Samvulachole,
Usiwadanganye ndugu zetu, japo ni kweli ulichosema lakini ukiingia kwenye social UK , jua umaskini umekukumba maisha na maisha. Ni ngumu mno kutoka kwenye maisha ya kukinga mkono mpaka baadaye ukafanikiwa.
Sawa tumia njia yoyote kupata makaratasi lakini jitahidi ku avoid social benefits maana zinalemaza mno. Hata USA ndio zimelemaza ndugu zetu wengi weusi kule.
Wengine tunachapa mabox yetu warehouse na mungu anasaidia hivyo hivyo.
True story..london wapo wabogo wamekaa UK miaka zaidi ya 15 wanakinga social benefits..wanaona haibu kurudi dar..shule waliacha sasa wamezaaa..they got nothing to show for it!! Jamani kama umekuja kusoma SOMA!! kama umekuja kufanya kazi na kutafuta maisha fanya hivyo lakini usisikilizie social benefits...its wot keep the poor poor..it creates a lazy class.. (chavs in the uk, blacks in the UK/USA etc...)
Lengo sio kuwasema vibaya bali ni kutoa mfano zaidi, kuna jamaa zangu wa visiwani ambao wapo huko UK baada ya kukimbia mapinduzi kisiwani. Hawa nao walitumbukia kwenye mfumo huu, hadi hii leo wameshindwa kuibuka. Mbaya zaidi hata watoto wao wametumbikia katika mfumo huu hivyo kuendelea kuishi katika mfumo huo, ambao unalegeza mbinu za kujituma katika kufanikisha maisha binafsi na ya kifamilia.
Kibunango,
Ulichosema ni kweli tupu. Ukiingia kwenye benefits unaishia kuishi kwenye council houses ambazo nyingi ziko maeneno ambayo yanakuwa mabaya. Matokeo yake hata huduma kama za shule zinakuwa mbaya, polisi hawaonekani hivyo hata crime inakuwa juu. Huduma za hospitali zinakuwa duni pia.
Mtoto anayezaliwa kwenye mazingira kama hayo ni ngumu sana kufanikiwa. Hata akiwa na uwezo bado anakosa motivation ambayo watoto wengine wanapata kwa kuona wazazi wao wanahangaika kila siku.
Akienda shuleni na kula chakula bila kulipa tayari ni mwanzo wa bulling kutoka kwa watoto wengine, hivyo hata kwenda shuleni kwenyewe kunaanza kuwa taabu.
Kama wageni tunataka kujikomboa kwenye hizi nchi za watu, njia ni moja tu, kuchapa kazi na kupanda taratibu kwenye ladder mpaka. Njia za mkato kama social benefits, zinakurudisha nyuma hatua tano.
Acheni kuwaongopea watu humu
kwanza ki statistic watu wa visiwani ndio wengi zaidi UK kuliko watu wa bara
na kwa taarifa yenu hawa ndio wanapeleka pesa zaidi nyumbani kuliko hao wanaojidaui wazalendo ambao ni wafanya kazi zaidi/wanafunzi
Mara ya mwisho nilikwenda kwa Dewji na aliniambia kuwa hawa jamaa waliojilipua wamekuwa blessing in disguisse kwani wanapeleka ma containers na saa zingine nusu ya meli ni ya vitu vya hawa jamaa kuanzia malori mpaka makontena ya bidhaa
Ndio wengi waliingia kwenye benefit lakini hawakukaa sana kama mnavyotaka kuwaongopea watu humu
wengi wao walipata British passports na wamekuwa economically active kuliko mnavyotaka kuwafanya na bila kusahau kuwa wamekuwa mobile kibiashara sana baada ya kupata pasi zao
Nendeni Kariakoo mkafanye uchunguzi mtaona maduka mengi kule na ma importers wengi kule ni watu wenye asili ya visiwani wenye British passports waliojilipua 1995
wanunuzi wa majumba kule kariakoo ni hawa wali waliojilipua
Kwa anaelewa benefit system ya UK ataelewa kuwa kupata income support ni hki la kila Mwingereza mwenye mtoto si lazima uwe uwe unemployed na mashaalah wengi wa hawa watu hawana haja ya IVF wanajaaliwa kupata watoto. Msisahau kuwa UK ni social democracy hivyo mambo hayo ni kawaida tuuu
Wanawake wa nyumbani mara nyingi hawana pesa za ma child minders lakini nchi hii hawa wanawake wanapesa pesa kujiendeleza kitaaluma kupitia projects mabali mbali
Mmezungumzia ma CHAV lakini mtu kuwa cha si lazima uwe kwenye benefit na hata David Bekhama kama mnataka tuingine kwenye definition ya u chav ni CHAV, the same applies to Rooney an Rio Ferdinand...bila kumsahau Sir Alan Sugar
Kutokana na cultureza nyumbani wanawake wengi kusema ukweli hawako economically active lakini second generation inabadilika kwa kiasi kikubwa
huu mjadala kuhusu watu waliojilipua umekuwa ukiendeshwa na watu ambao hawana zaidi ya VIVU tuu kwani waliowahi wakachukua advantage ya nafasi ndio hawa ambao wako active kiuchumi mnataka kuwapaka matope bila mpango wowote
Mara ya mwisho nilienda kutoa kontena langu Dar na naweza kukuambia kuwa majority ya waliokuwa pale kuprocess mambo ya kutoa mizigo yao pale ni hao waliojilipua na watu wa U, sikuona watu wa USA wanaosifiwa kuwa wamesoma na wameendelea zaidi
na kam mmendelea zaidi mbona mnakuja UK kuishi free rent wakati wa kusummer ? ndio its an open secret huwa mnakuja UK kufanya kazi kwa kutumia mjaina ya hawa hawa waliojilipua na NI zao?
acheni hii prejiduce mlionayo
that said najua waliojilipua kule Canada wengi wao maisha ni tofauti kutokana na serikali ya kule kuwalazimisha kusoma ili hali UK na Europe mambo ya kulazimishwa kusoma hayapo
leteni hoja nyingine lakini penye ukweli semeni