Mtaalam wa Afya: Maendeleo ya Kupanga Uzazi yanaendana na maendeleo ya Uchumi binafsi na wa Taifa

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Mratibu wa Uzazi wa Mpango kutoka Wizara ya Afya, Zuhura Mbuguni ameeleza kuwa jamii inazapozingatia Afya ya Uzazi wa Mpango ni rahisi pia kusaidia ukuaji wa Maendeleo ya Uchumi wa mtu binafsi na Taifa kwa jumla.

Amesema “Watanzania tunatakiwa kuunganisha maendeleo ya Kiuchumi au ya Nchi na Uzazi wa Mpango kwa kuwa vitu hivyo vinategemeana kwa sababu ukuaji wa idadi ya watu unatakiwa kuendana na ukuaji wa Uchumi pia.

“Kama tutafuata Kanuni za Kiafya ‘automatically’ kutakuwa na mtiririko mzuri wa ukuaji wa maendeleo ya mtu na jamii kwa jumla.”

Ameeleza kuwa taratibu za kiafya kitaalam zinaonesha baada ya Mwanamke kufikisha umri wa miaka 35 kunakuwa na hatari nyingi zinazoongezeka katika masuala ya uzazi.

Amefafanua kuwa “Kipindi kizuri cha uzazi ni kuanzia umri wa miaka 20 hadi 35 lakini simaanishi kuwa mtu hawezi kuzaa baada ya umri huo, lakini ni vigezo hatarishi kuongezeka.”

Akitaja vigezo hatarishi vya kujifungua baada ya Mwanamke kutimiza umri wa miaka 35 ni kujifungua kabla ya wakati, kupta Kifafa cha mimba, kutoka damu nyingi wakati wa kujifungua au kujifungua mtoto mfu.

Njia ya uzazi wa mpango
“Njia ya asili ambayo imekuwa ikitumiwa na wazee wengi ni kutengana kwa muda, lakini kwa sasa kumuacha mwenza wako kusema unaenda kulea ni hatarishi kwa kuwa huwezi jua unamuachaje mwenza wako huku nyuma,” amesema Zuhura na kuongeza:

“Njia nyingine ya asili ni kunyonyesha, hii inaweza kutumia miezi sita ya mwanzo ambapo mama mtu ananyonyesha mtoto wake kila baada ya saa mbili na iwe ni wakati ambao mzunguko wake wa hedhi haujarejea.

“Kitaalam mtoto anaponyonya kwa wingi na kila mara anachangia kuzalisha homoni moja ambayo inazuia kupevuka kwa yai, hiyi ni njia ya asilia ambayo ilitumiwa na wazee wengi.

“Kwa sasa kuifanya hivyo ni ngumu kwa kuwa Wamama wengi wanakuwa na pilika nyingi hivyo kukosa muda mzuri wa kunyonyesha watoto wao inavyotajiwa.”

Ameongeza kuwa kitaalam inaonesha mimba nne za kwanza kwa Mama zinakuwa katika mazingira salama kuliko zile ambazo zinapatikana baada ya hapo.
 
Back
Top Bottom