Hii mada ni nzuri sana, sijakaa Marekani zaidi ya watu wote waliotoa mada ila naweza kusema mategemeo ya watu waliokuwa wamekuja Marekani, wengi wamekumbana na ukweli ambao hawakuambiwa au kuonywa na ndugu zao wakati wanapanga safari yao ya kimaisha...
Kweli wimbi la massive migration ya vijana wa Tanzania limeanza mwaka 1992, na kuchukua kasi sana 1996 mpaka 2000...Tulipata vijana waliokuja hapa kwa njia tofauti, I-20 to F-1 visa za wanafunzi ambao ilikuwa ukiingia shule tu, unaomba Social Security namba, kwa wanaoishi US wanajua ndio kiini cha kupata kazi..
Miaka ya 1997-2001, vijana waliomaliza Form 4, hasa form 6 Tanzania wakaja kama Scout, wengine Summer camp, kutorokea mitaani na kutafuta ndugu jamaa na marafiki..hawa walipata shida kupata social security namba..wengine walitumia namba za marafiki kufanya kazi, shule ilikuwa ngumu labda kwa wachache wenye uwezo waliomba status ibadilishwe INS (wakati huo ilikuwa rahisi)wakafanikiwa..
Baada ya Sept 2001, Migration ya Vijana na ndugu zetu yakawa magumu na sheria hata za kupata social security namba zikawa ngumu sana, sheria nyingi za uhamiaji zilibadilika baada ya ugaidi wa Al-Queda Sept 11...Nakumbuka kuna miaka ilifuata hapo, Watanzania kadhaa waliingia Marekani kupitia mji wa Miami kama wacheza ngoma kikundi cha Ngoma ambacho chote kilitikitia mitaani katika majimbo mbalimbali kuanza maisha yao Marekani..
Kwa Mtazamo wangu, wengi walikimbia Tanzania miaka hiyo kwa sababu ya ugumu wa maisha ya Tanzania..lakini Ugumu wa Marekani unasababishwa na mambo matatu makuu, na moja dogo la niongeza
1.Elimu--Elimu ya Marekani, tofauti na watu wakitoka Tanzania, hufikiri ni rahisi, lakini inakuwa na Homework za kila siku, kwa hiyo discipline ya Kusoma na kujituma ni kubwa tofauti na kusomea mithihani nyumbani..Elimu ni Ghali na scholarship sio rahisi.Wengi huingia na kuacha, na hakuna atakayekukumbusha kurudi shule kama huna discpline
2.Upotevu wa Status: hili hutokea miaka au mwaka wa kwanza wa vijana wengi kuja Marekani..Baada ya kuacha shule au kutoroka hizo Summer camp, kwa ufupi, umeingia katika hili, hapo hauna Status na Mkataba uliopewa umevunjika, bila kupewa ukazi wa kudumu, inabidi urudi Tanzania kuomba visa upya na linanlotisha ni kujibu kwanini upewe wakati umekiuka mkataba wa kwanza..sasa utatuzi wa hili ni kitendawili ambacho kinawasumbua ndugu na wadogo zetu kwa muda mrefu, wengine hata miaka kumi bila ufumbuzi..hapa hulazimika aidha kuoa au kupata mdhamini wa kazi..Tatizo hapa ni information ambazo si sahihi, muda mwingine hupeleka watanzania kwenye Matatizo makubwa, hata kurudishwa nyumbani bila dhamira yao..Ndoa na Mmarekani inaweza kumpa mtu Green Card, lakini ndoa hizi zimepeleka watu kwenye kuanzisha familia bila matarajio, au matatizo mengine na waume na wake zao, au upotevu mkubwa wa pesa.
3. Credit--hili, labda sababu watanzania wengi hatupati,au hupata elimu ya utunzaji wa pesa wakiwa watu wazima..Hili somo ni muhimu kwa maisha ya Marekani..Ukishapata kazi au ukiwa tu na miaka 18, Mashirika ya Fedha na Mabenki yatajituma kukupa mkopo kwa chochote..Hapa wengine huishi maisha kimakosa au kimatumizi bila ufahamu wa matatizo ambayo hela za mikopo huweza kukufikisha na kujikuta na madeni mengi kuliko malipo ya kazi..Ukiweza kutunza huu uwezo wa udhamini (credit), maisha ya Marekani yatakuwa ni Mazuri.
4.Sherehe, Tafrija, Starehe na Party-- Utamaduni ambao umepungua nguvu miaka ya hivi karibuni wa Party za Mwezi tano jimbo la Ohio na Mwezi wa Tisa mji mkuu Washington, Dc, hivi sasa ziko Atlanta, New York, na Dallas wakati wa Sikukuu mbalimbali zilikuwa njia nzuri watanzania kukutana lakini nayo ilichangia vijana wengi ambao waliona ndio nafasi yao kujitutumua na kujikweza kuwa hali yao kiuchumi ni nzuri..ni sherehe ya siku tatu, kwa hiyo vijana wenye matatizo mbalimbali hukutana, sio wote, ila hukutana kutoka majimbo mbalimbali..Dhumuni ilikuwa ni ndugu jamaa na marafiki kukutana, lakini wengine waliamua kutumia hizi tafrija kujigamba, wengine mpaka ugomvi wa wanawake waliokuwa nao wakiwa Tanzania, hata miaka 5-7 iliyopita..zilipungua umaarufu sababu ya matukio kama hayo..Marekani ni kama Bara, hizi shughuli zilikuwa zinasaidia kukutanisha watu wanaoishi mbali kukutana kituo kimoja, kupunguza gharama.
In conclusion, Marekani bado ni Taifa lenye nguvu, na kuna watu, Watanzania wengi wamesoma na wanaishi vizuri, hawana matatizo niliyotaja juu ila hawapendi kujishirikisha na Watanzania sababu kama mambo ya ufisadi kila siku magazeti ya nyumbani, watanzania wa ughaibuni wana maneno, majungu hukatisha tamaa kaka zao kupewa ushauri..Mafunzo ya huku yanasaidia ila Nyumbani napo pameendelea..ushauri ni kujitahidi kupata angalau Elimu, Watanzania wa US huzidi wa Nyumbani kwa Lugha ya Kiingereza na hand-on experience, ambacho ni zawadi nzuri kwa mtu anayerudi ingawa wengi ni waoga sana kufanya uamuzi huo..Ila ushauri watanzania wakirudi wasishangae wenzao waliobaki Tanzania wakikuta wanamaendeleo zaidi yao baada ya kuachana miaka mingi toka kumaliza shule..sababu uamuzi wa kurudi nyumbani huwa ni jambo linatokea baadae sana kwa walioishi US..Ushauri wa Bure kwa ndugu zangu,Wasiliana na Nyumbani, soma magazeti mjue nyumbani kukoje na endeleza kwenu--Kijiji chako ni jukumu lako, sio la Serikali..Tunasema : Nyumbani Nyumbani..