Educated TZ Immigrants in US in tough Situation

Watu wa Marekani wamefanikiwa sana John Mashaka maarufu kama Mwanakijiji ameweza kumiliki redio yake inaitwa KLH NEWS,website, podomatic, makochi meupe,ana suti nyeusi, ana posts zaidi ya elfu nane Jambo Forums,anaandika magazetini n.k
haya ni mafanikio makubwa sana.


Yesu WANGU!!!!!!!!!!!!!
 
mkuu kamundu, heshima mbele nia ya mada yako ni njema sana, isipokuwa tu una ka-bias flani hivi against baadhi ya wabongo walioko us, na pia hujaona mengi sana duniani, lakini ninaheshimu kuwa nia yako bado ilikuwa njema, but:-

1. Ni lazima kuelewa sababu kwanza iliyomfanya mtu kwenda us in the first place, halafu pia uwezo wa yule mtu kufikiri, exposure aliyonayo kimaisha, anatokea maisha gani bongo, maana elimu sio kila kitu, nikiwa na maana kuwa us kuna wa-mexico, wanauza maua tu njiani na wanatuma hela kwao kila siku na wana maisha kuliko blacks wengi wanaolipwa mishahara mikubwa!

2. Si kweli maneno uliyosema as a general ststement, isipokuwa kuna some isolations ishus, lakini most of the times wa kulaumiwa ni wabongo wenyewe kwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu maisha, mazingara walikotoka na mazingara waliyomo sasa, yaani ya us, wengi wanaenda kule na mawazo kuwa bado wako bongo off course maisha yatakuwa ni magumu hata uwe na elimu, hivi unajua ni wamarekani wangapi wenye degree na wanaendesha tax na wana maisha bora na ya uhakika? West africans wako kibao, wanaendesha tax na wana elimu nzito, lakini ukiongea nao watakwambia kuwa the best decision they ever made katika maisha yao ilikuwa kusoma na kufanya kazi wanayo fanya walipo yaani kuendesha tax.

3. Wa-tanzania tunasumbuliwa sana na kasumba ya waingereza, ya kufikiri kuwa ni lazima uvae suti kwenda kazini ili uwe na maisha mazuri, ukweli ni kwamba us kuna ubaguzi mkubwa sana, kazi za elimu na malipo makubwa zimetengwa kwa ajili ya wazungu kwanza, halafu weusi wachache kwa ajili tu ya ku-balance na kuwa politically correct on corporate side, lakini hizi kazi sio kwa wageni, hizi ni facts ambazo ni lazima uzifahamu kwa undani kabla hujaenda us kuishi, ukiwa umesoma au hukusoma it does not matter!

4. Kabla ya ku-make a final decision ya kwenda kuishi us, kama inawezekana jaribu kutembelea na nchi zingine kwanza hata kenya tu ukasafishe macho, sio unatoka kigoma na bukoba, pruuuuu stop ya kwanza us, hata dar'salaama unapita tu kwenda airport, wengine wanapandia ndege kampala, i mean unategmea nini huko us kila kitu kitakuwa maajabu tu, yes ninasema hivyo kwa sababu nimeishi us 20 years, tena yote new york kwenye mambo yote kwa hiyo siongei hadithi ila ninaongea reality, wabongo huenda huko macho juu mno, wengine hata kazi hawajawahi kufanya inawachukua at least miaka mwiwili ya kwanza kutulia chini na kuanza kufikiri maan muda wote huo uliopita mnaona jamaa yupo tu kumbe bado analewa na ulaya, kutoka mlimani na degree peke yake hakuwezi kukufanya ukaishi "unavyotaka" au "ulivyotegemea" us,

5. Binafsi kabla sijaamua kwenda us, nilikuwa nimeshatinga melini in the process ya kazi hiyo nilipata bahati ya kutembela almost dunia nzima, kwa hiyo i had an-idea ni nchi gani inafaa kwenda kuishi kwa ajili ya kutafuta maisha na yanawezekana, guys hakuna nchi kama usa, that is it hata kama huna papers, bado maisha yake sio sawa na nchi yoyote duniani, yes i said nitajie nchi unayodhani ina maisha mazuri kwa mbongo hata kwa asiyekuwa na makaratasi, na elimu kama usa? Kama ukishindwa kuyaweza maisha us basi wewe huwezi mahali popote, tena ukirudi bongo utakufa mapema sana, lakini msilaumu nchi wala maisha!

