuhusu idadi na nafasi ya watoto wao.

Mashirika yasiyo ya kiserikali, ya serikali, sekta ya kibinafsi, vyombo vya habari, na watu binafsi hukusanyika ili kuadhimisha siku hiyo. Maadhimisho hayo yanatoa fursa nzuri ya kutetea umuhimu wa upatikanaji wa uzazi wa mpango.

download.jpg
Uzazi wa Mpango ni Nini?
Uzazi wa mpango ni maamuzi ya hiari ya wakati gani wa kupata mtoto, idadi, muda wa kupishana, nah ii inawahusu wenza wote japokuwa Wanawake ndio ambao huwa wanaachiwa mzi huo

Kuna njia nyingi za uzazi wa mpango baadhi ni; njia ya kitanzi, njia ya kudumu (kufunga kizazi), Kalenda, vidonge, Condom, sindano, vipandikizi (kijiti) na kitanzi.


JAMII INA UFAHAMU KUHUSU UZAZI WA MPANGO?

Michael, mkazi wa Mpunguzi - Dodoma
Anasema: “Elimu ya uzazi wa mpango ukweli ni kuwa watu wengi naweza kusema hatuna, hiyo imesababisha kuwe na matukio mengi ya utoaji mimba mitaani.

“Stori kama hizo zipo tunazisikia kila mara, japokuwa Serikali inazuia suala hilo la utoaji mimba lakini kwa kuwa mambo yanasikika kutokea mitaani inamaanisha watu hawafuati uzazi wa mpango.

“Mimi mwenyewe nina watoto lakini huwa naenda ile mara moja tu na mke wangu hospitali, kwa ajili ya kuandikishwa baada ya hapo huwa sifuatilii hadi anapojifungua, hata lile darasa ambalo huwa tunapewa nikienda naye huwa silitilii maanani kwa kuwa lengo langu siyo hilo.”

Happiness Mwinami, mkazi wa Matumbulu - Dodoma
“Mimi situmii hivyo vitu vya masuala ya uzazi wa mpango, wakati najifungua sikupata hiyo elimu, lakini kwa sasa nasikia wanatoa.

“Nikitaka kuzaa tena nadhani naweza kuipata lakini kwa sasa situmii na nina binti ambaye yupo kidato cha nne, sijawahi kukaa naye na kumwambia kuhusu hayo masuala

“Sitaki hata ayajue hayo masuala ya uzazi wa mpango, muhimu asijiingize tu kwenye mausiano, na aogope wanaume.

Hassan Mgaya, Ukonga – Dar es Salaaam
“Mimi nina mtoto mmoja sina elimu sana kuhusu uzazi wa mpango lakini nashauri kwa faida ya baadaye, Wizara ya Afya itoe elimu kwa umma hasa vijana kuanzia ngazi ya Shuleni wajue umuhimu wa Afya ya Uzazi ili wasiwe kama kina sisi.

“Mfano mimi hapa ninachojua mimba ikipatikana tu, tutaendelea kulea japokuwa mtoto wangu bado ni mdogo.”

Aisha Jumanne, Vingunguti – Dar es Salaam
“Mimi nina watoto watatu, sikufutilia uzazi wa mpango kutokana na mazingira yaliyokuwa yamenizungumza, nilimpa mtoto wangu wa kwanza kabla sijaolewa, iitokea tu.

“Wa pili na watatu wamefuatana nilikuwa nimeshaolewa tayari lakini sikujua kuhusu uzazi wa mpango ndio maana wakafuatana, ila nilisemwa sana na mauguzi, sasa hivi nimeshapata elimu nataka wanangu wapishane kwa muda kwanza.”
5a9e69f662cd483290870.jpg

MWANDISHI: JOHN HARAMBA
 
Back
Top Bottom