Ushauri: Aliwahi kutumia dawa za uzazi wa mpango sasa anapata ugumu kushika mimba. Anawezaje kupona tatizo hili? Nitafute mtoto kwingine?

Ntemii

JF-Expert Member
May 25, 2022
290
525
Habari wana MMU, natumai muwazima ndani ya jukwaa letu pendwa.

Mimi ni kijana wa makamo niliye ndani ya ndoa sasa yapata mwaka wa tatu, na tatizo linalonikabili ndani ya ndoa yangu, nilikutana na binti mrembo ambaye kusema ukweli nilipenda sana na kuvutiwa naye hadi kufanya maamuzi ya kufunga ndoa ya kanisani.

Mwanzoni mwa uchumba binti huyu ambaye ni mke wangu kwa sasa alitumia sindano za kuzuia mimba kwa muda wa miezi sita maana wakati huo alikuwa yupo masomoni chuoni. Nilipogundua nilipiga marufuku asiendelee kuchoma sindano hizo, aliacha na tukaendelea na mahusiano hadi ndoa.

Baada ya kumaliza tu tukafunga ndoa, sasa yapata miaka mitatu mke wangu hashiki mimba ana unene uliopitiliza, anaweza kaa hata miezi mitano hajaingia hedhi, anakiingia inaweza kaa hadi mwezi inatoka na inatoka mabonge mabonge, mwaka jana alishika mimba nayo ilitoka ndani ya mwezi mmoja, hadi sasa bado natafuta mtoto naye ila bado changamoto zake hazijakaa sawa.

Tumejaribu kwenda hospitali mbalimbali kubwa hapa mjini DSM tuaambiwa kuwa ni hormonal imbalance kwa sababau ya matumizi ya sindano za kupanga uzazi hivyo tukapewa dawa COC za miezi mitatu na kuambiwa tuendelea kuvumulia atatengamaa ila mpaka sasa bado.

Mimi wakati wa ujana nilifanikiwa kupata mtoto, ambaye ni kiliwazi, ndio faraja yangu kubwa kwa sasa, ingawa bado nahitaji sana watoto ndani ya ndoa yangu ukizingatia huyu mwanamke tumetoka naye mbali sana na nampenda, ila likija suala la uzao najihisi kukata tamaa na kuwaza kutafuta mwanamke mwengine anitafutie uzao.

Naombeni ushauri nifanyeje na pia msaada ili kuweza tibu tatizo la mke wangu, nitashukuru sana.🙏

Maamuzi ninayotaka kuchukua ni either kumuacha kabisa na kuoa mwanamke mwingine au kuendelea naye huku nikitafuta mtoto kwingine, maana umri unaenda na mimi siwezi kuendelea kuvumilia.

NB: Mabinti kama mnampango wa kujenga familia na kuzaa watoto msitumie madawa ya panga uzazi kilio mnakileta kwenye ndoa.
 
Kile kiapo ulicho apa mbele ya padre au pastor unakikumbuka "Tutavumiliana katika shida na raha" huo ndo muda wa kubeba msalaba wako.

Kingine mwambia mkeo aache kula vyakula vya mafuta mengi,maana nalo hilo unaliona ni kero sababu Kawa mnene sana.

Kama alishika Mimba na ikahariba basi atashika nyingine kuwa na subila tu mkuu.Pole kwa kipindi hiki kigumu katika ndoa y'ako.
 
Wewe mwenyewe umeshapima na kuonekana kuwa uko sawa unaweza kutungisha mimba? Maana inaweza kuwa wewe pia una tatizo na hata huyo mtoto wa ujanani ukawa umebambikiwa; au kuna tatizo limekupata huku ukubwani. Chunguza kwanza afya yako ya uzazi ili uwe na uhakika wa asilimia 100 kuwa mwenye tatizo ni mkeo na siyo wewe!

➡️➡️➡️ Na huyo mkeo sasa. Alikuwa anatumia dawa za kuzuia mimba wakati uko naye hamjaoana au kabla yako? Anapanga uzazi kabla ya ndoa? Au ni wale waliokuwa wameolewa ndoa bubu huko vyuoni au alikuwa anajiuza? 😳
 
Kile kiapo ulicho apa mbele ya padre au pastor unakikumbuka "Tutavumiliana katika shida na raha" huo ndo muda wa kubeba msalaba wako.