6. Wabongo muache kudanganyana kuhusu usa na ulaya kwa ujumla, nimewaona wabongo wengi sana kule us, wengi wao hata ile idea ya kwa nini wameeenda kule hawana kabisa, i mean absolutely no clue, wavivu, wazembe, at one time mimi nimewakaribisha jamaa ndio kwanza wameingia toka bongo, ninafanya kazi masaa 16 kwa siku kuanzia j'matatu mpaka jumapili, ijumaa na jumamosi jioni ninapiga disco kwenye club, nikitoka pale ninaingia kazini moja kwa moja, wao wanajimwaga tu mangoma na kufanya kazi masaa manane tena madukani, na kunishangaa mimi kuwa ninajitesa sana, ebo! Wewe ndio kwanza umeingia nchi ya watu huna lolote, ni lazima ukazane kwanza ili ujiweke sawa, baadaye ndio utatulia na kutafuta kazi unayoitaka, au ya shule, lakini lazima uwe na msingi mzito kujua kufanya kazi kwa bidiii, kwa sababu hata kama ukipata hiyo kazi ya elimu kama huna work ethics, ni bure, sasa yes maisha yatakuwa magumu sana huko majuu, maana kwanza utaridhika mapema na chochote unachopata badala ya kuhangaika,

7. Mabadiliko ya maisha hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, yanakuja kwa kuhangaika, ukifika kwanza unaaanzia chini hata kama umesoma, hiyo ni sheria ya kwanza ambayo watu wa west africa wanaielewa sana kuhusu us, then pole pole unaaanza kujifunza mazingara, huku ukitafuta kusonga mbele, regardless ya makaratasi, ukiona mtu analilia makaratasi mapema ujue ni mviovu huyo, wakuu ngoja niwaambie ukweli wabongo niliowaona nilipokuwa us, waliokuja na kudai wanatafuta makaratasi kwanza, 80%, walishia kurudi bongo kwa kushindwa maisha, 10% waliishia jela kwa kujaribu kutafuta papers kwa nguvu, 5% waliyapata lakini hawakupata kazi walizoziomea, 5% waliishia kuwa deported,

lakini 99.9%, ya wale wabongo waliokwenda kuchapa kazi ili wajiondoleee umasikini wao ambao wanaujua wenyewe, walifanikiwa sio tu maisha mazuri, but in the process za kuhangaika waliishia hata kupata makaratasi, ambayo wengi wao yalijileta yenyewe kwa njia mbali mbali wao wakiwa wanahangaika na maisha, and that is exactly what i did, i can go on and on kuhusu wabongo na kutokuwa serious, kutoelewa, kutojishughulisha, halafu kulaumu tu majuu.


naomba kwa sasa niishie hapa, hakuna nchi njema duniani kama usa, usome usisome it does not matter, lakini ni lazima uwe umekwenda for the right reasons, na uwe the right person, us na ulaya, sio kwa kila mtu, halafu kama ulishindwa maisha bongo hata kidogo tu basi uwezekano wa kutofanikiwa majuu ni mkubwa sana, kama umekwama uliza wengine wakusaidie, tuache uvivu na uzembe wa kufikiri, mind is a terrible thing to waste maana popote utaishia kuchekesha tu, kabla huja-give up uliza kwanza acha kitu wa-giriki wanaita egoooooo(ego) na pride zisizokuwa na msingi, be humble na kubali kuelimishwa, lakini usiruke tu na conclusion especially a sensitive kama hiii, kwa wale walioko bado hapa bongo wanataka kwenda huko ninawaambia kuwa huko us ni safi na hakuna noma yoyote!

Ahsante wakuuu!

FMES

This is a Masterpiece.
 
