Uelewa wa masuala ya Afya ya Uzazi watajwa kuwa sababu ya Wanawake kukumbana na changamoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mkurugenzi wa Huduma za Afya kutoka Taasisi ya Marie Stopes Tanzania, Dr. Geofrey Sigalla amesema Wanawake wamekuwa waathirika wa uamuzi wanaofanyiwa kwenye suala la huduma za Afya ya Uzazi.

Ameyasema hayo leo Machi 8, 2024 katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo Taasisi ya Marie Stopes imeiadhimisha kwa kuwakutanisha Wadau mbalimbali kujadili mchango wao katika masuala huduma ya Afya ya Uzazi.
WhatsApp Image 2024-03-08 at 18.56.04_b5ebf177.jpg

Dr. Geofrey Sigalla
WhatsApp Image 2024-03-08 at 18.56.04_ac7d4971.jpg

Ambapo amesema takwimu za kidunia zinaonesha Wanawake ambavyo wamekuwa wakifanyiwa uamuzi kwenye masuala ya afya ya uzazi zao.

"Inaonesha kwamba Duniani nusu ya Wanawake hawana uwezo wa kufanya maamuzi yao binafsi kuhusu Afya yao ya Uzazi," amesema Dr. Geofrey.

Ameeleza Wanawake uamuzi wao umekuwa ukitegemea ruhusa za wazazi wao au wenza wao jambo ambalo ni kikwazo. Amedai kati ya sababu ambayo imekuwa ikichangia hali hiyo ni tamaduni na desturi zisizompa nguvu ya maamuzi Mwanamke.

Ameongeza suala la uelewa hafifu wa masuala ya Afya ya Uzazi pia ni sehemu ya changamoto ambayo uchangia baadhi ya Wanawake uamuzi wao kushikiliwa na baadhi ya watu.

"Huu sio usawa mara nyingi tunaweza kusema kesho yao katika masuala ya afya haipo mikononi mwao, ipo mikononi mwetu tunahitaji kuwawezesha Wanawake kufanya maamuzi," amesema Dr. Geofrey.

Pia kwa upande wa Mkurugenzi wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Tike Mwambikile ambaye alikuwa sehemu ya wachangiji wakuu mjadala amesema kuwa kukosekana kwa Sheria rasmi inayojielekeza kwenye masuala ya afya ya uzazi ni changamoto.
WhatsApp Image 2024-03-08 at 18.56.04_024efa5f.jpg

Tike Mwambikile
WhatsApp Image 2024-03-08 at 18.56.03_23574dd8.jpg
"Tunaongelea changamoto ya kutokuwa na Sheria inayoongelea masuala ya afya ya uzazi kwa ujumla wake na ndio maana tunaposherekea siku ya Wanawake nichukue fursa hii kuiomba Serikali na wadau mbalimbali wanahusisha masuala ya Afya ya Uzazi kuja na mipango mahususi ya kwangalia hili eneo.

“Usipokuwa na wananchi wenye afya njema na usipokuwa na Wanawake kama tunavyojua maendeleo ya Nchi nyingi sana nyuma ya pazia Mwanamke anahusika sana," amesema Tike Mwambikile.

Aidha, ametoa rai suala hilo ni muhimu lichukuliwe kwa uzito ili kuona namna bora ambayo inaweza ikawezesha kuja na mkakati utakowezesha kutengeza Sheria inayohusu masuala ya afya ya uzazi ili hasa kuweza kumlinda Mwanamke asiweze kuishi kwa wasimamizi anapokutana na mazingira mbalimbali

Upande wa Sesilia Shirima kutoka Taasisi ya YAI, amesema kumekuwepo na changamoto ya elimu ya uelewa wa masuala ya Afya ya Uzazi kwenye jamii, huku akitaja changamoto za kisheria pamoja mila kuandamizi kama kikwazo cha kupiga hatua kwenye masuala ya Afya ya Uzazi.

Naye, Ritha Chuwa kutoka Marie Stopes amesema ili jamii iendelee kwenye masuala mbalimbali kuwekeza kwa Mwanamke hakuepukiki, ambapo amesema suala la afya ya uzazi ni jambo ambalo linatakiwa kupewa nguvu katika uwekezaji huo ili kuepusha changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikimkumba Mwanamke.

Sanjali na hayo baadhi ya wachangiji wa mjadala huo ambao umewahusisha baadhi ya wanahabari, wamedai kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa ripoti na takwimu mbalimbali zinazohusu masuala ya afya ya uzazi ambazo zinaweza kusaidia katika kuelimisha umma.

Akitolea maelezo suala hilo lililoibuliwa na mwanahabari Tike Mwambikile amesema wadau wanatakiwa kulibeba suala hilo kwa uzito ikiwemo kuweka ripoti na tafiti mbalimbali mtandaoni ili kusaidia wanahabari pamoja na kushawishi mamlaka kuchua hatua za haraka kulingana na taarifa husika.

Wadau hao kwa pamoja wametoka na maazimio mbalimbali yanayoweza kuongeza uwajibikaji kwenye masuala ya afya ya uzazi, kati ya maazimio hayo ni kujidhatiti kuendelea kutoa Elimu ya Afya Uzazi kwa kutumia uwasilishaji unaoeleweka haraka.

Wanahabari kuandaa habari zenye tija kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi, kuchapisha taarifa na ripoti mbalimbali kwa ajili ya kuonesha ukubwa wa tatizo, kuendeleza mashirikiano na wadau wengine ili kupunguza ukubwa wa changamoto za Afya ya Uazi.
 
Back
Top Bottom