Kingine mwambia mkeo aache kula vyakula vya mafuta mengi,maana nalo hilo unaliona ni kero sababu Kawa mnene sana.

Kama alishika Mimba na ikahariba basi atashika nyingine kuwa na subila tu mkuu.Pole kwa kipindi hiki kigumu katika ndoa y'ako.
barikiwa sana,kiuhalisia inaumiza sana
 
Mabinti nao wana haraka siku hizi, mtu hata hujaolewa, hujazaa unatumia uzazi wa mpango! Madhara yake ndo hayo mtu kuolewa mumeo anakuchoka mapema ingawa miaka 3 ya ndoa ni miduchu mnooo.....sema nini mkuu Ntemii mvumilie mkeo atapata tu mtoto japo alijiharibu kizazi chake sjui na hormones zake akiwa hajui madhara yake hayo makitu yanasumbua mtu anaacha kutumia hata miaka 10 lakini mimba holaaa
 
Wewe mwenyewe umeshapima na kuonekana kuwa uko sawa unaweza kutungisha mimba? Maana inaweza kuwa wewe pia una tatizo na hata huyo mtoto wa ujanani ukawa umebambikiwa; au kuna tatizo limekupata huku ukubwani. Chunguza kwanza afya yako ya uzazi ili uwe na uhakika wa asilimia 100 kuwa mwenye tatizo ni mkeo na siyo wewe!
Kabisa mkuu ila kwa jinsi alivyoelezea hali ya mkewe ni wazi kuwa izo contraceptive alizotumia zimemletea madhara, maana yale kuna watu wanatumia wanakaa miaka zaidi ya 10 ndo anapata katoto ka uzeeni
 
mkuu ni kuhakikishie huyo dogo ukimuona huulizi mara mbili,pia afya ya uzazi upande wangu nilishafanya haikuonekana tatizo,licha ya hivyo changamoto za mwanamke ziko wazi kabisa wala hakuna shaka na uwezo wake kukamata mimba katika hali alionayo sasa,mana anaweza kaa miezi hata sita hajaingia hedhi,mazingira kama hayo unaona kabisa sio rafiki.
 
Sema haya masindano na dawa za kupanga uzazi ni changamoto sana, nawafahamu zaidi ya mabinti watatu ambao nishakuwa nao kwenye mahusiano hao wanaweza kukaa hata miezi mitatu bila kuona siku zao, kiufupi mfumo mzima wa hedhi umevurugika, nawaza kama ikifikia muda wa kuzaa itakuwaje kuwaje.
 
Mabinti nao wana haraka siku hizi, mtu hata hujaolewa, hujazaa unatumia uzazi wa mpango! Madhara yake ndo hayo mtu kuolewa mumeo anakuchoka mapema ingawa miaka 3 ya ndoa ni miduchu mnooo.....sema nini mkuu Ntemii mvumilie mkeo atapata tu mtoto japo alijiharibu kizazi chake sjui na hormones zake akiwa hajui madhara yake hayo makitu yanasumbua mtu anaacha kutumia hata miaka 10 lakini mimba holaaa
changamoto sana,natamani sana kuvumilia ila najiuliza huu uvumilivu hadi lini ilihali mimi umri unakwenda na nisingetamani uzeeni kuzaa na kuhangaika na malezi.
 
Kabisa mkuu ila kwa jinsi alivyoelezea hali ya mkewe ni wazi kuwa izo contraceptive alizotumia zimemletea madhara, maana yale kuna watu wanatumia wanakaa miaka zaidi ya 10 ndo anapata katoto ka uzeeni
Nikweli kabisa mwanamke aliyesawa anajuikana tu hasa katika mzunguko wake huwa hausumbui,huyu wangu naweza kaa hata miezi 6 hajaona siku zake,ama anaweza ingia mara mbili ndani ya mwezi mmoja,ama aka bleed hata wiki 3 mfululizo tena mbonge mabonge.
 
Back
Top Bottom