Simpo facts za maisha, Tanzania ama Marekani;

1) Usiusemee moyo - JD, utamkuta club ukadhani ame-frustrate kumbe ndio raha yake! kama wewe wafurahia kuwa na nyumba wengine wafurahia kuwa na gari, au kuvaa vizuri! Mimi feeeling ya kuwa niko marekani tu, hata kama choka kiasi gani inanifanya nijisikie "high"
2) Money can buy a house not a home, waweza kuwa na jumba lako masaki na waishia kuogopa kwenda, wakati mie na XXL wangu twakaa kwenye sweet "home' $700/mo! Wengine wanasema money won't buy happiness
3) Katika long term impacts, kuna uwezekano mkubwa wa offsprings wa watu walioko marekani kufanya vizuri/kufanikiwa kuliko wa wale walio Tanzania
...
 
Hapa kila mtu na mtazamo wake, kama ww unaona bongo kunafaa ishi bongo, kama USA kunafaau au ulaya ishi huko. Masiha ni popote pale.
 
FMES

This is a Masterpiece.

- Naomba kuongeza hivi miaka mitano ya kwanza majuu, hasa US lazima uwe umepiga hatua kubwa sana kutoka ulikotoka, kama hakuna hatua huenda ni vyema ukaanza kufikiria kurudi nyumbani kwa sababu ulaya sio ya kila mtu.

- Lakini pia naomba kuwashauri vijana wa sasa wanaokwenda au wenye mpango wa kwenda huko hasa US, jaribu kuuliza, jaribu kutafuta ushauri kabla hujaondoka bongo kwa watu positive waliowahi kuishi huko, usijifanye unajua wakati kumbe kwa standards za US, ukweli ni kwamba hujui kitu kabisaa, usirukie tu mambo kwa pupa.

- US bado ni nchi nzuri pamoja na matatizo yake yote ya kichumi kwa sasa, vijana wengi wa sasa wanajaribu kutafuta njia za mkato, wengine mapak wamejiingiza kuolewa na kina mama wenye uwezo, jamani hatari sana hiyo halafu wengine wamejiingiza kuoa kina mama wa kimarekani, hao ninawapa pole sana, kwa sababu I do not care what unakuwa ume-lost tena bigtime, wengine wamejiingiza kwenye mambo ya ajabu sana hata ni aibu kusema.

- Nenda huko ufanye kazi, kubali kufa kwa sababu ya kufanya kazi, kule hakuna mambo ya kibongo bongo kumbuka ni dunia ya kwanza kule, work hard achana na starehe ambazo huziwezi, wewe bongo kwenyewe starehe hukuziweza sasa utaziweza vipi mwanzoni tu wa kufika US? Achana na kujifanya mnyamwezi kwa sababu haitakuja kutokea mnyamwezi akajifanya mbongo. Nyinyi wabongo hata mjibadili vipi kuwa kama wanyamwezi mbele ya wanyamwezi wenyewe nyinyi ni wabongo tu, hamna mpango.

Twende huko majuu kufanya kazi, sio kutegemea njia za mkato kwa sababu hazipo.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Achana na kujifanya mnyamwezi kwa sababu haitakuja kutokea mnyamwezi akajifanya mbongo. Nyinyi wabongo hata mjibadili vipi kuwa kama wanyamwezi mbele ya wanyamwezi wenyewe nyinyi ni wabongo tu, hamna mpango.

Tuko pamoja hapo, na ninaamini unamaanisha uzito wa hoja hiyo.

Na majuzi nikatoa mifano hai ya watu wanaojitahidi kwa udi na uvumba kujigeuza wazawa, kutopea, kuvaa utamaduni wa taswira ya Umarekani. Ukitoka sehemu masikini, sehemu inayodharaulika, ukawa bado kijana, mgeni mgeni ugenini, ukaonekana umeshuka kwenye boti juzi huna mitindo, umetokea kwa wenye unyuma, basi kama hujui vizuri sifa, thamani, historia ya unakotoka, mara nyingi ni lazima ujikatae. Mpaka jina lako utakataa.

Mimi nakataa kuchukua ubini mpya, napenda kuishi nje ya kasri ya Mwinyi mmiliki, kwenye kibanda cha mtwana.


ept_sports_ncaab_experts-910576787-1239074605.jpg

Hasheem Thabeet gets caught in his girlfriend's sunglasses
By Eamonn Brennan, Yahoo! Sports​
 
thanks ndundunyikanza... Aka bubu asemasema

watanzania wanaopata hiyo mia yako kwa mwaka wapo[ingawa si wengi] na hiyo nusu ndio kabisaaaaaaaaaaaaaaaa kaa kimya!!!

