Je, bangi husababisha matatizo ya uzazi kwa wanaume?

lord atkin

Senior Member
Sep 30, 2018
197
683
Salaam,

Ninaomba kufahamu hili kutoka kwa wataalam wa afya waliomo humu ndani. Nina shemeji yangu mmoja hivi amekuwa na tatizo la kupata mtoto kwa miaka kadhaa sasa. Ana mtoto mmoja lakini ameshindwa kupata mtoto wa pili kwa miaka mingi sana. Mtoto wake wa kwanza ana miaka 20 sasa na hana mdogo wake. Dada yangu amehangaika hospital zote Kila akipimwa anaambiwa yeye Hana tatizo lolote hivyo wamekuwa wakishauri ampeleke na mume wake ili wapimwe wote. Kila akimwambia mumewe kuhusu kwenda hospitali anakataa.

Mwanzo alikuwa akisema mkewe ndiyo mwenye shida ya uzazi anajaza choo. Alipata mchepuko kwa Siri akampangishia ili amzalie alidumu naye miaka mitatu bila mafanikio ya kupata mimba akaamua abaki tu njia kuu.

Shemeji yangu huyu anavuta sana bangi na sigara, anavuta mpaka macho yanakuwa mekundu na ni kwa miaka mingi kabla hata hajaoana na dada yangu. Sasa hivi karibuni nimekuwa nikisikia uvumi kwamba tatizo la uzazi kwa mwanaume linaweza kusababishwa na uvutaji wa bangi.

Ninahitaji kujua iwapo hili ni la kweli na kama Kuna tiba kwa mwanaume ambaye ana matatizo ya uzazi yaliyosababishwa na uvutaji bangi.
 
Bob Marley left 11 acknowledged children from 7 women…na mmoja wa role model wa wavuta msuba si ni Marley ? Au nasema uongo masta. Japokuwa unalosema linaweza likawa na ukweli maana birthrate ya jamaica ni ndogo pia
 
Sigara ndio changamoto...tulienda regency Hosp mwaka Fulani nyuma,baada suala la kupata mtoto wa pili kuwa issue, kitu cha kwanza Doc aliniuliza kama navuta sigara!
 
Back
Top Bottom