Mkuu Kamundu, heshima mbele nia ya mada yako ni njema sana, isipokuwa tu una ka-bias flani hivi against baadhi ya wabongo walioko US, na pia hujaona mengi sana duniani, lakini ninaheshimu kuwa nia yako bado ilikuwa njema, But:-
1. Ni lazima kuelewa sababu kwanza iliyomfanya mtu kwenda US in the first place, halafu pia uwezo wa yule mtu kufikiri, exposure aliyonayo kimaisha, anatokea maisha gani bongo, maana elimu sio kila kitu, nikiwa na maana kuwa Us kuna wa-Mexico, wanauza maua tu njiani na wanatuma hela kwao kila siku na wana maisha kuliko Blacks wengi wanaolipwa mishahara mikubwa!
2. Si kweli maneno uliyosema as a general ststement, isipokuwa kuna some isolations ishus, lakini most of the times wa kulaumiwa ni wabongo wenyewe kwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu maisha, mazingara walikotoka na mazingara waliyomo sasa, yaani ya US, wengi wanaenda kule na mawazo kuwa bado wako bongo off course maisha yatakuwa ni magumu hata uwe na elimu, hivi unajua ni wamarekani wangapi wenye degree na wanaendesha tax na wana maisha bora na ya uhakika? West Africans wako kibao, wanaendesha tax na wana elimu nzito, lakini ukiongea nao watakwambia kuwa the best decision they ever made katika maisha yao ilikuwa kusoma na kufanya kazi wanayo fanya walipo yaani kuendesha tax.
3. Wa-Tanzania tunasumbuliwa sana na kasumba ya waingereza, ya kufikiri kuwa ni lazima uvae suti kwenda kazini ili uwe na maisha mazuri, ukweli ni kwamba US kuna ubaguzi mkubwa sana, kazi za elimu na malipo makubwa zimetengwa kwa ajili ya wazungu kwanza, halafu weusi wachache kwa ajili tu ya ku-balance na kuwa politically correct on corporate side, lakini hizi kazi sio kwa wageni, hizi ni facts ambazo ni lazima uzifahamu kwa undani kabla hujaenda US kuishi, ukiwa umesoma au hukusoma it does not matter!
4. Kabla ya ku-make a final decision ya kwenda kuishi US, kama inawezekana jaribu kutembelea na nchi zingine kwanza hata Kenya tu ukasafishe macho, sio unatoka Kigoma na Bukoba, pruuuuu stop ya kwanza US, hata Dar'Salaama unapita tu kwenda airport, wengine wanapandia ndege Kampala, I mean unategmea nini huko Us kila kitu kitakuwa maajabu tu, yes ninasema hivyo kwa sababu nimeishi US 20 years, tena yote New York kwenye mambo yote kwa hiyo siongei hadithi ila ninaongea reality, wabongo huenda huko macho juu mno, wengine hata kazi hawajawahi kufanya inawachukua at least miaka mwiwili ya kwanza kutulia chini na kuanza kufikiri maan muda wote huo uliopita mnaona jamaa yupo tu kumbe bado analewa na ulaya, kutoka Mlimani na degree peke yake hakuwezi kukufanya ukaishi "unavyotaka" au "Ulivyotegemea" US,
5. Binafsi kabla sijaamua kwenda US, nilikuwa nimeshatinga melini in the process ya kazi hiyo nilipata bahati ya kutembela almost dunia nzima, kwa hiyo I had an-idea ni nchi gani inafaa kwenda kuishi kwa ajili ya kutafuta maisha na yanawezekana, guys hakuna nchi kama USA, that is it hata kama huna papers, bado maisha yake sio sawa na nchi yoyote duniani, yes I said nitajie nchi unayodhani ina maisha mazuri kwa mbongo hata kwa asiyekuwa na makaratasi, na elimu kama USA? Kama ukishindwa kuyaweza maisha US basi wewe huwezi mahali popote, tena ukirudi bongo utakufa mapema sana, lakini msilaumu nchi wala maisha!
6. Wabongo muache kudanganyana kuhusu USA na ulaya kwa ujumla, nimewaona wabongo wengi sana kule US, wengi wao hata ile idea ya kwa nini wameeenda kule hawana kabisa, I mean absolutely no clue, wavivu, wazembe, at one time mimi nimewakaribisha jamaa ndio kwanza wameingia toka bongo, ninafanya kazi masaa 16 kwa siku kuanzia J'matatu mpaka Jumapili, Ijumaa na jumamosi jioni ninapiga disco kwenye club, nikitoka pale ninaingia kazini moja kwa moja, wao wanajimwaga tu mangoma na kufanya kazi masaa manane tena madukani, na kunishangaa mimi kuwa ninajitesa sana, ebo! wewe ndio kwanza umeingia nchi ya watu huna lolote, ni lazima ukazane kwanza ili ujiweke sawa, baadaye ndio utatulia na kutafuta kazi unayoitaka, au ya shule, lakini lazima uwe na msingi mzito kujua kufanya kazi kwa bidiii, kwa sababu hata kama ukipata hiyo kazi ya elimu kama huna work ethics, ni bure, sasa yes maisha yatakuwa magumu sana huko majuu, maana kwanza utaridhika mapema na chochote unachopata badala ya kuhangaika,
7. Mabadiliko ya maisha hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, yanakuja kwa kuhangaika, ukifika kwanza unaaanzia chini hata kama umesoma, hiyo ni sheria ya kwanza ambayo watu wa West Africa wanaielewa sana kuhusu US, then pole pole unaaanza kujifunza mazingara, huku ukitafuta kusonga mbele, regardless ya makaratasi, ukiona mtu analilia makaratasi mapema ujue ni mviovu huyo, wakuu ngoja niwaambie ukweli wabongo niliowaona nilipokuwa US, waliokuja na kudai wanatafuta makaratasi kwanza, 80%, walishia kurudi bongo kwa kushindwa maisha, 10% waliishia jela kwa kujaribu kutafuta papers kwa nguvu, 5% waliyapata lakini hawakupata kazi walizoziomea, 5% waliishia kuwa deported,
lakini 99.9%, ya wale wabongo waliokwenda kuchapa kazi ili wajiondoleee umasikini wao ambao wanaujua wenyewe, walifanikiwa sio tu maisha mazuri, but in the process za kuhangaika waliishia hata kupata makaratasi, ambayo wengi wao yalijileta yenyewe kwa njia mbali mbali wao wakiwa wanahangaika na maisha, and that is exactly what I did, I can go on and on kuhusu wabongo na kutokuwa serious, kutoelewa, kutojishughulisha, halafu kulaumu tu majuu,
Naomba kwa sasa niishie hapa, hakuna nchi njema duniani kama USA, usome usisome it does not matter, lakini ni lazima uwe umekwenda for the right reasons, na uwe the right person, US na Ulaya, sio kwa kila mtu, halafu kama ulishindwa maisha bongo hata kidogo tu basi uwezekano wa kutofanikiwa majuu ni mkubwa sana, kama umekwama uliza wengine wakusaidie, tuache uvivu na uzembe wa kufikiri, mind is a terrible thing to waste maana popote utaishia kuchekesha tu, kabla huja-give up uliza kwanza acha kitu wa-giriki wanaita egoooooo(Ego) na pride zisizokuwa na msingi, be humble na kubali kuelimishwa, lakini usiruke tu na conclusion especially a sensitive kama hiii, kwa wale walioko bado hapa bongo wanataka kwenda huko ninawaambia kuwa huko US ni safi na hakuna noma yoyote!
Ahsante Wakuuu!