Nipo dar nafanya kazi dar, nalipa nssf dar... Napata zaidi ya 50k dar.... Na katika team niliyopo wapo staff 25 na kati ya hao 12 wanapata zaidi ya 50 k dar

fanya research yako ndio uje hapa na ububu wako kuweka vitu vague ewe michael jordan wa jf
Mkuu naifahamu bongo saana.......hio 50k ina maana kwa mwezi ni more than 4000USD huu ni mshahara wa watu wachache saana tena naweza kusema wale top executive ambapo kuzipata chances kama hizo ama ujulikane undugunization au ulale kwa waganga wa kienyeji......


Maisha sio hela tu, kukwanza kuna rule of law, maji hayakatiki kisenge senge kama bongo, hakuna mgao wa umeme, barabara nzuri, kazi bwerere, shule kwa wenye watoto zipo nzuri tena za public, hewa safi, mademu wazuri, ngoma sio kama bongo, starehe za kumwanga, ukiwa na college digirii basi una uhakika wa kazi hata kama huna makaratsi, public transportation ya kueleweka, misosi ya kumwaga, kuna welfare (kwa wasio jiweza), watu wenye disabilities wanathaminiwa (bongo wana uawa...mfano albinos), hakuna mafuriko baada ya vimvua vidogo kama cha juzi, serikali ni serikali kweli sio uzushi kama wakina Pinda na buraza K, polisi hawaombi rushwa, hakuna malaria wala typhoid na kadhalika kwanina mengine muhimu zaidi ya kuwa na mfuko ulotuna kwa mapesa na ndio maana kila mtu huko bongo ni fisadi kwa upumbavu wenu wa kudhani fwedha ndio kila kitu!
point tupu.....kwa vitu ulivyoviorodhesha hapo nakubaliana na wewe 1000% yaani hivyo ndio hasa vinaniboa kila siku nawaza kukimbia.......bongo unaweaa kuwa na hela kama za MTM sababu ya mfumo hovyoo ukajikuta unakufa bila mungu kupenda kwa kugongwa na mataahira kama chenge....
.......sina cha kuongeza umemaliza kabisa........
 
Last edited:
I can understand hapa kila mmoja anayatazama maisha kinamna yake lakini kuwa na maisha yenye mwelekeo marekani sio lazima uwe educated.Kuna kazi nyingi tu Marekani ambazo hazihitaji hiyo elimu mnayoizungumzia nyinyi zinahitaji maarifa na uhard work wako.Kuna watu wanaingiza six figure na ukiwaona wala huwazanii sema maisha yashawafit kwa kile kipato chao hivyo hiyo six figure inaingia kwenye account leo na week ijayo account nyeupe lakini yote ni maisha.Na overall ni bora ya huku mlio bongo msijidanganye kama kuna mipango yoyote ya kuja huku mnapokuita unyamwezini njooni wala msisite hata kidogo.Hebu niwaulize nyie mlioko hapa America kwani mtu awe na kipato cha kiasi gani kwa mwaka hata mkubali kwamba mambo yake safi ?

SAHIBA.
 
Maskini vijana wetu na mbio za kujihalalishia kuishi nchi za wengine!! Taabu tupu mwajitakia bure!!! Nilikuwa Marekani juzi kwenye mkutano mkubwa tu huko Monterey CA, maprofessa wengi tu wamarekani walikuwepo, na sisi tulikuwa wachache tu kutoka Africa. Nilipata nafasi kutembea tembea kuona hali halisi ya akademia nchini marekani. Sasa kwenye ule mkutano sikuona mswahili ingawaje najua wapo wasomi watz wanaofudnisha nchini Marekani ( ingawaje naambiwa kwenye masomo ya lugha kama kiswahili, wabongo hamwoni ndani ni wakenya!). Nikiri kabisa watz mlio nje, mmekaa kimya mno, hatuwasikii kwenye hata radio mbao za wenzetu, hatuoni chochote mnacholeta huku, zaidi ya malalmiko. Lawama kwamba kuna viongozi mafisadi hapa bongo ni sahihi, lakini sio sababu ya kukufanya usije ukashiriki katika kulisukumu gurudumu. Ingawaje hata wale tuliowaopoa huko tukawapa madaraka hapa nyumbani wamekuwa mstari wa mbele wa kutufisadi, ni hao Balali, Masha na wengine wengi. Inasikitisha kweli!

Kwanza ni muhimu kuelewa kwamba maisha ni jinsi unavyotaka wewe yawe! Huwezi ukatamani tu yakawa mazuri, lazima uyasotee. Kusema sisi tulio hapa TZ ni wazembe, tunalala, sijui tunachukua muda mwingi kupiga gumzo, kula lunch ni kutuonea. Watu tunafanya kazi hadi jumapili, na muda wa kutoka ofisini sio saa 9 ni saa mbili usiku. Labda kwenye section za makarani ambao hawana la maana zaidi ya kuhudumia wateja wa siku. Hatujui holiday, hatujui hata leave za mwaka huwa tunabembelezwa. Sijui mnapata wapi mawazo hayo. Kweli mishahara yetu ni midogo, lakini sis sio wezi au mafisadi. Tunahangaika na hapa nazungumza wale ambao ni wa level yenu, mmesema 'educated TZ' ambao tunachanganya kazi za mwajiri na kazi za public service yaani consultancy. Kwa ajili hio tunaweza kutumia simu za mkono (kwenu ni rahisi lakini hapa walau $100 kwa mwezi kwa matumizi ya kawaida), gari na mafuta yake, kusomesha watoto.

kwa nini ukatafuta vikaratasi tena kupitia vibabu na vibibi, mnajidhalilisha. Njooni nyumbani lakini sio mkakae beach au Rose Garden, you have to be here ready to work 18 hours a day! Kwa nini mnyanyasike kiasi hicho. Angalieni wenzenu wakenya na wasomali na wanigeria, na waghana wanafanya kweli, tunaona matunda ya kazi yao kwa nchi zao, ninyi poaaaaaaaaaaaaaaaa mnalala kibongo bongo bongo, mnisamehe kama nitakuwa nimegusa mioyo yenu
 
thanks ndundunyikanza... Aka bubu asemasema

watanzania wanaopata hiyo mia yako kwa mwaka wapo[ingawa si wengi] na hiyo nusu ndio kabisaaaaaaaaaaaaaaaa kaa kimya!!!

Nipo dar nafanya kazi dar, nalipa nssf dar... Napata zaidi ya 50k dar.... Na katika team niliyopo wapo staff 25 na kati ya hao 12 wanapata zaidi ya 50 k dar

fanya research yako ndio uje hapa na ububu wako kuweka vitu vague ewe michael jordan wa jf

Bongo tunaijua bwana, si wageni wa nchi yetu hadi tufanye research ama sivyo wasomi wetu ambao wengi wangependa kufanya kazi Tanzania wasingekimbia kwenda nchi mbali mbali zikiwemo Namibia, RSA, Botswana, UK, US, Canada n.k.

Wewe uko Bongo lakini unajua kwamba Watanzania wanaopata mshahara kama huo si wengi!! Sijui hizo data ulizipata wapi. Kuna Watanzania wengi sana ambao hawana majigambo wala hawapigi kelele ya jinsi mambo yalivyowanyookea kutokana na elimu zao walizozipata Tanazania au nchi za nje. Kurudi Bongo inataka moyo wa hali ya juu na hizi karaha zisizokwisha kila siku mara maji hamna, mara umeme hakuna mara mafuriko, vyote hivi kama tungekuwa na Viongozi wazuri ni vitu ambavyo tunaweza kabisa kuvimaliza lakini wapi watapanda majukwaani na kupiga alinacha zao huku nchi ikirudi nyuma kila kukicha. Msiwachuuze wenezenu wakafungasha kurudi bongo halafu wakabaki wanajuta kilio cha kusaga meno. Viongozi wakikutana na Watanzania walio nje kila siku hudai kwamba serikali inaweka mazingira mazuri mbali mbali ikiwemo ajira ili mrudi nyumbani lakini miaka inakatika bado hayo mazingira mazuri yamebaki ni alinacha tu.
 
Bongo tunaijua bwana, si wageni wa nchi yetu hadi tufanye research ama sivyo wasomi wetu ambao wengi wangependa kufanya kazi Tanzania wasingekimbia kwenda nchi mbali mbali zikiwemo Namibia, RSA, Botswana, UK, US, Canada n.k.

Wewe uko Bongo lakini unajua kwamba Watanzania wanaopata mshahara kama huo si wengi!! Sijui hizo data ulizipata wapi. Kuna Watanzania wengi sana ambao hawana majigambo wala hawapigi kelele ya jinsi mambo yalivyowanyookea. Kurudi Bongo inataka moyo wa hali ya juu na hizi karaha zisizokwisha kila siku mara maji hamna, mara umeme hakuna mara mafuriko, vyote hivi kama tungekuwa na Viongozi wazuri ni vitu ambavyo tunaweza kabisa kuvimaliza lakini wapi watapanda majukwaani na kupiga alinacha zao huku nchi ikirudi nyuma kila kukicha. Msiwachuuze wenezenu wakafungasha kurudi bongo halafu wakabaki wanajuta kilio cha kusaga meno. Viongozi wakikutana na Watanzania walio nje kila siku hudai kwamba serikali inaweka mazingira mazuri mbali mbali ikiwemo ajira ili mrudi nyumbani lakini miaka inakatika bado hayo mazingira mazuri yamebaki ni alinacha tu.

BAK

Hawa jamaa haina haja hata ya kuwajibu na hawa ndio wale unaowaona humu JF ambao angalau wanaweza kumiliki ama kutumia hizo iternet za makazini na wakirudi majumbani hadi umeme akadiriwe na Tanesco.Tatizo sisi huku hasa hizo habari za mafisadi ndio zinatuchefua kabisa hatujui kama tuwaonee huruma Watanzania ama tuwaache tu maana ni sawa na sikio la kufa.Hawa wenye mawazo haya ni wabinafsi wa hali ya juu na wanajifikiria wao tu na hawajali vizazi vingine,na hili ndio tatizo kubwa la Mwafrica.

SAHIBA
 
.....hii article ni generalization ya hali ya juu,naona kuna kawivu kidogo ka kuwapaka matope jamaa wa unyamwezini,hizo njaa zenu za bongo kaeni nazo na kama maisha ya watu hayaendi vizuri mjue si mtoni tuu tena bongo 99.999% ni njaa tupu na diseases,nina uhakika mpiga box wa unyamwezini anaishi vizuri na kutengeneza $$$ zaidi kuliko mawaziri wenu ambao sio wezi...walioshindwa maisha wengi wao ni matatizo yao wenyewe lakini sio kwa sababu wako unyamwezini,kama waliosoma wanapoteza kazi ni mambo ya kawaida tuu huku na hakuna aibu kufanya kazi mnazoziita za hali ya chini kama mnavyofikiria,unyamwezini ndio mambo yote huko bongo mnajidanganya tuu!

Thank you, Well said! hapa ndipo utakapoona jinsi wabongo walivyo na ntimanyongo...Wana wivu wa hali juu!!!! Na kutaka kusema vitu ambavyo hawajui lolote au kutumia mifano michache na kutaka kuifanya mifano hiyo michache ni 100% ya hali halisi za Watanzania wote!!!
 
Kama una make kilo au nusu kilo "mnyamwezi" kwa mwaka, who gives a https://jamii.app/JFUserGuide!? Thread imejaa majigambo na kandia zisizo na sababu za msingi..wandugu eenh tena kwa SAUTI KUBWA, kila mtu na maisha yake kivyake! Watu wanalosti US, watu wana losti bongo, watu wana fanikiwa US, watu wanafanikiwa bongo..ni ishu ya mtu binafsi jinsi anavyozichanga karata zake! Maisha unyamwezini matamu bana aaahaggg, kwanza kuna rule of law, maji hayakatiki kisenge senge kama bongo, hakuna mgao wa umeme, barabara nzuri, kazi bwerere, shule kwa wenye watoto zipo nzuri tena za public, hewa safi, mademu wazuri, ngoma sio kama bongo, starehe za kumwanga, ukiwa na college digirii basi una uhakika wa kazi hata kama huna makaratsi, public transportation ya kueleweka, misosi ya kumwaga, kuna welfare (kwa wasio jiweza), watu wenye disabilities wanathaminiwa (bongo wana uawa...mfano albinos), hakuna mafuriko baada ya vimvua vidogo kama cha juzi, serikali ni serikali kweli sio uzushi kama wakina Pinda na buraza K, polisi hawaombi rushwa, hakuna malaria wala typhoid na kadhalika kwani uroda ni mwingi mno kuuorodhesha wote hapa! Maisha sio hela tu, kuna mengine muhimu zaidi ya kuwa na mfuko ulotuna kwa mapesa na ndio maana kila mtu huko bongo ni fisadi kwa upumbavu wenu wa kudhani fwedha ndio kila kitu!

Hivyo vijisenti ( $50,000) kwa mwaka vya MTM mtu yeyote hapa unyamwezini mwenye bidii ya kazi anavitengeneza tena kwa kubeba boksi tu..ebo!

Maindini maisha yenu, acheni kutaka kujua na kufuatilia maisha ya wengine kwani huo ni uswahili na ndio hasa unaokimbiza wengine nje ya bongo! Hooovyo!

Pambaf..mnaboa kwa ujuaji!

Mods pls fanyeni kazi yenu tunayowaaminia.
 
Kama una make kilo au nusu kilo "mnyamwezi" kwa mwaka, who gives a https://jamii.app/JFUserGuide!? Thread imejaa majigambo na kandia zisizo na sababu za msingi..wandugu eenh tena kwa SAUTI KUBWA, kila mtu na maisha yake kivyake! Watu wanalosti US, watu wana losti bongo, watu wana fanikiwa US, watu wanafanikiwa bongo..ni ishu ya mtu binafsi jinsi anavyozichanga karata zake! Maisha unyamwezini matamu bana aaahaggg, kwanza kuna rule of law, maji hayakatiki kisenge senge kama bongo, hakuna mgao wa umeme, barabara nzuri, kazi bwerere, shule kwa wenye watoto zipo nzuri tena za public, hewa safi, mademu wazuri, ngoma sio kama bongo, starehe za kumwanga, ukiwa na college digirii basi una uhakika wa kazi hata kama huna makaratsi, public transportation ya kueleweka, misosi ya kumwaga, kuna welfare (kwa wasio jiweza), watu wenye disabilities wanathaminiwa (bongo wana uawa...mfano albinos), hakuna mafuriko baada ya vimvua vidogo kama cha juzi, serikali ni serikali kweli sio uzushi kama wakina Pinda na buraza K, polisi hawaombi rushwa, hakuna malaria wala typhoid na kadhalika kwani uroda ni mwingi mno kuuorodhesha wote hapa! Maisha sio hela tu, kuna mengine muhimu zaidi ya kuwa na mfuko ulotuna kwa mapesa na ndio maana kila mtu huko bongo ni fisadi kwa upumbavu wenu wa kudhani fwedha ndio kila kitu!

Hivyo vijisenti ( $50,000) kwa mwaka vya MTM mtu yeyote hapa unyamwezini mwenye bidii ya kazi anavitengeneza tena kwa kubeba boksi tu..ebo!

Maindini maisha yenu, acheni kutaka kujua na kufuatilia maisha ya wengine kwani huo ni uswahili na ndio hasa unaokimbiza wengine nje ya bongo! Hooovyo!

Pambaf..mnaboa kwa ujuaji!

Mkuu umeshasema thread imejaa ujuaji... halafu na wewe unaweka ujuaji!! sijui umegain nini!!???

To be honest, i work for the government so that money is impossible.. the motive was to highlight that even 50k is available in poor tanzania because 80% ya contribution humu ndani ni negative about our Tanzania

Yourname is Mine.. why does it hurt so much!!? your posts exposes a deep rooted slave who would say anything to disguise his/her home and family... naifananisha na mwana anayeshinda kwa mjomba kwasababu ya vitu na wanaangalia TV na yuko tayari kubadili ubini wake ili tu asifanane na kwao kwenye taa ya chmli

Halafu, Pumbaf mwenyewe kwa ujuaji
 
Mkuu naifahamu bongo saana.......hio 50k ina maana kwa mwezi ni more than 4000USD huu ni mshahara wa watu wachache saana tena naweza kusema wale top executive ambapo kuzipata chances kama hizo ama ujulikane undugunization au ulale kwa waganga wa kienyeji......



point tupu.....kwa vitu ulivyoviorodhesha hapo nakubaliana na wewe 1000% yaani hivyo ndio hasa vinaniboa kila siku nawaza kukimbia.......bongo unaweaa kuwa na hela kama za MTM sababu ya mfumo hovyoo ukajikuta unakufa bila mungu kupenda kwa kugongwa na mataahira kama chenge....
.......sina cha kuongeza umemaliza kabisa........


Yo Yo, at least you have taken a better approach to a very provocative post... its is true that the average pay in TZ is still below 500USD per month but it is wrong to say that everything bad is in Bongo and 50K are available and not uncommon... there are good things and more opportunities come our way everyday WE SEE THEM AND SOME SEIZE THEM PERIOD!!

Yes there re risks and we face them everyday and wont stop because its a route a nation has to follow to reach promised land, but this is everywhere and if all of us decide to abandon TZ like one YNIM [even using foul language for his/her motherland], sijui kama tutakuwa tunasaidia ndugu zetu

If all of us agree on everything... then JF would be very boring
 
Nadhani hii thread ingeitwa "TZ Immigrants come to the US with unrealistic expectations" ingekua accurate zaidi.
 
Huku Taifa linawahitajia kutowa mchango wao kwanini wasirudi hapa nyumbani ?mara kwa mara viongozi wetu wamekuwa wakiwashauri ndugu zetu walio nje ya nchi kurudi nyumbani na kulijenga taifa hili ambalo bado changa .Rais siku zote katika matembezi yake huko ulaya na marekani amekuwa na jitihada za kuwaeleza ndugu hao umuhimu wa kurudi nyumbani .
 
Niliondoka Tz kwa hiari yangu mwenyewe nitarudi kwa hiari yangu mwenyewe.
Rais hajui kilichotuleta vipi aingilie kati kututaka turudi?

Kama ni msoto, mbona upo kila mahali?

Hapa tunabeba mabox na kufagia vyoo lakini hatuadhiriki na kubomu kila mtu au hatuli kwa shangazi na mjomba.
Kizuri zaidi hizo coin wanazotupa mwisho wa mwezi zimeweza saidia wazee wetu waliostaafu na kulipwa pensheni mbuzi kule Malinyi.

Heri lawama kuliko fedheha.

WOTI IZI BAITINGI YU GAIZI?? WI A LEYING DAUNI HIA CHILLING BATI YU SIIM TU MAINDI.

HUAI A YU GETTING BANIDI WITH ZE PEPA WHICH IZI IN ZE FILDI???? EEH?

AZA PIPO BWANA!!!
 
1. Yaani mimi na mara ya kwanza kuona Mtanzania anakosa uzalendo na kusifu US au UK-a developed country kuliko home for whatever reasons!

Mkiona vinaelea basi vimeundwa!

Karibuni sana nyumbani ndugu zangu..bado ni nyumbani kwenu tu ni sehemu ya historia

yetu!

Karibuni Supu tam ya Kuku wa Kienyeji, Kongoro safi na mengine mengi tu mazuri tele!

2. Tz imebadilika sana na opportunities kibao tu! Wako wengi wameishi nje mda mrefu na kurudi Bongo na kuwa challenged na makubwa peers wao walioyafanya kwa mda mfupi bila hata kuiba!

3. Maendeleo ni popote tu duniani..sema uskae ukadharua nyumbani na wazee na mila

zetu! Wazee husema "Mpanda ngazi hushuka"!
 
kweli nyumbani ni nyumbani, lakini tanzania nako MH!!!!!! Ufisadi mwingi. USA na Ulaya kuna unafuu.
 
Back
Top Bottom